Wiki iliyopita nilisafiri na basi kwa jinsi nilivyoona mwendo nikahisi mwendo umeshapita km 80 kwa saa hivyo nikaingia kwenye application ya speedometer kwenye simu yangu.
Gari lilikuwa linakwenda zaidi ya km 90 kwa saa hata sehemu zenye kona kali. Nikamuuliza konda akasema eti speed haizidi 85.
Nikasikiliza kwa makini nikasikia sauti ya kidhibiti mwendo ikilia mfululizo lakini kwa sauti ya chini sana. Kumbe wanapunguza sauti halafu wanaenda mwendo kasi mwendo wanaotaka.
Wahusika limulikeni hili kama mlikuwa hamjui au mnajua maana maisha ya watu yanachezewa na vichaa.