Akishatiwa mbaroni, mashtaka mengine yako mbeleni.. tunataka abambwe kwanza... ni lazima tuhakikishe kuwa hawezi kuunda Kikosi cha Kisasi, au kula Njama kuharibu uchunguzi. Kwa jinsi mambo yalivyo inaonekana huyu ndiye Malaika wa Shetani ambaye kwa hakika tuhuma anazokabiliwa nazo ni sawa na Salamu toka Kuzimu.
Yeyote ambaye anamfahamu au anafahamu alipo ahakikishe kuwa anampatia ujumbe toka serikali ya Tanzania ujumbe ambao ni sawa na Simu ya Kifo. Sina uhakika kama ana ulinzi wowote kiasi cha kuweza kuonekana ni Maskini Jeuri kwani jinsi anavyofahamika hapendi kuonekana mchana, mara nyingi utamkuta Dar-es-Salaam Usiku.
Kwa yeyote anayemtafuta lazima ahakikishe yeye mwenyewe anayo Hawala ya Fedha kwani endapo atahitaji tiketi aweze kurudi naye salama ama sivyo itakuwa ni Roho Mkononi. Huyu bwana kutokana na shughuli zake amekuwa kama kile kisa cha Ngoswe - Penzi kitovu cha Uzembe na watu kumuamini walifanya makosa.
Jitihada za kumtafuta zitakuwa ni kama Usiku wa Balaa ambapo hakuna kinachotabirika kwani hadi mwisho ni lazima wale wanaomtafuta wajiulize "Tutarudi na Roho Zetu?". Makosa kidogo tu yatakuwa yanawafanya wamtafutao wapotee kama yule bwana aliyepotea katika Mzimu wa Watu wa Kale. Ni lazima tuunganishe nguvu zetu na kudhamiria kama Kuli vinginevyo itakuwa ni kama mtu Aliyeonja Pepo au kama mambo ya nchi ya Kusadikika.
Nina uhakika huyu bwana atajaribu kutoa kitu kidogo ili asikamatwe lazima watu wamuambie "Pesa Zako Zinanuka". Hata hivyo isidhaniwe kuwa kwa kuwekwa mbaroni huyu bwana atakuwa amefikia Kikomo, kwani inasadikiwa anayo Roho ya Paka. Hata hivyo tusikubali geresha hizo na tufanye jitihada zetu za kumtia mbaroni ziwe ni za Kufa na Kupona.
Kwa hakika ndugu zangu kukamatwa kwa Vithlani na hatimaye kufikishwa Mahakamani na hatimaye kukutwa na hatia itakuwa ni jitihada zinazostahili Zawadi ya Ushindi! Wanausalama wetu watumie njia zote kumtia mbaroni kwa amani, lakini Akibisha, Mlipue!
Mwanakijiji asante sana kwa kunikumbusha hizo riwaya, umenifurahisha sana. Na jinsi ulivyopangilia huo mlolongo, hongera, imependeza.