Kero ya Vidhibiti mwendo kwenye Mabasi ya Mikoani

wanasema bora uwende polepole lakini ufike salama


Lakini hii siyo njia pekee ya kumaliza tatizo, wangeshirikisha vichwa na wadau wote nchini kutafuta dawa ya ajali za mabasi, je ughaibuni wanakoendesha kwa 100++ KMPH na hatusikii ajali wanafanyaje, zingeenda team huko zikajifunze
 
Nadhani gari limetengenezwa kwa spidi zake kama trekta, basi na mengineyo, na ajali sio mpaka isababishwe na mwendo kasi, kuna uzembe, njia mbaya, kutofanya matengenezo ya kutosha na vingine Vingi, nadhani ni muda muafaka wa kuangalia suala hili kwa mapana yake, ifike hata spidi 100
80% ya ajali husababishwa na mwndokasi,
Juzi nimetoka mbeya saa 12 asubuhi, nimefika dar saa 4 usiku, poa tu muhimu kufika, kama una haraka safiri nda ndege.
 
Ingekuwa vyema kwanza kama wangeanza na usalama wa miundo mbinu yenyewe halafu wakakagua vifaa vyenyewe vya usafiri. Kuna mabasi ni mabovu hakuna mfano ila yapo barabarani yanafanya kazi
 
Lakini hii siyo njia pekee ya kumaliza tatizo, wangeshirikisha vichwa na wadau wote nchini kutafuta dawa ya ajali za mabasi, je ughaibuni wanakoendesha kwa 100++ KMPH na hatusikii ajali wanafanyaje, zingeenda team huko zikajifunze
Wana barabara bora wale...kila lane ina speed yake
 
Sidhani kama ni mabasi yote yamefungwa hivyo ving'amuzi, kama yote yamefungwa basi kuna mengine yatakuwa ya watu wanene wasioguswa, ninasafiri mara nyingi na bus moja ya BM Moro - Moshi route, ikimaliza mpaka wa Tanga na Kilimanjaro speed yao ni beyond 100 KMPH
Mara ya Mwisho umesafiri Lini mkuu?
 
Ingekuwa vyema kwanza kama wangeanza na usalama wa miundo mbinu yenyewe halafu wakakagua vifaa vyenyewe vya usafiri. Kuna mabasi ni mabovu hakuna mfano ila yapo barabarani yanafanya kazi
miundo mbinu ndio mchawi mkubwa. na sio speed. Waweke double lane waone kama hayo yatatokea
 
Speed ndogo ya mabasi imekua kero kweli tena bora basi zingekua sleep liners lakini so zenye siti za kukalia watoto. Zambia basi kutembea mwisho ni saa tatu usiku ila zina amsha 12 asubuhi,hakuna tochi nchi nzima zaidi ya check points na ajari sio nyingi kama Tanzania.
 
miundo mbinu ndio mchawi mkubwa. na sio speed. Waweke double lane waone kama hayo yatatokea
Itakua hujapanda basi za mkoani..kuna siku sumry anataka kuovateki kwenye kona..scania ilikua inakuja vibaya huko mbele
 
Aisee spidi 80 ni kero mnoooo kwa abiria. Ni spidi ndogo na inachosha mnoooo. Mi naona dawa ni moja tufanye magari yote ya private, Serikali na mabasi yaende spidi 80 ndio watajua kero yake. Wao wanatembea spidi 160 ndio maana hawaoni kero yoyote ya spidi 80.

Binafsi reasonable spidi iwe 110 sio 80 iliyopo sasa. Hiyo spidi 80 ni ya enzi hizo barabara ni mbovumbovu.
 
Chinga One nawasalimu wana JF,

Baada ya Salam hizi napenda kutoa pongezi kwa Sumatra na Jeshi la Polisi Tanzania kwa jitihada wanazochukua kukabiliana na ongezeko la ajali barabarani na lakini pamoja na jitihada hizo imejitokeza kero ambayo abiria wengi wanailalamikia kutokana na Bus hizo kufungwa ving'amuzi ama vidhibiti mwendo vinavyolazmisha Gari zisitembee zaidi ya Spidi 80 ambayo kiuharisia kwa safari za Bus hiyo spidi ni ndogo mnooo.

Kwa sasa kusafiri mikoani imekuwa kama adhabu sehemu ambayo zamani ulikuwa unasafiri masaa 9 let us say Dar Iringa sasa hivi utasafiri masaa 15,inachosha mnoo yani kama unajambo lako unawahi kijijini kwenu sahau kabisa,nadhani kwa masafa ya Mbeya Dar au Dar Arusha siku hizi unaweza kusafiri saa 24,too much boring mazee,hata kama tunapambana kudhibiti ajari but sio.kwa namna hii.

Ushauri:Ni vyema wakaangalia upya swala hilo la Spidi 80 waweke hata 100 atleast mana safari za mikoani si lelemama.

Naomba niishie hapa maana kengere ya msosi ishagonga hapa Kwenye Kambi ya wakimbizi KT na mimi nimeshakuwa Senior Villager so nimepewa jukumu la kuwaongoza new Villagers.
Jumatatu iliyopita nilikua natoka Dar nakuja songea asee balaa spidi mwisho 80 ikizidi kelele nimefika huku saa 6 badala ya saa 3 inaboa sana yaani
 
Back
Top Bottom