Where is Vithlani? Still in UK or already in Tanzania? Sirikali iko kimyaaaaa haitaki kutufahamisha nini kinaendelea kuhusu fisadi huyu.
.
Wajameni hawa PCCB hawana lolote. Vithlani japo anatafutwa lakini hana kesi yoyote ya maana.
Hata hii kesi ya kina Mramba, Mgonja na Yona, serikali itapigwa chini.
Ile habari ya this day na kulikoni kuhusu kukamatwa kwa Vithlani ni uzushi tuu kama uzushi wa kukamatwa kwa Mzee wa zeutamu.
Kisheria Vithlani amefanya biashara safi. Kapendekeza bei, serikali ikakubali. John Cheyo akazama kwenye mtandao, akapata bei halisi, akaitisha press conference kupinga, serikali ikaziba masikio, sasa yameibuliwa na SFO ndipo serikali kupitia PCCB inajidai eti inajali!.
Aminini msiamini, mgao haukuishia kwa mzee wa vijisenti, ulipanda mpaka juu darini. Kwa akili ya kawaida, haiwezekani mtuu huyo huyo alambe deal zote hizo yeye mwenyewe na washirika wake, Rada/Ndege ya rais, Helcopter za jeshI, magari ya jeshi na deal nene la silaha za kivita (ila hii ni siri).
Kesi anayotafutiwa Vithlani sio kesi, kusema uwongo chini ya kiapo ni kifungo cha kuanzia mwezi mmoja na kisizidi mwaka mmoja.