Dah ama kweli wewe mgumu sana kuelewa mapana ya Muungano..Yaani wewe na mkeo akipewa fedha toka nje azilete tu ndani ya nyumba na halali yake?. Ebu kwa kiola unapofikiria jambo iweke ndoa yako na mkeo halafu ndio ujue yapi na mke na yapi na ya ndoa ruksa.. Na labda nikuulize MEMBE Ni nani? anaiwakilisha serikali ya bara au ya Muungano? iweje swala hili liwe na Zanzibar ikiwa wawekezaji wote nchini wanapitia njia hiyo hiyo. Nini azma yao na deni hili litawahusu kina nani ikiwa Zanzibar inajulikana sio Nchi nje ya Muungano wetu. Mwinyi alipowauzia Saidia Loliondo ilikuwa kaingilia maswala ya bara?..Hivi rais akitokea Zanzibar hawezi kuweka ama kukataa misaada na mikataba inayohusu Bara!..Maswala yanayohusu serikali ya Mapinduzi Zanzibar Serikali ya muungano inayaingilia kati yapo mengi tu mojawapo ni hii hapa : Membe akalia 200bn za Zanzibar Bonyerza hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/303380-membe-akalia-200bn-za-zanzibar.html Mkuu Mkandara
labda nikwambie hivi hata Marekani kwenyewe walioanza kabla yetu Sii Senator, Governor wala Member wa Congress anaweza kwenda nje na kuweka mikataba ya aina yoyote wala kupokea misaada toka nje pasipo kupitishwa na serikali kuu. Mkuu mahusiano yoyote ya kimataifa ni lazima yapitie Ofisi wa Membe maana ndiye mwakilishi wetu sote. Mama Clinton majuzi alikuwa Malawi anawakilisha Marekani na hadi zozote anazozitoa zitawahusu Wamarekani wote..
Hivi kuna tatizo gani kwa Zanzibar kupitia serikali ya Jamhuri ya muungano kuwawakilisha ktk mikataba yake nje ua mpaka awepo Mzanzibar ndio mnaiona haki..Rais kachaguliwa na sisi wote iweje nyie mjiweke kimbelembele kwenda kuweka mikataba ambayo inahusu zaidi mahusiano yetu KITAIFA. nani huko anaijua Bendera ya Zanzibar au Tanganyika!
Hawa walioleta hiyo misaada walielewa vizuri sheria na walijua ktk kutaka kugombanisha serikali hizi mbili ni kuonyesha lengo la kutoa fedha kwa serikali ya Zanzibar wakati wanajua fika haiwezekani huu sio Utawala wa Kisultan ambao Sultan wa UAE anaweza kuweka mikataba pasipo Sultan wa Dubai au Sharja kuhusika. Hii ni serikali ya JAMHURI babuu mbona hamuelewi.
Wewe hapo ulipo unaweza kabisa kupinga mkopo wowote unaotolewa ama kupokelewa kutoka nchi ambazo zinalenga kuharibu mahusiano ya muungano wetu...Hao Oman watoe misaada kwetu wakati maisha yao wenyewe yanawashinda, Oman wana struggle kiuchumi hizi sadaka zimetokea wapi. Wazanzibar waliohamia huko tu wanabaguliwa na hata kupewa Soweto yao leo wawe na huruma sana kwa Zanzibar....