Kesi za ulawiti hasa kwa watoto wadogo zimekithiri sana. Hatua gani kali zifanyike? Kwanini sheria imepooza katika hili?

Guantanamoh

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
2,367
4,808
Habari wadau.

Hivi sasa ni saa 01:40 usiku wa manane sijalala naumia na kuumiza kichwa hivi hizi kesi za kulawiti kwanini zimekithiri?

Wanaume wamefikia hatua wanalawiti watoto wa miaka mitatu, wazee wasiojiweza na hata wagonjwa walio pooza. Wanalawiti wanawake kwa wanaume bila huruma!!

Jamii inawajua hawa walawiti na inawakingia kifua?

Je? Ni sheria zimelega sana ndo maana watu wanafanya wakijua sheria ina lacuna?

LHRC, mbona juhudi zenu zipo kwenye reaction za wananchi tu? Yani huwa mnasubiri msikie mwanaume mmoja alilawiti mtoto wananchi wenye hasira kali wamemchoma moto au msikie walawiti wameanza kukatwa jinsia zao au hadi msikie wamepangwa mlimani wanafyatuliwa shaba kichwani ndo huwa mnaibuka na kukemea wanachokua wamefanyiwa.

Inaumiza sana na haya matukio. Yani watoto ndo inauma sana. Kila siku unasikia jipya,

Je nguvu ni ile kauli ya kwamba “mwanaume ndo alivyoumbwa hawezi kujicontrol hisia? “ kwahiyo ndo ulawiti mtoto?

Sheria gani kali iundwe ili iwe fundisho la mfano. Mnaharibu kizazi chetu.
 
Kuna Iman za kishirikina hapo zinachangia pia,eti ukitaka kuwa Tajiri lawiti Mtoto.
Kuna haya mapicha machafu ya ngono Kila MTU anaangalia Yana mtia nyege anaishia kulawiti
Sheria yetu ni capital serikali ishikilie hapo hapo hakuna kulegeza ili kutokomeza unyanyasaji

Siasa kwenye kukemeea hayamquchafu juzi hapa naibu waziri katuhumiwa kulawiti Kwa chupa,Rais kamtumbua lakini DPP analeta sarakasi za kulindana. Unajiuliza vp Watu wabakaji, wafiraji,wenye fedha hawawezi kuinunua mahakama na dpp

Cha kushangaza ukienda magereza wabakaji na wafiraji wa watoto wadogo wamejaa wengi mpaka unashangaa hivi Watu hawaogopi miaka 30
 
Kwa kweli hili ni janga kubwa, Sheria ya kifungo cha miaka 30 si haba, lakini unatakiwa msisitizo Kwa jamii wa namna ya kuwalinda vijana wadogo.
Kwanini isitungwe sheria ya kunyongwa hadharani? Yaani mtu amebaka mtoto wanampeleka mahakamani wanampa na dhamana. Ya nini? Hili suala la haki za binadamu ifike pahala wawachukulie wahalifu wa makosa haya kama part ya armed robbery! Wasiwe na dhamana. Yani ukiingia jela iwe ndo kimoja! Taifa linaangamia! Baada ya miaka 20/30 wanaume marijali watapungua kwa asilimia kubwa sana kwasababu waliharibiwa utotoni.

Sheria mpya iundwe na iwe ya kutisha kwelikweli
 
Kuna Iman za kishirikina hapo zinachangia pia,eti ukitaka kuwa Tajiri lawiti Mtoto.
Kuna haya mapicha machafu ya ngono Kila MTU anaangalia Yana mtia nyege anaishia kulawiti
Sheria yetu ni capital serikali ishikilie hapo hapo hakuna kulegeza ili kutokomeza unyanyasaji

Cha kushangaza ukienda magereza wabakaji na wafiraji wa watoto wadogo wamejaa wengi mpaka unashangaa hivi Watu hawaogopi miaka 30
Na cha kushangaza, wengine wanafanya hivyo vitendo, bado wapo mtaani na wanakingiwa vifua.
 
Ushirikina ndio chanzo cha huo ujinga wote.

Bado jamii yetu kwasasa ni PRIMITIVE, Kudeal na watu primitive inapaswa kuhakikisha watu wote wanakwenda shule au ukatili, kila anayebainika na ushahidi upo usio na shaka auwawe tu.
Ifike pahala haki za binadamu zisiwe na double standards. Yani matukio kama haya huwasikii wakipiga kelele ila wanasubiri reaction mbaya ya wananchi ndo inawauma.

Mfano mtu kalawiti anatundikwa uwanja wa taifa pale anachapwa viboko hadi anachakaa alafu ndo anaingia jela sasa yani bila ukatili hatutafika. Inaumiza sana
 
Habari wadau.

Hivi sasa ni saa 01:40 usiku wa manane sijalala naumia na kuumiza kichwa hivi hizi kesi za kulawiti kwanini zimekithiri?

Wanaume wamefikia hatua wanalawiti watoto wa miaka mitatu, wazee wasiojiweza na hata wagonjwa walio pooza. Wanalawiti wanawake kwa wanaume bila huruma!!

Jamii inawajua hawa walawiti na inawakingia kifua?

Je? Ni sheria zimelega sana ndo maana watu wanafanya wakijua sheria ina lacuna?

LHRC, mbona juhudi zenu zipo kwenye reaction za wananchi tu? Yani huwa mnasubiri msikie mwanaume mmoja alilawiti mtoto wananchi wenye hasira kali wamemchoma moto au msikie walawiti wameanza kukatwa jinsia zao au hadi msikie wamepangwa mlimani wanafyatuliwa shaba kichwani ndo huwa mnaibuka na kukemea wanachokua wamefanyiwa.

Inaumiza sana na haya matukio. Yani watoto ndo inauma sana. Kila siku unasikia jipya,

Je nguvu ni ile kauli ya kwamba “mwanaume ndo alivyoumbwa hawezi kujicontrol hisia? “ kwahiyo ndo ulawiti mtoto?

Sheria gani kali iundwe ili iwe fundisho la mfano. Mnaharibu kizazi chetu.
Pole sana. Wewe uko kama mimi. Hili limekuwa kamamoja ya sehemu za utamaduni wetu. Kuna sababu nyingi.
1. Watu kuzaa hovyo huku wakiwa hawana muda wa kuwalea watoto kwa sababu ya kukimbizana na maisha magumu.
2. Ndoa nyingi kuvunjika na kuacha watoto walio na single parents.
3. Kushamiri kwa imani potofu za ushirikina zinazoachiwa zienee kwa kasi kwenye social media na vyombo vya habari
4. Jamii kutokuchukuwa hatua mara wanapoona viashiria vya unyanyasaji wa watoto.
5. Serikali iliyoshindwa kila kitu na muda mwingi unatumika kwenye kulaghai wananchi kwa sababu haina majibu wala vision ya kuondoa matatizo
6. Jeshi la polisi mahakama vililojaa rushwa kuachia watuhumiwa wanapokamatwa
7. Rais wa nchi anayeachia mambo yajiendee yenyewe, asiye na ushawishi na anayedharaulika na walio chini yake (unakumbuka yule kijana wa Babati na ushahidi wa alichofanyiwa na mbunge lakini rais akamlinda?)
 
Pole sana. Uwe uko kama mimi. Hili limekuwa kamamoja ya sehemu za utamaduni wetu. Kuna sababu nyingi.
1. Watu kuzaa hovyo huku wakiwa hawana muda wa kuwalea watoto kwa sababu ya kukimbizana na maisha magumu. 2. Ndoa nyingi kuvunjika na kuacha watoto wasio na single parents. 3. Kushamiri kwa imani potofu za ushirikina zinazoachiwa zienee kwa kasi kwenye social media na vyombo vya habari 4. Jamii kutokuchukuwa hatua mara wanapoona viashiria vya unyanyasaji wa watoto. 5. Serikali iliyoshindwa kila kitu na muda mwingi unatumika kwenye kulaghai wananchi kwa sababu haina majibu wala vision ya kuondoa matatizo 6. Jeshi la polisi mahakama vililojaa rushwa kuachia watuhumiwa wanapokamatwa 7. Rais wa nchi anayeachia mambo yajiendee yenyewe, asiye na ushawishi na anayedharaulika na walio chini yake (unakumbuka yule kijana wa Babati na ushahidi wa alichofanyiwa na mbunge lakini rais akamlinda?)
Basi wananchi waachiwe wafanye wanachotaka ili kulinda kizazi chetu
 
Ushirikina ndio chanzo cha huo ujinga wote.

Bado jamii yetu kwasasa ni PRIMITIVE, Kudeal na watu primitive inapaswa kuhakikisha watu wote wanakwenda shule au ukatili, kila anayebainika na ushahidi upo usio na shaka auwawe tu.
Kwa kiasi nakubaliana na wewe hasa hili la ushirikina. Lakini tungekuwa na viongozi wenye nia ya kuongoza hili ni tatizo ambalo linaweza kudhibitiwa. Ilivyo sasa hivi ni kama viongozi wanaachia mambo yafanyike bila kujali. Rais ndiye kabisaa, huwezi kujua ni rais mwanamke kwa sababu katika marais wote waliopita, hivi vitendo vimeshamiri zaidi kwenye hii awamu yake na yeye yuko kimya kama haoni.
 
Wananchi hawajakatazwa kufanya watakalo. Nadhani kuna tatizo la mass ignorance. Wananchi wakiamua, kwa muda wa mfupi kabisa haya mambo yataisha.
Nasema ole wao hao haki za nini wanyanyue midomo wananchi wakichoka!

Mimi nimestuka kuskia walivo react makonda kumdhalilisha yule dada, yani hivyo ndo vity vya kushupazia sauti saizi kweli? Kesi za ulawiti zipo kibao ila wanasubiri zenye public sympathy.
 
Back
Top Bottom