Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Bidhaa za nyama, gesi ya kupikia, mkaa na viazi mviringo zimetajwa kuongeza mfumuko wa bei kutoka asilimia 3.8 Agosti hadi asilimia 4.0 kwa Septemba mwaka huu.
Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Oktoba 8 jijini Dodoma, imetaja bidhaa nyingine zilizoongeza mfumuko wa bei ni ngano na maziwa ya unga.
Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema sababu za kuongeza mfumuko ni kutokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma.
Minja alisema mabadiliko hayo ni kwa mwaka ulioishia Septemba ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Agosti 2021.
Amesema badiliko hilo la asilimia 0.2 limechangiwa na kasi ya mabadiliko ya bidhaa za vyakula kama unga wa ngano kwa asilimia 6.8, nyama ya ng’ombe kwa asilimia 3.4, maziwa ya unga kwa asilimia 9.2, mayai kwa asilimia 5.0 na viazi mviringo kwa asilimia 4.7 na kufanya kuongezeka kwa asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.6 mwezi Agosti.
Amesema pia bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko ni gesi ya kupikia kwa asilimia 2.7, mkaa kwa asilimia 3.5, na huduma ya malazi katika nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7na kufanya bidhaa hizo kuongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.0 mwezi Agosti.
Mwananchi