Wadau kulingana na taswira ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa, eneo la Mbezi Luis, ni eneo ambalo limekaa kimkakati katika kukuza uchumi wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla, cha kushangaza miundombinu yake ni mibovu sijapata kuona.
Kuna mtaa unaitwa Luis, leo ni karibu mwezi mzima, wananchi wanaacha magari barabarani, barabara haziingiliki, kuna barabara ambayo inaunganisha mtaa wa Luis kata ya Mbezi na Tegeta A kata ya Goba.
Ni barabara ya kimkakati lakini Serikali imeifumbia macho kabisa, kuna madaraja ya kujengwa hasa eneo linaloitwa kwa mama Ndeshi ndio kichomi kabisa.
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti, ili barabara hii waifanyie kazi, hasa kuweka daraja la kwa mama ndeshi.