Woga tupa kulee
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,752
- 1,311
inawezekana ni kweli unachosema, sina uhakika lakini habari za juu juu zinasema kuwa sheria za marekani zimetengenezwa kuwalinda watu wao na ICC, kwasababu sijazisoma izo sheria zao niiache tu hewani. however, laiti kama Bush na Ramsfed wangekuwa wamefanya makosa hayo baada ya mwaka 2002 icc statute ilipoanza kufanya kazi, international community ingewapigia kelele sana na kuna uwezekano marekeni wangeona hakuna jinsi ila kusalenda. pia ingewanyima ujasiri katika mambo mengi sana ya kidiplomasia. kitu kingine ni kwamba, wenzetu wakienda kupigana vita pamoja na kwamba wanavunja sana sheria za vita, wanapigana kisomi sana, wako radhi hata kutumia mabilioni ya dola alimradi kile wanachokifanya wajustify na sheria waonekane hawajavunja, wanaziba mianya yote ya ushahidi na wao wanajizatiti kwasababu wameforsee what might happen to them after the war, hivyo kwa viongozi wa marekani au hata uingereza kushitakiwa na mahakama hii ni vigumu kidogo. hata hivyo, sioni kama ni kitu kibaya hata kama icc ingekuwa kwa waafrika pekee alimradi inawashughulikia watu ambao kweli walifanya ukatili na mauaji kwa raia wasio na hatia. angalia Bagbo wa ivory coast, alivyo kataa kuachia madaraka baada ya uchaguzi, angalia hata kibaki alivyokataa kuachia madaraka pamoja na kwamba yeye hayuko kule, hivyo ni vitendo ambavyo utaviona africa tu, sehemu zingine za dunia huwezi kuviona, na hata kama icc ingekuwa inalalia upande mmoja wa waafrica tu, hiyo sio hasara kwetu wala si ukoloni mamboleo kwasababu inashughulikia viongozi ambao sisi waafrica wenyewe tusingeweza kuwashughulikia. HAYO NI MAWAZO YANGU TU LAKINI.nakuhakikishia kua as long as you and i are alive hakuna rais au rais wa zamani wa marekani au uingereza atapelekwa ICC. Hilo hata wewe unalijua