Serikali ingilieni suala la mabasi kutembea kwa mwendo kasi

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,187
Wiki moja nyuma nilikuwa na safari ya kutoka Dar kwenda Shinyanga. Nimechukua gari mitaa ya Mwenge na kwenda kukata tiketi pale Shekilango.

Ndipo nikaangukia kwenye bus kampuni ya Ally’s star
Nauli VIP ni 120,000/=
Sisi kajamba nani ni 90-65k

Cha kushangaza niliambiwa muda wa reporting time ni saa 10 mpk 10:30 usiku na muda wa safari ni saa 11:00 Alfajiri.

Kweli siku ya safari ikafika aisee kutoka tuu Dar mpaka Morogoro huo mwendo sio wa kawaida bus inatupwa 100-120+

Kufika Singida ghafla tukawa bampa na bus kampuni ya Katarama gari imetupita kama tumesimama na 120+ yetu kuuliza wasema hiyo gari imetoka Dar saa 12:00 aisee gari zikaanza kufukuzana kufika Shinyanga ni kwenye saa 2:07 usiku gari zina overtake ovyo ovyo Mungu saidia

Wakati wa kurudi kutoka Shinyanga kuja Dar nikapanda bus (Katarama ya Mwanza) muda huo bus ya Shinyanga to dsm ni Ally’s ambayo ni 1 tuu kupata shida…

Kama kawaida hizi bus za Mwanza zikaanza kutimuana kuja kufika Kibaigwa nashangaa gari inataka kuipita mpaka gari iliyotokea Shinyanga yaani bus za Mwanza zinaipita gari ya Shinyanga

Ombi langu kwa Serikali wasisubiri mpaka vifo vitokee ndio waanze kutupa pole wakati wana uwezo wa kuzuia hii ishu mapema

NB:
 
Bumps za mita 5 urefu
Kila baada ya umbali gani maana kufukia mashimo wanajua kishenzi. Hapa penyewe wanatamani yasiwepo hayo matuta.

Hapo issue ni kusimamia sheria na taratibu bila kujali chombo/gari ni ya nani?
 
Unampigia mbuzi gitaa, swala la overspending lilianza kushughulikiwa wakati Sumaye akiwa waziri mkuu. Kipindi hicho kila Basi lilifungwa speed governor ya michongo. Watu wakauza speed governor wakatajirika , tukaachana nazo.

Wakaongeza alarm ili abiria wasikie na LATRA waone Kama gari imezidisha mwendo, nayo haikufanikiwa. wakasema trafik asindikize gari apande la mbele ili lisiovertakiwe, kiasi fulani kwa magari toka Mbeya mpaka mpaka na Iringa walifanikiwa , wakasema kila gari iwe na ratiba ili iwe rahisi trafik kuangalia limefika sehemu husika kwa muda au limewahi, (kipindi chote hicho trafik wanaporomosha majumba Mbagala na Kitunda)
Now they have run out of ideas.

Halafu wanaosimamia haya Mambo Ni wazee wa STK STL STM ambao speed zao wawapo barabarani Ni Kama ndege iliyoibiwa, wataweza kusimamia kitu wasicho amini?
 
HII NI KWELI.

Kwasasa KATARAMA wapo kwenye battle na ALLY'S , battle ambayo inachochewa na wanazi kule twitter, kwa sifa na wengine kubeti hela kabisa.

Hapo mwanzoni ALLY'S hakuwa na safari ya saa 11 alfajiri mpaka pale alipokuwa anafutwa na kutanguliwa na bus mpya ya KATARAMA. Kwakua gari zake ni mchina na kwamba haziwezi kushindana na SCANIA (Katarama) akaamua kubuni safari ya 11 alfajiri ili angalau awe na gari moja inayofika muda sawa na Katarama.

Sasa we fikiria gari iliyotoka Dar au Mwz saa 11 alfajiri, inatanguliwa na gari iliyotoka saa 12 alfajiri, humo njiani ni patashika.
 
Wiki moja nyuma nilikuwa na safari ya kutoka Dar kwenda Shinyanga. Nimechukua gari mitaa ya Mwenge na kwenda kukata tiketi pale Shekilango.

Ndipo nikaangukia kwenye bus kampuni ya Ally’s star
Nauli VIP ni 120,000/=
Sisi kajamba nani ni 90-65k

Cha kushangaza niliambiwa muda wa reporting time ni saa 10 mpk 10:30 usiku na muda wa safari ni saa 11:00 Alfajiri.

Kweli siku ya safari ikafika aisee kutoka tuu Dar mpaka Morogoro huo mwendo sio wa kawaida bus inatupwa 100-120+

Kufika Singida ghafla tukawa bampa na bus kampuni ya Katarama gari imetupita kama tumesimama na 120+ yetu kuuliza wasema hiyo gari imetoka Dar saa 12:00 aisee gari zikaanza kufukuzana kufika Shinyanga ni kwenye saa 2:07 usiku gari zina overtake ovyo ovyo Mungu saidia

Wakati wa kurudi kutoka Shinyanga kuja Dar nikapanda bus (Katarama ya Mwanza) muda huo bus ya Shinyanga to dsm ni Ally’s ambayo ni 1 tuu kupata shida…

Kama kawaida hizi bus za Mwanza zikaanza kutimuana kuja kufika Kibaigwa nashangaa gari inataka kuipita mpaka gari iliyotokea Shinyanga yaani bus za Mwanza zinaipita gari ya Shinyanga

Ombi langu kwa Serikali wasisubiri mpaka vifo vitokee ndio waanze kutupa pole wakati wana uwezo wa kuzuia hii ishu mapema

NB:
Aly 🌟 ndo michezo yao,waarabu pori jeuri Kama nini,lakin kwanini upande gari inakimbia hovyo wakati gari za kistaarabu zipo?mamlaka hazijal rushwa imetawala jali usalama wako ndugu
 
Back
Top Bottom