KERO: DAWASA Acheni kutuma SMS za madeni kwa wingi

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,567
10,554
Kwanza Maji yenyewe mnayatoa kwa mgao (Hamjatangaza tu), huku Tabata hasa Kinyerezi maji mnabangaiza kuyatoa. Mkijiskia ndio mnayaachia hamfati ratiba inayoeleweka.

Nirudi sasa kwenye KERO.

Mnatuma sana SMS zenu kila muda mnatuma hayo madude yenu. Kuweni na weledi basi na mkiwa mnafanya Automation mshirikishe wadau/wateja wawape mawazo yao.

Mnatuma sana hizo SMS zenu za kipuuuzi. Sasa wengine tumeunga nyumba mbili au zaidi kwa namba moja ya simu. Na kila nyumba itumiwe SMS 20 kwa siku hivi tutafika kweli?.

Tengenezeni User portal mteja awe anaingia huko na kuruhusu notifications kama anataka. Na kama hataki ana disable tu. Na malipo yote yanafanyika huko huko kwa kuunganisha API ya DAWASA na hizi API's za Mitandao ya Simu na Banks kama walivyofanya watu wa betting.

Haya maswala ya kutumiana SMS 20 kwa siku tutakuja kuonana wabaya.

Nimemaliza.
 
Screenshot_20231031_192456.jpg

Ndani ya Lisaa limoja mnatuma SMS 5 hapo tangia asubuhi mnatuma tu mataka taka yenu..
 
Ukitaka wasikutumie msg lipa bili on time, dawa ya deni ni kulipa
Sina mpango kabisa wa kulipa hili deni elfu 88,000. Hili deni limetokana na kitu ambacho sikijui.

Baada ya kuona maji hayotoki. Na wakiyaachia ilikuwa wanayaachia usiku mkubwa tukiwa tumelala.

Nikaachana nao nikachimba kisima. Alivyokuja msoma mita nikamwambia watoe mita yao. Nikamwambia pamoja na kwamba Umeme wanakata kata.

Lakini muda ambao umeme umekatwa hausomi. Kuanzia hapo wakawa wanaongeza 2000,2000.

Deni limetokana na matumizi ambayo sijayatumia na niliwaambia. Na nikawaambia silipi
 
Safi.

Mie mita ya hapa kwangu ilijaa ukungu nikawa najiuliza hawa watu wanasomaje hizi namba? Nikasema silipi mpk msoma mita nionane nae.

Wakaja kunikatia maji maana nilikaa miez 3 bila kulipa. Nikalipa wakarudisha maji.

Wakajichanganya kusoma mita kwemye nyumba nyingine wakaongeza UNIT ambazo sio sahihi deni likaja kubwa, mbona walinikoma pale ofisini kwao. Hapakukalika.
 
Kwanza Maji yenyewe mnayatoa kwa mgao (Hamjatangaza tu), huku Tabata hasa Kinyerezi maji mnabangaiza kuyatoa. Mkijiskia ndio mnayaachia hamfati ratiba inayoeleweka.

Nirudi sasa kwenye KERO.

Mnatuma sana SMS zenu kila muda mnatuma hayo madude yenu. Kuweni na weledi basi na mkiwa mnafanya Automation mshirikishe wadau/wateja wawape mawazo yao.

Mnatuma sana hizo SMS zenu za kipuuuzi. Sasa wengine tumeunga nyumba mbili au zaidi kwa namba moja ya simu. Na kila nyumba itumiwe SMS 20 kwa siku hivi tutafika kweli?.

Tengenezeni User portal mteja awe anaingia huko na kuruhusu notifications kama anataka. Na kama hataki ana disable tu. Na malipo yote yanafanyika huko huko kwa kuunganisha API ya DAWASA na hizi API's za Mitandao ya Simu na Banks kama walivyofanya watu wa betting.

Haya maswala ya kutumiana SMS 20 kwa siku tutakuja kuonana wabaya.

Nimemaliza.

Kama hutaki kuona SMS zao, i-spam tu hiyo namba au iblock...
 
Yeah, kuna watumishi wa Dawasco sio waaminifu, kuna wengi wamekumbana na kadhia kama yako na ukienda dawasco hupati msaada wowote
Wakikosea wao kukupa bill kubwa na ukalipa hawana REFUND. Na Kingine kama hujalipa wanastopisha usomaji mpk utumie mpk pale waliposoma kimakosa so kuna option ya kuilipa yote au kulipa kienyej (makadirio).
 
Taasisi nyingi za serikali zinafanya kazi kwa kubahatisha wakiwemo hawa tunaowaita Dawasco, Tanzania tunasafari ndefu sana
 
Back
Top Bottom