Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Sina mamlaka ya kumhukumu mtu na wala sitahukumu, lakini jamii inajiuliza, iweje hawa wawe huru wakati miongoni mwa washtakiwa mahakama ilikiri kuwa walikuwepo waliokuwa eneo la mauaji msitu wa Pande, Mbezi Luis, jiji Dar es salaam siku ya mauaji hayo January 14, 2006.

Wananchi wanajiuliza, imethibitika bila kuacha shaka yoyote kuwa waliouawa hawakuwa majambazi. Imethibitika bila kuacha shaka yoyote kuwa waliouawa walikamatwa wakiwa hai mbele za watu, walifungwa pingu. Imethibitika bila kuacha shaka yoyote kuwa wakiwa hai waliwapeleka msituni Pande, imethibitika bila kuacha shaka yoyote kuwa walirudishwa kutoka msitu wa pande wakiwa maiti.

Katika hukumu yake, Jaji Massati alisema mahakama imeridhika kuwa wafanyabiashara watatu na dereva taksi mmoja waliuawa kwa kupigwa risasi kikatili kwenye msitu wa pande. Hakuishia hapo, alisema kuwa Zombe alikuwa na jukumu la kujua wahalifu walikohifadhiwa baada ya kukamatwa badala yake alifuata fedha. Jaji akanukuliwa akisema, Hapa ni wazi kuwa ni kweli Zombe alijua kilichokuwa kinaendelea! Akawaachia huru.
__________________________

Kunahitajika maoni bila ya jazba kuhusiana na kesi hii ambayo haina shaka yeyote ile kuwa wahusika au washitakiwa wamo ambao wamekiri mauaji haya na hata hivyo wameachiwa huru ,kuna imani kwamba ukinunua kitu cha wizi na wewe utakuwa mwizi namna ya wahusika walivyohusishwa katika kesi hii moja kwa moja na wao watakuwemo katika mkumbo wa mauaji.Kama kuna mtu anaweza kuwaweka sawa watu hawa na kutuonyesha kuwa hawastahili adhabu yeyote ile itakuwa vizuri atuwekee hapa na atufafanulie ili kueneza mwanga kwa WaTanzania walioachwa midomo wazi wakiishangaa Serikali na mahakama zake. Au ni sabotaji ya kuikwamisha serikali ya CCM na kuipa wakati mgumu.
 
Tuna matatizo makubwa kwa prosecutors na detectives. Jamaa hawafanyi home work yao.

Ingekuwa ni ajabu sana endapo jaji angewahukumu kuua. Jamaa hawakuua kwa mujibu wa maelezo ya prosecutors na wastakiwa lakini inaonekana walihusika kwa kiasi kikubwa. Sasa endapo wangekuwa walishtakiwa kwa kushiriki kuua hiyo ingekuwa kesi ya kushinda.

Maelezo ya mawakili wa Serikali (Jamhuri) hayakusema kwamba jamaa wameua, wala hayaku-point mtu aliyeua. Hata yule aliyekiri, hakukiri kuua wala kuona mauaji yakifanyika. Jamaa alisema alisikia mlio wa bunduki na akaona maiti zimelala chini. Haya siyo maelezo ya kumhukumu kuua. Yule aliyetoa maelezo ya kuona tukio likifanyika (Marehemu Lema) naye asingehukumiwa kuua kwani hakuua. So, sheria imefuata mkondo wake.
 
Bwana mwiba Masati JK, as he then was, amejaribu kueleza kwa kirefu jinsi killa mmoja wa washtakiwa alivyotuhumiwa kwa mauaji hayo lakini mwishoni alisema kuwa waendesha mashtaka walishindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa walihuska directly kwenye mauaji hayo na kuwaachia huru kwa kuagiza polisi wawatafute wauaji.

Vilevile aliagiza washtakiwa wote waachiwe huru iwapo kutakuwa hakuna uhalali wa kisheria wa kuwakamata tena. Hata hivyo walishindwa kukamatwa tena pengine kwa sababu hata vyombo vya dola havikutegemea hivyo.

Najaribu ku-attach hukumu hiyo imekwama nitajaribu tena kesho. Labda ni kubwa mno hivyo ikishindikana nitaituma kwa vipande au nitawasiliana na watu wa IT.
 
Bwana mwiba Masati JK, as he then was, amejaribu kueleza kwa kirefu jinsi killa mmoja wa washtakiwa alivyotuhumiwa kwa mauaji hayo lakini mwishoni alisema kuwa...
Sawa mkuu hiyo hukumu itatusaidia sana. Thanks in advance.
 
Sasa hata kitendo cha wao kushiriki hakina nafasi ya kupata hukumu ? Tunasikia baadhi ya hukumu kuwa mshitakiwa hakutenda kosa fulani lakini alishiriki hivyo atahukumia kifungo kadhaa na kutumikia jela miaka kadhaa.

Waliouliwa walikamatwa hai wakafungwa pingu na watu wameona kama haitoshi wakapelekwa msituni na ushahidi umetolewa wakarudishwa kutoka huko msituni wakiwa maiti ,sasa hawa waliowapeleka na kuwarudisha si ndio hawa hawa walioachiwa huru?

Sasa kama walipelekwa huko na kuuliwa na mtu mwengine ,inamaana hawa waliowachukua ndio waliowapeleka kwenda kuuliwa ,hata akiwa mtekelezaji wa kitendo cha kuwaua ni mwengine ,hawa wanaingia katika system yote ya utayarishaji wa mauaji. Tusubiri hiyo hukumu ambayo imesemwa itawekwa hapa tuichambue.
 
Kwa kifupi Jaji Masati amewaambia Polisi na Prosecutors waache usanii, waanze kufanya kazi sasa, kama hawataki lawama kutoka kwa wananchi.

Kuwa lawama zitawaandama na wanao wajibu wa kuwalinda waliokuwa wameshtakiwa ili wasidhurike. Na zaidi ya hapo ni kama pia ameiambia serikali yetu kuwa hawa ndiyo Prosecutors ambao mnao, sasa chagueni kuwanoa zaidi wajue kazi au muwarudishe kina Zombe kazini na kuwalipa fidia.

Chaguo ni lenu. Na zaidi sana ameikumbusha pia serikali, na haswa DPP kuwa hata hizo kesi chache za mafisadi zitaishia hivyo hivyo kama hamtakuwa makini.

Ninahakika Jaji Masati angesoma comments hizi angekiri kuwa nimemwelewa vizuri.
 
Sasa hata kitendo cha wao kushiriki hakina nafasi ya kupata hukumu ? Tunasikia baadhi ya hukumu kuwa mshitakiwa hakutenda kosa fulani lakini alishiriki hivyo atahukumia kifungo kadhaa...

Mwiba, mahakama haiwezi kumfunga au kutoa hukumu yeyote mshitakiwa kwa kosa ambalo hakushtakiwa. Ndo maana waendesha mashtaka makini wanapompeleka mtu mahakamani wanaorodhesha makosa mengi inavyowezekana. Sasa hawa walishtakiwa kwa kosa moja tu yaani la mauaji. Hapo ndipo DPP alipocheza mchezo wake mchafu.

Unajua hata mauaji ya halaiki ya Rwanda, mtuhumiwa anafunguliwa makosa mengi. Wangekuwa wanafunguliwa kosa moja wengi wangetoka. Ndo maana huwa tunasikia hukumu kwamba hakupatikana na kosa la genocide ila la kushiriki mauaji kwa kuwafichua watusi waliokuwa wamejificha kanisani nk. Nadhani utakuwa umenipata Bw./Bi. Mwiba.
 
Jeshi la la Polisi nchini limesema haliwezi kuzungumzia hatima ya kibarua cha Zombe kwa sasa, kutokana na serikali kutoa notisi ya kukata rufaa juu ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Agosti 17 mwaka huu.

Akikaririwa na chanzo chetu cha habari..msemaji wa jeshi hilo Kamanda Abdalah Msika, alisema...“Mwanasheria Mkuu wa serikali ameshapeleka notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, kwa hiyo hatuwezi kuzungumza chochote kwa sababu kesi hiyo haijaisha na wala matokeo ya kesi iliyosomwa katika Mahakama Kuu hayajaja kwetu,”.

Akiendelea alisema........“Katika kesi hii watu waliokuwa ni waajiriwa katika jeshi hili ndio walishtakiwa, lakini jambo likiwa katika shughuli za kimahakama sisi hatuwezi kulizungumzia, ni kama tu kesi hii ilivyokuwa Mahakama Kuu hatukuweza kuzungumza chochote,” alisisitiza Msika.

Zombe na wenzake hivi karibuni walishinda kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge, mkoni Morogoro na dereva teksi mmoja mkazi wa Manzese, jijini Dar es Salaam iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama Kuu chini ya Jaji Salum Massati.
http://www.darhotwire.com/home/news/2009/08/28/polisi_yachemka_kuzungumzia_kibarua_cha_zombe.html
 
Mwenyekitiwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Manento, amesema Mahakama Kuu ya Tanzania imetekeleza wajibu wake katika kutoa hukumu ya aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na wenzake wanane, na kwamba anayesema kinyume cha hukumu hiyo anakiuka Katiba ya nchi.

Aidha, alisema kwa mujibu wa Katiba, haki za binadamu zimezingatiwa, maana mahakama ndicho chombo cha juu cha kutekeleza haki hiyo na hukumu hiyo haiwezi kutenguliwa kwa namna yoyote sasa, mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo na Mahakama ya Rufaa, hatua hiyo ikichukuliwa.

“Mahakama imeshatoa uamuzi, hakuna anayeweza kuongeza hapo wala kupunguza, hakuna mwingine anayeweza kusema tofauti ya hukumu hiyo na ikatekelezeka na kama atatokea, atakuwa anakiuka Katiba,” alisema Jaji Manento ambaye alikuwa akifafanua Kifungu cha 107 (A) (1) cha Katiba.

Jaji Manento alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii, waliomtaka afafanue mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu Haki za Binadamu na Biashara, kwa viongozi wa kampuni na asasi mbalimbali nchini.

Akifafanua kifungu hicho, pamoja na mambo mengine, alisema kinaeleza kuwa mahakama ndiyo mamlaka ya juu inayohakikisha haki za binadamu zinapatikana na inatekeleza hilo kwa misingi ya Katiba ambayo ni sheria mama.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, mahakama ikishatoa uamuzi, hakuna wa kuongeza wala kupunguza na akitokea mtu mwingine kutoa hukumu kinyume na iliyotolewa mahakamani si sahihi, kwa kuwa mahakama imetekeleza wajibu wake na haijafanya kitu nje ya sheria zilizopo.

Kuhusu malalamiko ya wananchi hasa ndugu wa wafanyabiashara waliouawa Januari 14, 2006, Jaji Manento alisema amesoma kwenye magazeti kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ameonesha nia ya kukata rufaa, ambayo alisema ndiyo njia sahihi ya kuendeleza haki za binadamu na si vinginevyo.

Alisema katika Mahakama ya Rufaa, kesi itasikilizwa na majaji watatu na si mmoja kama ilivyokuwa katika Mahakama Kuu na kuongeza, kuwa kinachofanyika si kumpinga Jaji aliyetoa hukumu, bali ni kupitia kesi kwa mara nyingine.

Hata hivyo, alisema wananchi wanaolalamika, wana haki ya kufanya hivyo, kwa kuwa wanatekeleza moja ya haki za msingi za mwanadamu za kujieleza na kusikilizwa, ili mradi havunji sheria za nchi, lakini akawataka wananchi waheshimu uamuzi wa mahakama.

Aidha alisema kwa misingi ya maadili ya ujaji, haruhusiwi kudadavua hukumu iliyotolewa na Jaji mwenzake, hata kama ingekuwa na upungufu na kuwaonya baadhi ya watu wenye nafasi kama hiyo, kuwa macho wasije kukiuka maadili ya kazi.

Zombe na wenzake waliachiwa huru na Mahakama Kuu, Dar es Salaam Jumatatu wiki hii baada ya Jaji Salum Massati kueleza kuwa watuhumiwa hao wameonekana hawana hatia huku akiwataka waendesha mashtaka kuwatafuta watuhumiwa wawili (Saad na James) ambao walitajwa kuhusika moja kwa moja kuwapiga risasi wafanyabiashara hao.

Wafanyabiashara waliouawa katika msitu wa Pande, Mbezi Luis, Kinondoni, Dar es Salaam Januari 14,2006 ni Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Mathias Lung’ombe na dereva teksi wa Manzese, Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Kutoka Ulanga, John Nditi anaripoti kuwa wanakijiji cha Ipango, wanakusudia kufanya maandamano ya amani hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kutoa kilio chao juu ya kuachiwa huru kwa washtakiwa hao. Kutokana na uzito wa jambo hilo, Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Ulanga ilitarajia kukutana jana katika kikao cha kawaida na kuingiza ajenda ya hali ya kisiasa kuhusu hukumu hiyo kwa kuwaita viongozi wa matawi wa Ipango na wa kata ya Mahenge ili kujadiliana.

Pamoja na msimamo wa wanakijiji hao wa kufanya maandamano, ndugu wawili wa kiume wa familia ya Chigumbi, Selestin na Franco, kwa nyakati tofauti walisema familia yao haijaridhika na hukumu.

Hata hivyo walisema familia iko tayari kuungana na Serikali kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo licha ya familia kukosa uwezo wa kifedha na kuwaomba wananchi kuwaunga mkono.

Naye Mzee Lunkombe, ambaye ni mzazi wa marehemu Mathias alisema ni mapema kuzungumzia hatua familia inayotaka kuchukua baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo. Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Ipango, Festo Uyalo, alisema moyo wa kujitolea kwa wananchi wa kijiji hicho baada ya hukumu hiyo umekufa.

Pamoja na kukusudia kufanya maandamano hayo, wanachama wa CCM wamesusa fomu za uongozi wa serikali za vitongoji na vijiji unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2010 kwa madai kuwa serikali imewanyima haki.

Katibu wa tawi la CCM Ipango, Pacienci Lyahera, alithibitisha baadhi ya wanaCCM wa kijiji hicho kurudisha fomu walizochukua kuomba uongozi kupitia chama hicho ingawa hakutaja idadi yao, lakini hali haiko hivyo katika sehemu zote kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ulanga, Leticia Mtimba.

Hata hivyo alikiri kwamba eneo la kijiji cha Ipango, ambako ndiko kwao marehemu, upo ushawishi wa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kwa wananchi kuugomea uchaguzi huo wa Serikali za mitaa hasa kwa upande wa CCM.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3293&cat=kitaifa
 
Mtu anayesaidia kutenda kosa (kwa kesi hii, kuua) (accessory before the fact) hawezi kupatikana na hatia mpaka mtenda kosa (principal offender) naye awe amepatikana na hatia!

Kwa hiyo kama Saad na James wangepatikana na kutiwa hatiani basi kulikuwa na uwezekano wa kuwatia akina Zombe hatiani kwa kusaidia kutenda kosa!

Hata hivyo kungekuwa na utata kuwatia hatiani kwa kosa la kusaidia kutenda kosa kwa kuwa hawakushtakiwa nalo na pia sio cognate offence!
 
Mimi huwa napata Shida sana ninaposikia Vyombo vya Habari na hata watu na wengine ni wataalam waliobobea kwenye Sheria wanasema eti Jaji wa Mahakama ya Rufaa amekosea kuamua kesi ya kina Zombe kisa eti Zombe na Wenzake HAWAKUHUKUMIWA kifungo au kunyongwa.

Natumia neno HAWAKUHUKUMIWA kifungo au kunyongwa au faini ili muweze kunielewa. LAKINI watu hawa wamepata hukumu WAMEHUKUMIWA kutokuwa na hatia ya KOSA waliloshitakiwa.

Nasema KOSA waliloshitakiwa kwa sababu ukifuatilia tangu mwanzo wakiwa Watuhumiwa kwa maana ya kwamba walipokuwa hawajathibitishwa na Mahakama kama wanakesi ya kujibu huitwa Watuhumiwa na hata baada ya kushitakiwa kwa maana ya kuthibitishwa kwamba wanamashtaka ya kujibu, Mlolongo wote kulikuwa na SHITAKA MOJA TU lilifunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. SHITAKA hilo ni KOSA LA KUUA.

Sasa upande wa Mashtaka ulitakiwa uthibitishe pasipo shaka kwamba ZOMBE na wenzake waliua. Hili ndilo kosa la Kisheria lililofanyika. Mhe. JWMK alisema hakuna ushahidi wa kuthibitisha kwamba ZOMBE na wenzake waliohukumiwa kuwa huru waliua.

Mimi nilitegemea MKURUGENZI WA MASHTAKA angefungua mashtaka zaidi ya moja mfano kosa la kuua, pili kosa la kutoa habari za uongo kwamba wale ni wezi - kwenye Utumishi ni kosa kusema uongo, Tatu kutumia Ofisi yake kuwahukumu watu bila ya kuthibitisha kosa n.k
 
Back
Top Bottom