Kero katika saluni za kiume

Kero katika saluni za kiume

the_forum

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2017
Posts
774
Reaction score
1,005
Kama kichwa cha habari kinavojieleza...kwakweli kuna tabia za vinyozi hua zina kera sana unapokua umeenda kupunguza nywele...

1; Unakuta kinyozi .anapokea simu anaanza kuongea huku anaendelea na kazi ya kukata nywele au anaweza akastop kazi husika na akaendelea kuongea na simu,na unakuta maongezi ya kipuuzi tu...kwakweli inakera sana!

2; Vinyozi wavivu,yeye kazi yake ni kukuzungusha kichwa kama steering vile anaendesha gari...yani yeye hataki kuzunguka,au hata kuzungusha kiti...kazi yake inakua ni kukuzungusha kichwa utasema anataka kuking'oa...kwakweli inakera.

3; Mashine mbovu mbovu, imekua tatzo sana ktk saloon nyingi skuiz...unakuta mashine inabadili mlio afu kinyozi anastop anachukua screw driver anaanza kuikaza kaza baadhinya nati...ikikaa sawa anaendelea na zoezi hilo ni endelevu...inaboa sana!

4; Kinyozi unakuta anakupitishia waya wa mshine mara shingoni,mara unapita kifuani,mara aushike aurishie kati kati ya miguu yako...inakua kero ...hajui kua ule ni umeme cjui...


Kwakweli kero ni nyingi wadau...leteni zenu hapa nahisi wahusika wakisoma watajirekehisha!
 
Unakuta umemuelekeza akunyoe style flani,jamaa unakuta anaongea mpaka anapindisha tofauti na ulivyomuelekeza,unajiuliza huyu anawezaje kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja,huku ananyoa,huku anapiga story na huku anaangalia TV ukutani..!
 
Unakuta umemuelekeza akunyoe style flani,jamaa unakuta anaongea mpaka anapindisha tofauti na ulivyomuelekeza,unajiuliza huyu anawezaje kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja,huku ananyoa,huku anapiga story na huku anaangalia TV ukutani..!
Mkuu nafikiri wakisoma watajua la kujifunza
 
Tena hizi ambazo zina Ac unakuta kuna kundi kubwa la watu ambao hawajaja kunyoa wapo tu hata personality zao zinatia mashika, kinyozi ananyoa anapiga story..mara awashe tv mara aweke sauti kubwa ya mziki.... utadhani umemwambia ndio kilichokuleta. ..ukimuelekuza analeta ujuaji.

Imefika hatua nachukia kuingia barber shop simply naingia ka saloon simple and smart kitaa basi.
 
Nikienda salon nikikuta kuna kundi la watu ndani, naondoka

Nikienda salon nikimkuta kinyozi kanyoa na kuvaa kihuni naondoka..
 
Back
Top Bottom