Kero katika saluni za kiume

Kero katika saluni za kiume

Msiwalaumu wanyozi,...hiyo kazi ina gharama zake; lazima kinyozi awe update na kinachoendelea worldwide...iwe ni siasa, mpira , etc. ili in case ukamuuliza kitu jibu ni hapo hapo...ndo utamu wa saluni.
 
Wewe bado unaenda Salon, siku hizi kuna Babershops unahudumiwa na professionals mpaka zile huduma ukihitaji unapatiwa
mkuu hili jukwaa lina linguistic professionals pia...hebu nikuulize tu; naomba tofauti ya barbershop na salon
 
unaenda saloon za namna hiyo. usione tabu kulipa elfu 5 kwaajili ya kichwa chako
 
mkuu hili jukwaa lina linguistic professionals pia...hebu nikuulize tu; naomba tofauti ya barbershop na salon
Salon ni premise amabayo mtaalam wa urembo na mitindo mbali mbali ya nywele na urembo hufanyia shughuli yake

Babershop ni premise ambayo shughuli zoote za kunyoa na kufanya mitindo mbali mbali ya nywele na ndevu pamoja na kupamba wanaume hufanyika.
 
Daaah we kijana leo umetoa article poa sana kwani tabia #4 me niliwahi kupigwa na Short aisee Shavuni ila niliambuli kunyolewa bure na Pole, Sasa sijui ningezimia ingekuwaje
najua umeshapoa mkuu..ila pole sana Nimecheka sana aisee
 
Nikienda salon nikikuta kuna kundi la watu ndani, naondoka

Nikienda salon nikimkuta kinyozi kanyoa na kuvaa kihuni naondoka..
Hili la watu kujaa ndani na hawana issue ya msingi hata mi hua naondoka fasta.
 
Salon ni premise amabayo mtaalam wa urembo na mitindo mbali mbali ya nywele na urembo hufanyia shughuli yake

Babershop ni premise ambayo shughuli zoote za kunyoa na kufanya mitindo mbali mbali ya nywele na ndevu pamoja na kupamba wanaume hufanyika.
kuna tofauti gani ya 1:UREMBO/MITINDO YA NYWELE na 2:KUNYOA (kufanya mitindo ya nywele)
 
Saloon za mikoani ukute kadada kameishatongozwa na mapredeshee ukiingia kuoshwa yaani kanakulipua ili uondoke haraka kanaona kama vile unakakera
 
Kuna hili la kulazimishana kukandwa na maji ya moto,mwenyewe anaogopa kushika kile kitambaa kilivyo cha moto. Lakini anataka kukukanda nacho usoni. Nilitaka kumpiga dada mmoja. Bila haya ananiambia mie mshamba,mshamba kwenye kuunguzwa?
 
unakuta kuna mziki unapigwa wa sauti ya juu na wavuta sigara ndani huko huko nachukia sana
 
Kwa kinyozi, ndo poa chini ya mwembe, kioo kimening'inizwa kwenye shina.

Wembe, mkasi, mashine isiyo ya Umeme, maji kidogo daaaah ukimaliza kinyozi anachukua kioo kingine kisha anaweka nyuma yako unajiona kichogo.

Jamaa ni kiboko haswa walikuwa WAMAKONDE.
 
Back
Top Bottom