Kesi ya Mbowe na wenzake inaitesa Serikali, inawatesa viongozi wa vyama na Serikali na inatutesa raia wema kuliko inavyomtesa Mbowe na wenzake

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,490
13,022
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa

Sote tunafahamu yanayoendelea hapa nchini kwetu,ukiachana na suala la Ngorongoro Conservation suala la moto kwa Taifa hili ni kesi ya Freeman Aikaeli Mbowe

Kesi hii inamtesa kiongozi mkuu wa nchi, inawatesa viongozi wa vyama na serikali na inavitesa vyombo vya ulinzi na usalama kuliko inavyomtesa Mbowe na wenzake

Kesi hii,inawatesa wengi kwa kuwa mazingira ya kuitunga na watu walioitunga hawakutumia akili.Mkubwa wa nchi anataka kuifuta lkn,anahisi itamdhalilisha kwa kuwa alishasema "wengine walishafungwa" lkn, ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa tayar ameshafungwa kutokana na kesi hii.

MATOKEO YA KESI YA MBOWE KWA SERIKALI NA MIHIMILI YAKE
Kwa upande wa serikali, kesi hii inaondoa hali ya serikali kuaminiwa na raia wake wa ndani na nje ya nchi na hata wageni (wasio raia) waliondani na nje ya nchi hawawezi kuiamini serikali tena kutokana na utungwaji wa kesi hii. Serikali imewatumia watu kutoka ndani ya idara ya usalama wa Taifa ambao ni Kidando, Jaji Tiganga na wengineo (mawakili wote wa serikali kwenye kesi hii ni watu kutoka idara ya usalama wa Taifa kutoka kwenye desk ya mahakama) kwa hiyo kwa watu wenye akili timamu hawawezi kuiamini serikali kwakuwa inatumia watu kutoka kwenye organs za serikali kutesa raia wake.

Muhimili wa mahakama umepoteza imani yake kwa wananchi kutokana na mwenendo wa kesi yenyewe lkn,muhimili huu utapoteza imani kwa wananchi zaidi endapo utamfunga Mbowe na wenzake.

HATUA INAYOFUATIA
Hatua pekee iliyobaki kwa ccm na serikali yake ni kumfunga Mbowe kwa kulazimisha na baada ya muda fulani Mkuu wa nchi atatoa msamaha ili ionekane kuwa Mbowe alikuwa na hatia ndyo maana serikali ilimfunga pia,serikali itatumia kigezo kuwa imemsamehe Mbowe kwa kuwa alipanga kufanikisha ugaidi lkn,hakuwa amefanya ugaidi pia,alipokuwa gerezani alionyesha nidhamu njema

USHAURI KWA MBOWE NA CHADEMA
Kamwe, msikubali kumuomba Lucifer (CCM na Serikali yake) msamaha kwa kuwa huo msamaha utaambana na masharti magumu (attached with difficult conditionalities) miongoni mwa masharti hayo itakuwa ni pamoja na kuandika barua ya kukiri kuwa mlishiriki kwenye njama za kupanga ugaidi na baada ya hapo Chama kinaweza kufutiwa usajili kwa kuwa kitaonekana kama ni chama cha kigaidi ndyo maana Zitto anang'ang'ania sana suala la Mbowe kuachiwa kwa njia ya msamaha maana anajua kitakachofuatia ni Chadema kufutiwa usajili kama chama cha upinzani then,chama chake ndyo kitakuwa chama kikuu cha upinzani

Mbowe akiomba msamaha ataonekana kama kweli ni gaidi so,atazuiwa kufanya siasa kwa maisha yake yote yaliyobaki chini ya jua,ataishi chini ya uangalizi maalum wa jeshi la polisi na mbaya zaidi kuna baadhi ya nchi anaweza kuzuiwa kuingia.

USHAURI KWA SERIKALI
Rais futa kesi hiyo kwa kutumia akili,muagize hata Jaji wako Tiganga aifute kwa kuwa nafasi bado inaruhusu kwa wewe kufanya hivyo

MWISHO
Kesi hii inatengeneza doa kwa serikali,inawapa wananchi hasira na hali ya kuichukia nchi yao pamoja na kutokuwa na imani na nchi yao
Kesi hii, inawafanya wawekezaji kutokuleta mitaji yao Tanzania kwa kuwa ni kesi iliyobeba sura ya nchi kwenye angle ya usalama na haki (hakuna muwekezaji makini anayeweza kupeleka mtaji wake kwenye Taifa ambalo haliwezi kutenda haki) Kesi hii, inalichafua Taifa kwenye mipaka ya kimataifa,inawachafua viongozi wa vyama na serikali

Katika ulimwengu wa kiroho, kesi hii inaliletea Taifa laana na kuondoa baraka za Mungu Muumba wa vyote kwenye uso wa ardhi. Kumbukeni kipnd Pharaoh alipowazuia wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi Mungu alileta mapigo kwa raia wote wa Misri so yatakuja mapigo mengi kwa Taifa na watawala. Pia, Mungu hatapokea maombi yenu ninyi watawala na wala sadaka zenu kwa kuwa vitabu vinasema "kama umekosana na jirani yako urudi ukapatane nae ndipo utoe sadaka yako"

"Maombi ya mwenyedhambi ni machukizo mbele za Mungu"

Mbowe siyo gaidi, tunahitaji katiba mpya

Asanteni!
 
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa

Sote tunafahamu yanayoendelea hapa nchini kwetu,ukiachana na suala la Ngorongoro conservation suala la moto kwa Taifa hili ni kesi ya Freeman Aikaeli Mbowe
ndiposa unajiuliza watu wanakwenda misikitini kufanya nn! wanakwenda makanisani kufanya nn! unawatesaje binadamu wenzio wasio na kosa kiasi hicho! na ktk kuwatesa wanateseka familia na wadau wote - watu wengi.

Trump aliposema baadhi ya nchi zetu ni shit-hole countries alikua amekosea! kuna hata msomi flani hapa hapa kwetu aliedhalilisha taaluma yao kwa kusema aliokotwa jalalani na lugha hiyo kuonyesha kilichopo ktk baadhi ya vichwa vyao!

nchi hii kulishawahi kuwa na mahakimu mahiri wenye kuheshimu taaluma zao ambao kuwepo kwao kuliifanya taaluma kuonekana inakidhi mategemeo, ambao hawakuidhalilisha kwa kuilinganisha na jalala, naamini hao bado wapo. lkn inaelekea kuwepo kwao na kupewa nyadhifa hizo ni vitu 2 tofauti. mfumo unawapenda wanaojinasib kuwa wame pendelewa kwa kuokotwa toka huko kuchafu, wanaona ni fadhila. sijui kwa mfumo tulio nao kama tutajapata watakaoona kujidhalilisha hakuna heshima... au ni suala la tumbo!

ni kesi ya aina yake. mashahidi 90% wa ukoo 1 wa mapolisi, wanaamini wasemalo ndilo, kesi ya kuangusha miti kuanzia moro-mbeya, mz, ars... nk. bila shoka, msumeno wala chain saw na kuisambaza barabarani kwa watu 3 wakisimamiwa na Mbowe huku waTz tukiwa tunaangalia ...duh! ugaidi wa watu 4 kujaza miti barabarani nchi nzima huku dunia ikiangalia!! hawachoki?! watatoa wapi hizo nguvu?! kesi hizi mnazitoa wp? ingalawa fanyeni basi maandalizi msisumbue watu.

imefikia mahali heshima kwa kiongozi ni muhimu. awaachie achekwe, awafunge achekwe! jamaa wakishinda kesi, fidia ni balaa. dawa ni wahukumiwe alafu baada ya muda waachiliwe kwa huruma.
nawaonea huruma majaji waloko ktk mhimili huo, kesi za kisiasa zitawatesa.
au na wenyewe suala la katiba mpya linawatesa!? labda!
 
kesi yoote shahi mmoja tu. polisi
 
Kinachowezekana tu watamfunga hapo miezi sita angalau kufuta aibu.
Wanaweza kumfunga maisha. Usicheze na kitu kinaitwa utamu wa madaraka. Wamfunge miezi sita kwa kumuogopa nani au nini?

Tatizo hapa ni uduni wa fikra na kutokujiamini kwa wafuasi na wapenzi wa Mbowe na wapigania demokrasia wote nchini. Kweli imeshindikana kuliamsha dude ili serikali iombe poo??
 
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa

Sote tunafahamu yanayoendelea hapa nchini kwetu,ukiachana na suala la Ngorongoro conservation suala la moto kwa Taifa hili ni kesi ya Freeman Aikaeli Mbowe
monde arabe japo sifahamu Elimu yako lakini ninakuona wewe ni mweupe sana kwenye mambo ya Serikali na siasa.

Hivi unaijuwa Serikali au unadhani ni kikundi fulani cha watu? Serikali ni taasisi yenye vyombo vinavyowezesha Nchi itawalike. Hata wewe mwenyewe sasa hivi ukipewa nafasi ya kuwa IGP au DG TISS, utahakikisha kuwa Mbowe anafungwa.

Serikali siyo hoteli au benki au kikundi cha kufa na kuzikana bali Karl Marx anaitafsiri ifuatavyo "Government is a coercive instrument to the people".

Ili Serikali ipate uhalali wa kuitwa Serikali lazima i- "coerce". Kwa kiswahili ku -coecre ni kutumia nguvu. Serikali ambayo hai coerce ni Serikali legelege na rahisi kupinduliwa au Kuondoka madarakani.

Tuje suala la Mbowe, si kweli kwamba ni issue mtaani. Kwanza mtaani kumetulia hatuna bugudha za maandamano, watu wako kwenye mishe za kutafuta fedha, chakula, watoto wao waende shule. Mbowe anajadikiwa na wale wanaokwenda Mahakamani na kwenye mitandao ya space tu
 
ndiposa unajiuliza watu wanakwenda misikitini kufanya nn! wanakwenda makanisani kufanya nn! unawatesaje binadamu wenzio wasio na kosa kiasi hicho! na ktk kuwatesa wanateseka familia na wadau wote - watu wengi.
Usichezee kitu kinaitwa madaraka. Mungu yupo lkn anatenda kwa neema na rehema zake kwa kila awaye yote. Hekima ya Mungu haichunguziki na haitumii kanuni za wanadamu..

Ndiyo maana Kuna watu ni waovu sana Kwa jicho la wanadamu lkn wamefanikiwa sana maisha I mwao
 
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa

Sote tunafahamu yanayoendelea hapa nchini kwetu,ukiachana na suala la Ngorongoro conservation suala la moto kwa Taifa hili ni kesi ya Freeman Aikaeli Mbowe

Kesi hii inamtesa kiongozi mkuu wa nchi,inawatesa viongozi wa vyama na serikali na inavitesa vyombo vya ulinzi na usalama kuliko inavyomtesa
Hii nchi ni kubwa sana Mjumbe, kesi ya Mbowe ni kitu kidogo sana kwa Mtanzania wa kawaida, mnaifuatilia nyie wachache mlio maslahi nayo kiitikadi. Watu wa nje ndiyo hawo EU na UN ambao wamempa Mama trilioni 2 bwerere bila masharti ili iwasaidie WAO balaa la climate change, yaani wanamuomba awape mapori yawe carbon sink waokoe viwanda vyao. Hao hao wanamtaka awasaidie Kamanda IGP na Kamanda JWTZ kuzuia ugaidi.

For your information mbowe huyuhuyu kama ni angekuwa kwao kwa vitendo hivihivi ushahidi huuhuu wa Afande Urio na miamala tigopesa wangeshamsweka Guantanamo. Hawaoni cha mno kwenye kesi hii ndiyo maana wanaenda na barakia: cha ajabu kwao ni kwa nini magaidi 4 bado wapo huru.
 
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa

Sote tunafahamu yanayoendelea hapa nchini kwetu,ukiachana na suala la Ngorongoro conservation suala la moto kwa Taifa hili ni kesi ya Freeman Aikaeli Mbowe
USHAURI KWA MBOWE NA CHADEMA

Kamwe, msikubali kumuomba Lucifer (CCM na Serikali yake) msamaha kwa kuwa huo msamaha utaambana na masharti magumu (attached with difficult conditionalities) miongoni mwa masharti hayo itakuwa ni pamoja na kuandika barua ya kukiri kuwa mlishiriki kwenye njama za kupanga ugaidi na baada ya hapo Chama kinaweza kufutiwa usajili kwa kuwa kitaonekana kama ni chama cha kigaidi ndyo maana Zitto anang'ang'ania sana suala la Mbowe kuachiwa kwa njia ya msamaha maana anajua kitakachofuatia ni Chadema kufutiwa usajili kama chama cha upinzani then, chama chake ndyo kitakuwa chama kikuu cha upinzani

NOMA SANA!
 
Back
Top Bottom