Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Hawa wamekuwa wakigawana mapato dhalimu hivyo hakuna ambaye angeripoti mwenzie.Hili ni jeshi la polisi au jeshi la manyang'au. Mheshimiwa Masha, safisha hilo jeshi la majambazi.
Kuna jamaa aliniambia mauaji ya namna hii yako mengi tu na huko nyuma raia wengi walikuwa wanauawa kwa njia kama hizi na mapolisi fisadi.
Huyo Zombe sio tu afungwe lakini wataifishe hata mali zake zote.
Pia inaelekea jeshi letu la polisi halina maadili kabisa. Mkuu anakuambia kaue na unaenda kweli kuua, kwanini? Je hakuna sehemu kwa kwenda kutoa siri kimya kimya na kuokoa maisha ya raia wema?
Amini usiamini wameuawa wengi tu ka njia hii. Na hasa kwa kisingizio cha ujambazi.