Kha..! Nyie BAKWATA kulikoni..?

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama mwezi uliwahi kuondoka kwenye mhimili wake hata usionekane.

Wanasayansi wapo siku zote na mkitaka kuamini waulizeni kama walishawahi kutouona. Na sii kuuona tu hata ukitaka kwenda kutalii huko mwezini watakupeleka.

Sio vizuri kuwaita viongozi wa dini ambayo huiamini wapumbavu hawa.... Ukiangalia sana BAKWATA wanafuata maelezo ya vitabu, wengine wanafuat Jografia na busara za maendeleo ya teknolojia. wote wako sawa kwa imani zao

Vitabu gani wanavyofuata? Baadhi ya watu (wanafunzi na mwalimu wao I think) walioko Kibiti-rufiji huko walishuhudia mwezi na wakamwambia shekhe wa Bakwata wa wilaya hiyo na waliosema ni watu wenye akili timamu na ni wa-amini katika imaan ya kiislamu na wakashuhudia kumwogopa Mwenyezimungu lakini shekhe huyo wa bakwata hakutake action yoyote. Ni vitabu gani vya hadith wanavyofuata. Na Bakwata walipokubaliana kushirikiana katika kuandama kwa mwezi kwa kutumia kanda wanapata wapi-Kenya na Tanzania wawepo katika ushirikiano huo na somalia wasiwepo, then itokee Mtwara uonekane mwezi na kenya wakakubali kutokana na tangazo la bakwata but somalia hawajauona; je waweza kupata picha wale wakaazi wa mpakani baina ya somali na kenya watakavyokuwa treated. Wapi tofauti ya mipaka iliyobuniwa miaka ya ya 1800 ilikuwa factor katika maamuzi ya masuala ya kiislamu?

Ndio natoka home kuelekea kazini lakini misikiti ya karibu yangu wanaswali eid??!

Walikuwa wanapata maamuzi kutoka Serikalini wakati wa Nyerere, kwa sasa wanapata kutoka kanisani!

Shenzi mkubwa wewe? upumbavu wenu na kutokuwa na mshikamano na kutotumia akili, bado manatafuta mchawi wenu nani? shenzi kabisa, kanisa lina husika nini na ushenzi wenu. kwani kanisa ndo ninatoa mwezi?

Hapa ndo naona rangi halisi!
Faiza foxy analaumu kutoonekana kwa mwezi na kutotangazwa na Bakwata kuwainasababishwa na wakristo?
Nitashangaa sana kama kuna waislam wanaokubaliana naye. waislamu naowajua mimi they cant take that shit.

endeleeni na kufunga kesho ndio idd bila kuwa na mashaka tena.wengi tulijua ni j5. west africa ndio wanashehereka leo.

Mkuu, dini hii haiendeshwi kwa website kama wataka hivyo angalia ushuhuda bac kupitia hizo website then uangalie which one can be accepted under the muslim shariah! Je Unakumbuka kuwa iliwahi kutokea shakhe mkuu wa bakwata aliwaomba radhi waislamu kwa kuwa waliwaambia mwezi haujaandama na watu wakala siku ya kwanza ya kuingiya ramadhani hali ya kuwa mwezi ulionekana maeneo kadhaa ya huko tz, so akawaambia wailipe siku hiyo. Na kule zenj pia unakumbuka tukio kama hilo lilitokea. Tatizo la Bakwata sawasawa na magamba, elimu wanazo lakini hawataki kuifanyia kazi elimu hiyo, na M/mungu atawauliza sawasawa wenye elimu kisha wakashindwa kuitumia elimu hiyo. Swali kwako mkuu:- Kwa kuwa Msikiti wa Mtume Madinna leo wameswali idd, je ingelikuwa mtume yu hai, yeye ndiye (possibly) angeliswalisha swala ya idd, Je Bakwata wangelikuwa wanamfuata nani? Jitahidi usome dini yako na elimu utakayopata uitumie ipasavyo mkuu.

Eid moon sighted by Peshawar Ruet body | Newspaper | DAWN.COM

Tatizo Mkuu hapa utaambiwa una itikadi kali !

Hivi wewe unajua Uislam kweli au unaleta porojo zako za CCM!

Kwa taarifa yako kesho dunia nzima ni EID kasoro Tanzania tu. Usipotoshe watu hapa JF, hao BAKWATA wako nani kawapa mamlaka ya kuwasemea Waislam wa Tanzania! Ningekujibu zaidi sema hapa sio mahali pake, ebu pitia hii site uone kesho ni siku gani kwa Waislam dunia nzima. www.isna.net

Chonde chonde kwenye mas'ala haya ya ibada!.
Bakwata si wanaotuongozea ibada!.
Wala si lazima kua na ibada kwa wakat mmoja. Tatizo hamsomi mas'ala haya kwa undani. Hapo hakuna tatizo kabisa wewe kama umeona ukila leo ndio utakua umepatia vile umeungana na waislam wengineo fanya hivyo. Lakin ukumbuke ibada kubwa ni swala katika uislam ila unaiswali tafauti kila siku na waislam unaowafuata leo ulimwenguni...sasa sijui hili nalo utasemaje?
Mwezi wa kiislam hauna siku 31 leo tunakamilisha 30 kuna tatizo gani? Pia kenya nao wamefunga leo. Tatizo mnahamasisha watu ili muendane na wakiristo...sasa sijui kawafundisheni nani?

Ndio maana wanafanya njama kuhakikisha waislam wanfarakana katika kila jambo hata katika ibada zao.
Zote ni athari za mfumo kristo ila mwisho wake unakuja karibuni.

Hapo umetuboa!no sense na uwatake radhi wakristo kama waislamu wana matatizo yao ni high time ya kuyashughulikia si kusingizia wasiokuwemo
Kwanza kiongozi wa nchi mwenyewe muislamu na kazi yake siku hizi ni kufuturisha, mfumo kristo kivipi?

PESHAWAR: Khyber Pakhtunkhwa and tribal areas will keep up their tradition of two Eids thanks to an announcement by the maverick. "Ruet-i-Hilal committee" based in the Qasim Ali Khan mosque said that moon had been sighted on Monday.
Saudi Arabia, the UAE, Qatar and Egypt will also celebrate Eidul Fitr on Tuesday.
Mufti Shahabuddin Popalzai, who chaired a meeting of the committee, proclai-med that Eidul Fitr would be celebrated on Tuesday as sufficient evidence about sighting of the Shawwal moon had been received from different areas of the province.
"About 10 people appeared before the Ulema and gave convincing evidence about moon sighting," he told media after the meeting.
Ulema in Mardan, Bannu, Charsadda, Bajaur Agency and North Waziristan followed the Peshawar-based body`s announcement with their own declarations that Eid moon had been sighted on Monday.

Hapa pana utata kabisa kwani leo Makkah leo wamesherekea na kuswali Eid mubarack ata London angalia ata Islamic channel.Je kila bara lina Eid yake?Ndugu waisilam nipeni elimu kuhusu ili.

Ulivyoanza maelezo yako nilifaham mwisho lazima ujichanganye!
Mwezi una hisabu zake nawe wafunga kwa kufuata hizo siku. Sio lazima wakiswali makkah au indonesia watu wote waswali idi.
Hapo ndipo hujua uelewa wa wachangiaji unapoanzia...
Tazama katika uislam ibada muhim na ngumu kuliko zote ni swalat lakin ibada hii inaswaliwa kutokana na masaa ya eneo husika mbona hamjasema kuna swalat ngapi????
Umuhim ni hizo siku ulivyoanza kufunga na utavyomaliza kufungua.
Wala halina maelezo na hujja nyingi kama wengi wanavyohiaji kulizungumzia. Hapo hakuna utata...ndio maana wasomi wakubwa hawawezi jadili hilo...linabaki kwenu wachache wa ilm hiyo!
Ndio muingie madrasani mjifunze vizuri.
Tena kwenye majamvi ndio penyewe!

moon-sighting-ap.jpg-543.jpg
"Ruet-i-Hilal committee" based in the Qasim Ali Khan mosque said that moon had been sighted on Monday. - File Photo

Jana watu wengi waliamini kuwa leo ni sikukuu, na hii ilitokana na baadhi ya vyombo vya habari hasa vya dini ya kiislam kutangaza kuwa mwezi umeandama hivyo leo ni sikukuu ya eid. Pamoja na kuwa mimi sio mwislam lakini kutokana na vyombo hivyo kutangaza na kuweka nyimbo na mawaidha tuliyozoea kuyasikia wakati wa wa mwandamo wa mwezi sikuwa na shaka ila swali kubwa nililokuwa nalo ni je vyombo hivyo ndiyo vyenye mamlaka kutangaza tukio kubwa kama hilo?

Inawezekana kweli mwezi umeandama ila ninachoamini mimi ni kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza tukio hilo bila kutiliwa shaka ni BAKWATA au mtu aliyepewa mamlaka na BAKWATA, pia naamini kuwa BWAKWATA hawawezi kutangaza mwandamo wa mwezi bila kupata taarifa kutoka kwenye chanzo kinachoaminika. Bila kuthibiti mambo kama haya itakuwa ni mvurugano na kujichanganya. BAKWATA Isilaumiwe kabisa kwa hili kwani hicho walichokifanya ni fundisho tosha kwa watu wasiopenda utaratibu na kufanya mambo bila kufanya utafiti n kujiridhisha kwa hali ya juu.

Hili liwe ni fundisho si kwa hao waliojitangazia sikukuu bali kwa watu wote wasiopenda utaratibu.Ni wakati muafaka kwa serikali kuweka sheria kali zinazohusu uhalali wa kutoa matamshi kwa mambo yanayogusa maslahi ya taifa na jamii kwa ujumla, kama mambo haya hayatadhibitiwa kuna siku vyombo ya namna hii vitatangaza kuwa nchi imepinduliwa au imetekwa au tumevamiwa maana hakuna sheria inayoweka mipaka na kama ipo basi serikali imekuwa kimya kwani baadhi ya redio hizo zilizotangaza sikukuu zimekuwa na tabia ya kutoa matangazo ambayo ni ya kuwagawa wananchi lakini sijasikia hata siku moja kiongozi yeyote akikemea au kuzikosoa.

Kwa hili la kutongaza mwandamo wa mwezi, walichokifanya BAKWATA ni sahihi kwani kama watakaa kwa kufuata taasifa za redio mbao watajivunjia heshima.

Nawatakia waislam wote wanaopenda utaratibu Eid njema!!

Tatizo Mkuu hapa utaambiwa una itikadi kali !
Hata wenye akili kali si ndo wanaofaulu madaraja ya juu! Magamba tu kampeni yao ya kufarakanisha watu.
Mwenyezi Mungu katika surat Yunus aya ya 5 anabainisha kuwa mwezi hupita katika vituo vyake ili kutokana na hilo watu wajue hisabu za nyakati( idadi ya siku na miezi na miaka). then ifahamike kuwa idadi ya vituo hivyo ni 28, yaani 14 kila upande hivyo baada ya siku ya 29 ni siku ambayo mwezi utakuwa less visible na siku inayofuata utaanza kituo chake kipya. Ndipo mtume akasema funga ni siku 29, la kama hamkuuona (kutokana na sababu mbalimbali, na ukumbuke katika kipindi hicho kupata habari ni suala la barua inayopelekwa kwa masiku kadhaa) tofauti na siku hizi. Pia ifahamike kuwa kuuona (shahida)kulikokusudiwa hapa ni kushuhudia/shahidi bimaana ikiwa tu baadhi ndio waliouona na wameshuhudia hata wale ambao hawakuuona wanalazimika kufuata mwandamo huu. La ikiwa kuuona huku si kwa kushuhudia vipi ya wale ambao wana ulemavu wa macho. Kumbuka kwamba hii hesabu ya kukamilisha 30 inategemea na environment/geographical features and weather conditions. Kwani ni possible kutokana na mazingira ya kijiografia na hali ya hewa inawezekana eneo fulani wanaweza kuuona mwezi na jingine wasiweze kuuona, hivyo ni wajibu kwa waliouuona wawambie wale wasiouona ili nao wafuate. Sasa hili kama nilivyosema mwanzo, kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni vigumu kupashana habari ndani ya saa 24 lakini kwa sasa ni suala la seconds. So why Bakwata mnataka kuipotosha dini hii na kuyumbisha watu. Mwisho Kifo cha Bakwata kitakuwa kama kifo cha ccm, watu hawatakubali kila siku kuwayumbisha.

Hapo ndio utajuwa kwanini Waislaam tunataka kadhi na mahakama ya kadhi virudishwe, vilikuwepo vikaondolewa na nyerere kwa udini wake.

na mimi sasa naanza kuchanganyikiwa na huu mwezi maana naona hizi observations zina 'ukweli' usio rasmi! Lakini katika ulimwengu wa sasa ni kiasi cha kukubaliana tu kuwa Makao Matakatifu kwa kuwa ni Makka basi tusijari kama tumeuona au la bali wenyewe wakishirikiana na wataalamu wa mambo ya anga, kwa maana ni kweli kwamba mwezi haujawahi kupotea bali upo siku zote.
...hizi ni changamoto za imani katika karne ya 21!!
Sidhani kama mwezi uliwahi kuondoka kwenye mhimili wake hata usionekane.

Wanasayansi wapo siku zote na mkitaka kuamini waulizeni kama walishawahi kutouona. Na sii kuuona tu hata ukitaka kwenda kutalii huko mwezini watakupeleka.
[RINGO EDMUND[/URL said:
[/U];2424893]waulizeni dada zetu kama wameuona tuanze kupiga mambo.

Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom