Hivi hii case ya bandari si inaweza kuhamishiwa Kwenye mahakama ya kimatifa (ICC)?

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
315
882
Kwanza itambulike kwamba SIO KWELI kwamba Watanzania hatutaki wawekezaji kutoka nje wala hatutaki kubinafsisha mifumo yetu ya uendeshaji. La ubinafsishaji unaruhusiwa Tanzania ndo maana huko Nyamango, Kahama n.k kuna wawekezaji kutoka nje.
Lakini pia katika uwekezaji huo tulionao mfano huko Nyamongo sio kwamba mikataba yake ipo vizuri, la lakini kama taifa hatutaki kurudia makosa yale yale miaka nenda miaka rudi.

Mkataba wa Dp world umeonesha mapungufu makubwa sana hasa kutokiweka wazi:
  • Thamani ya mali na rasilimali anazochukua kwa ajili ya kuendesha baandari zetu zote za Tanganyika.
  • Muda halisi wa wao kukaa kwenye huo mradi husika
  • Namna atakavyo wajengea uwezo na ubunifu vijana wa kitanzania ili baada ya miaka yake labda tuseme 20. Vijana wa kitanzania wao wenyewe waje wawekeze kwenye hiyo bandari.
  • yapo mengi ya kuingizwa kwenye mkataba kwa lengo kuiboresha bandari na kuwezesha win win situation.
Sasa kwa kuwa viongozi wetu wanaendelea ma hili jambo pasipo haya, vp kuhusu jambo hili kufikishwa The hugue kwenye mahakama ya kimataifa (ICC) kwa maana nimepita kazi zao nimeona pia wanashughulikia UHALIFU DHIDI YA BINADAMU NA UHALIFU WA UCHOKOZI. Nadhani serikali kiendelea na jambo hili angali wananchi wanalipinga nadhani huu ni UHALIFU DHIDI YA BINADAMU tena wenye nchi na ni UHALIFU WA UCHOKOZI dhidi ya watu waliowaweka madarakani.

Kwa sababu maandamo sio jambo linapendwa katika hizi ncho zetu za kiafrika. Nadhani mawakili wetu wasomi mnaweza kutumia hili jukwaa la ICC kuipeleka serikali huko kuanzia mkuu wa chi na wasaidizi wake walio husika kusaini huo mkataba.

Kufungua kesi ICC sio lazima kifunga safari hadi huko ulaya ila mawakili wetu mnaweza kuandaa nyaraka za namna serikali ilivyokiuka haki za wananchi kwa kuingia mkataba wa bandari unaolalamikiwa na wengi. Hili jambo nadhani litakuwa zuri endapo viongozi wetu watakapoanza kupandishwa kwenye vizimba vya ICC wataanza kuheshimu na kujua cheo ni dhamana leo ni kiongozi kesho unakuwa mkimbizi huko Italia.
 
Unawapelekea wale waliomsainisha Chifu Mangungo?

Wakamuingiza choo cha Kike.
 
Ni bandari tuh au kuna mengine mkuu
 
Watanzania hawajaridhika na Mkataba wa Bandari ya salama. Serikali isione haya kuachana na Waarabu
 
screenshot_2023-07-26_082547-jpg.2700387
 
Back
Top Bottom