BAADA ya kutulia kwa muda, sakata la ununuzi wa rada, limeibuka tena na safari hii kwa sura tofauti, baada ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuazimia kulijadili bungeni katika moja ya vikao vyake vinavyoendelea.Hoja hiyo jana ilifikishwa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alisoma kauli ya serikali dhidi ya hatua ya Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kutoa fedha za tozo ya rada kwa asasi za kiraia.
"Tanzania ni nchi maskini, lakini haiko tayari kudharauliwa kiasi hicho kwa serikali yake, tasisi zake na asasi zake kutoaminiwa. kuruhusu hilo lifanyike ni kuruhusu kuibiwa kwa mara ya pili,"alisema Membe.Membe alisema kitendo cha BAE kutaka kuzipeleka fedha hizo kwenye asasi za kiraia nchini Uingereza ili zije kufanyia shughuli hapa nchini ni kinyume na makubaliano yaliyofikia kati ya Serikali ya Tanzania, SFO na serikali ya Uingereza.
Baada ya taarifa hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisimama na kuomba mwongozo wa spika na kusema," Mheshimiwa Spika, tunaomba taarifa hiyo ya serikali ijadiliwe bungeni."Baada ya kusema hivyo takriban wabunge wote walisisimama kuuuga mkono kitendo kilichomfanya Spika Anne Makinda kusema atatafuta fursa kwa ajili ya kujadili suala hilo bungeni.
Source: Mwananchi
My take:
This radar change has absolutely nothing to do with recovering the money on behalf of ordinary Tanzanians, but has everything to do with 2015. Membe alikuwa wapi siku zote asiseme uchunguzi ufanyike ili washiri kwa upande wa Tanzania wachukuliwe hatua. Mbona ang'ang'ania hela bila uwajibikaji wa wale wote waliofanikisha dili? Na hao wabunge waliounga mkono hoja kwa kishindo wamejuwa lini Tanzania imelanguliwa kwenye ununuzi wa Radar? Na wamefanya nini tangu walipogunduwa ulanguzi huo?
Kwa upande mwingine nahisi fitna za kuwatoa kafara mapacha watatu zimekuwa ngumu hivyo wazee wa ‘kuzunguka mbuyu' wamepata kona nyingine. Wataanza na rada kujadiliwa bungeni na baadae tunaweza kuona mizimu mingine ikifufuliwa lengo likiwa kupata mtaji wa kumtoa mtu kwenye matumaini ya 2015!