Kenyatta na ICC; Watu na Maraisi wa Africa wana uwezo mdogo wa kufikiria?

kichangaa

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
689
0
ni kweli viongozi wa afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,hiki chombo cha icc ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina blair na bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia nchini iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
kwa nini viongozi walisaini mkataba wa icc??walilazimishwa?hiyo kesi itatumika kumblackmail kenyatta.WAZUNGU HAWAMWANGALII MTU USONI.WANAANGALIA MASLAHI TU.NUKTA.
 
NDESSA

JF-Expert Member
May 2, 2013
1,925
2,000
Ni kweli Viongozi wa Afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,Hiki chombo cha ICC ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata Viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina Blair na Bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia Nchini Iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
Mkuu nikukumbushe kitu kwamba Marekani sio mwanachama wa ICC bila shaka hata Uingereza hvyo hyo mahakama haina uwezo wa kuwatia hatiani kwa sababu hawakusign makubaliano na ICC.
 
Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,140
1,250
Kwani Bush na Blair wanatofauti gani na Kenyatta na Ruto? Are the 2 white men half gods and more superior then the 2 black men? That it is somehow acceptable for the former to kill human beings merely because of their wealth but it's appalling and unacceptable if a less wealthy person kills other human beings?

Kwaio tukubali tu kuwa such injustices are common in the justice system hivyo basi tuendelee tu. Sasa isn't that self defeating in itself. How can justice be served in an unjustice organisation?
 
NDESSA

JF-Expert Member
May 2, 2013
1,925
2,000
viongozi wa africa hawana ujuzi wa sheria za kimataifa, halafu wanasikia tu icc icc lakini hata hawaijui. hii ni pamoja na wakenya wote, as if kenya hakuna hatam wanasheria mmoja mwenye uelewa wa sheria za jinai ya kimataifa (international criminal law). kwa kifupi hiyo ni aibu sana kwa waafrica wote, sijui labda kwasababu viongozi wetu huko ikulu kwao hawana washauri wa kisheria au nini, kama wangekuwa nao basi wangeongea kwa akili. kenya walipewa nafasi ya kuweka mahakama palepale kenya au kutumia mahakama zao zilizopo, lakini hawakuitumia nafasi hiyo. koffi annan, mkapa na international community walijitahidi sana, hadi ocampo anakuja kenya, kila mtu alijua kenya are not willing to prosecute perpetrators. Ruto alipinga mahakama za kenya kufanya kazi hiyo na akasema bora twende icc....

kulingana na article 17 of the ICC statute, which talks about principle of complimentarity, kama kosa linaloshitakika na mahakama ya icc likitokea na nchi ikawa haiko willing kutumia local courts, hawana uwezo (labda ni failed state kama somalia), au wamefanya gelesha ya kushitaki lakini ili kumlinda perpetrator etc. nchi husika imepewa nafasi ya kwanza kutumia mahakama zake za ndani, kama haitafanya hivyo hapo ndo icc inaingilia kama mwaka mmoja umeshaisha na nchi haijachukua hatua. kenya walimaliza zaidi ya mwaka wanabembelezwa watumie mahakama yao hawakufanya hivyo, walivyoona kitu kimetinga icc, wanakuja wanalialia na viongozi wa africa wanashabikia na kutetea. hivi akili za mwafrica zitafumbuka lini?
Mkuu maelezo mazuri kabisa!
 
NDESSA

JF-Expert Member
May 2, 2013
1,925
2,000
Namkumbusha mleta uzi kuwa Rwanda sio member wa ICC na hata zile kesi za mauaji ziliundiwa mahakama maalum INTERNATIONAL CRIMINAL TRIBUNAL FOR RWANDA(ICTR) na iliwekwa Arusha kwasababu Rwanda wakati huo kulikuwa na political instability,nataka kuweka sawa kwamba ICC haijahukumu kesi za Rwanda, Lakini sioni shida kwa nchi zilizosign mkataba wa ICC na kama viongozi wake wamefanya uharifu kama watashitakiwa huko bila kujali kwamba kuna kiongozi mwingine hakupelekwa na tukumbuke pia tunapomzungumzia G. Bush tujue kuwa Marekani sio member wa ICC.
 
mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,531
0
Ni kweli Viongozi wa Afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,Hiki chombo cha ICC ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata Viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina Blair na Bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia Nchini Iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
good point...huwezi ku pick n choose nani wa kumshtaki mpaka leo hii bush hajakamatwa hivi bush na kenyatta nani muuaji zaidi...hao wazungu wasituzingue wamuache kijana aongoze nchi
 
montroll

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
318
250
Obama ameamua kuto tembelea KE na inasemekna sababu moja wapo ni kutounga mkono juhudi za kenyata za kugomea icc na kujaribu kujisafisha. Hii inamaana haendi KE sababu anaunga mkono Icc.
Marais wa afrika kama wanaubavu bac waache kutembelea Uk na US kushinikza viongozi wa huko nao wapelekwe Icc.
Hapo tutajua kweli wanamaanisha angalau.
 
montroll

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
318
250
good point...huwezi ku pick n choose nani wa kumshtaki mpaka leo hii bush hajakamatwa hivi bush na kenyatta nani muuaji zaidi...hao wazungu wasituzingue wamuache kijana aongoze nchi
Kwa hiyo unamaana wezi wote tz kwa mfano wasishtakiwe hadi hapo akina chenge washtakiwe?
 
Crucial Man

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
3,406
2,000
Ni kweli Viongozi wa Afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,Hiki chombo cha ICC ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata Viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina Blair na Bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia Nchini Iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
wao sio wanachama wa rome statu..icc inadeal na member states only.
 
sina-ajira

Senior Member
May 1, 2013
136
0
Mkuu nikukumbushe kitu kwamba Marekani sio mwanachama wa ICC bila shaka hata Uingereza hvyo hyo mahakama haina uwezo wa kuwatia hatiani kwa sababu hawakusign makubaliano na ICC.
Hawakusaini Makubaliano kwasababu walijua kwa kufanya hivyo kungewapa uhuru wautakao wa kupanga,kuratibu na kusimamia mipango yao ya kuvamia mataifa mengine moja kwa moja kijeshi au kupitia vibaraka wao ili kusimika mirija yao ya unyonyaji wa rasilimali wa mataifa hayo hali ingekuwa tofauti kama wangejiunga na ICC maana hata Iraq wasinge ivamia cha kushangaza ni kwamba Mataifa hayo hayo ya Marekani na Uingereza ndio yanayotoa msukumo mkubwa kwa ICC kuhusu kukamatwa kwa baadhi ya Viongozi wanao waona hawana Maslahi kwao.Hutasikia Mataifa yakimtaka Mkapa ICC kwa ishu za Visiwani kwasababu ya wema aliowafanyia katika rasilimali za Nchi hii.Wanamuandama Kenyatta kwasababu wanamjua vyema yule hawana chao Kenya.Na pengine wanazitolea macho estates anazozimiliki Kenyatta.Just thinking.
 
Crucial Man

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
3,406
2,000
Mbona tunakuwa na simpathy za ajabu ajabu humu? Viongozi wa Africa wanajaribu kuwatetea hao ma criminals.,wakenya walipema nafasi ya kuanzisha mahakama yao wenyewe..ruto uhuru pamoja na wapambe wao walisimama kidete na kupaza sauti,'tuacheni twende kwa ocampo sisi atumuogopi' walitumia swala la Icc kukonga mioyo ya jamii zao,..walitumia Icc kama chompo cha kufanyia kampeni,mwisho wa siku wakapata urais..sasa leo wanalia kwa nini? Msiwaonee uhuma waliyataka wenyewe..
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
viongozi wa kiafrika ni wanafki wakubwa wanapenda kulalamika pasipo sababu wenyewe walipokua wanatia saini kujiunga na ICC walikua mbumbu mithili ya mangungo wa msovero sasa hivi wanalalamika ujinga tu.
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
2,901
2,000
Yote hiyo ni kutafuta uhalali wa kuua raia wao. ICC should be there ili viongozi wahuni kwa kiasi waogope kuleta machafuko katika nchi zao.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,875
1,500
Ni kweli Viongozi wa Afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,Hiki chombo cha ICC ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata Viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina Blair na Bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia Nchini Iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
Bush hawezi kushitakiwa/kupelekwa ICC kwasababu USA hajaridhia/kusign mkataba wa ICC. Lakini ma-viongozi yote ya KIAFRIKA yamesign mkataba wa ICC.

Huyo Huyo Museveni anayelalamikia ICC sasa, aliwahai kumwambia Bashir Rais wa Sudan kwamba akikanyaga tu Uganda anamkamata na kumpeleka ICC kwasababu anatafutwa kwa makosa ya genocide. Leo eti Museveni anaiponda ICC na wewe unamuona SHUJAA!!

VIONGOZI WA KIAFRIKA ARE FULL OF HYPOCRISY.
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,447
2,000
Subiri Boss wao Obama awakomalie uone kama kuna mtu ataongea..wote watajificha...
 
DaPilly

Senior Member
Mar 2, 2012
178
225
ni kweli viongozi wa afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,hiki chombo cha icc ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina blair na bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia nchini iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
umeonaeeeeee!!!
 
Marry Hunbig

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,685
2,000
Mkuu nikukumbushe kitu kwamba Marekani sio mwanachama wa ICC bila shaka hata Uingereza hvyo hyo mahakama haina uwezo wa kuwatia hatiani kwa sababu hawakusign makubaliano na ICC.
Kwani Bush na Blair wanatofauti gani na Kenyatta na Ruto? Are the 2 white men half gods and more superior then the 2 black men? That it is somehow acceptable for the former to kill human beings merely because of their wealth but it's appalling and unacceptable if a less wealthy person kills other human beings?

Kwaio tukubali tu kuwa such injustices are common in the justice system hivyo basi tuendelee tu. Sasa isn't that self defeating in itself. How can justice be served in an unjustice organisation?
Namkumbusha mleta uzi kuwa Rwanda sio member wa ICC na hata zile kesi za mauaji ziliundiwa mahakama maalum INTERNATIONAL CRIMINAL TRIBUNAL FOR RWANDA(ICTR) na iliwekwa Arusha kwasababu Rwanda wakati huo kulikuwa na political instability,nataka kuweka sawa kwamba ICC haijahukumu kesi za Rwanda, Lakini sioni shida kwa nchi zilizosign mkataba wa ICC na kama viongozi wake wamefanya uharifu kama watashitakiwa huko bila kujali kwamba kuna kiongozi mwingine hakupelekwa na tukumbuke pia tunapomzungumzia G. Bush tujue kuwa Marekani sio member wa ICC.
good point...huwezi ku pick n choose nani wa kumshtaki mpaka leo hii bush hajakamatwa hivi bush na kenyatta nani muuaji zaidi...hao wazungu wasituzingue wamuache kijana aongoze nchi
Hawakusaini Makubaliano kwasababu walijua kwa kufanya hivyo kungewapa uhuru wautakao wa kupanga,kuratibu na kusimamia mipango yao ya kuvamia mataifa mengine moja kwa moja kijeshi au kupitia vibaraka wao ili kusimika mirija yao ya unyonyaji wa rasilimali wa mataifa hayo hali ingekuwa tofauti kama wangejiunga na ICC maana hata Iraq wasinge ivamia cha kushangaza ni kwamba Mataifa hayo hayo ya Marekani na Uingereza ndio yanayotoa msukumo mkubwa kwa ICC kuhusu kukamatwa kwa baadhi ya Viongozi wanao waona hawana Maslahi kwao.Hutasikia Mataifa yakimtaka Mkapa ICC kwa ishu za Visiwani kwasababu ya wema aliowafanyia katika rasilimali za Nchi hii.Wanamuandama Kenyatta kwasababu wanamjua vyema yule hawana chao Kenya.Na pengine wanazitolea macho estates anazozimiliki Kenyatta.Just thinking.
Bush hawezi kushitakiwa/kupelekwa ICC kwasababu USA hajaridhia/kusign mkataba wa ICC. Lakini ma-viongozi yote ya KIAFRIKA yamesign mkataba wa ICC.

Huyo Huyo Museveni anayelalamikia ICC sasa, aliwahai kumwambia Bashir Rais wa Sudan kwamba akikanyaga tu Uganda anamkamata na kumpeleka ICC kwasababu anatafutwa kwa makosa ya genocide. Leo eti Museveni anaiponda ICC na wewe unamuona SHUJAA!!

VIONGOZI WA KIAFRIKA ARE FULL OF HYPOCRISY.
umeonaeeeeee!!!
ni muhimu sana kuelewa jambo hili kwamba, ICC ni mahakama ya kimataifa iliyoanza kufanya kazi mwaka 2002. na haichagui mtu wala nchi, nchi iwe imesaidi au haijasaini, kama watu wake watafanya makosa ya kimataifa na wakawa hawajachukuliwa hatua na nchi zao, ICC itaingilia na kuwatolea arrest warrant baada ya preliminary investigation kama ilivyokuwa kenya na nchi zingine.

tusichanganye jambo hili na ICTR hapo Arusha (kwa Rwanda) ambapo makosa ya Rwanda yalifanyika mwaka 1994 tu. remember ICTR inashughulikia makosa yaliyofanyika mwaka 1994 tu na ndani ya Rwanda na nje yake alimradi yawe yalikuwa na connection ya kitu kile kinachofanyika Rwanda wakati wa mauaji yale.

USA, SUDAN na nchi zingine nyingi tu hazijasaini Rome statute of International Criminal Court (ICC), lakini bado tu kama wakifanya makosa yanayokinzana na sheria ile na wakawa hawajashughulikiwa na nchi husika watakamatwa tu na kupelekwa ICC. ndivyo tulivyoona kwa al bashir wa sudan.

hatuwezi kuwazungumzia Bush na Ramsfed kwa sasa, kwasababu je? makosa waliyoyatenda, yalitendeka baada au kabla ya mwaka 2002? kama yalitendeka wakati ICC STATUTE ipo in force, wangeshapelekwa jambo lao kule ICC, nchi nyingi zimejaribu hili lakini wanaona kuwa mambo waliyoyafanya iraq etc waliyafanya kabla icc statute haijaanza kufanya kazi. huwezi kumshitaki mtu kwa kutumia sheria ambayo wakati kosa linafanyika haikuwepo.

pili, ICC iliundwa in order to replace ad hoc tribunals...AD HOC TRIBUNALS NI NINI? ni mahakama hizi mbadala kama vile ICTR, ICTY, special tribunal for Lebanon na Special tribunal for Sierra Leone na ile ya Cambodia pia. jumuiya ya kimataifa iliona kuwa, hatuwezi kuwa tunaunda mahakama ya eneo fulani tu kiwa wakati makosa ya aina hii yakifanyika, bora tuunde mahakama moja itakayoshughulikia mambo yote haya. ndipo ikaundwa ICC. this means that, ICTR, ICTY na hizo zingine, ziko limited only to offences committed during certain period of time. makosa yeyote yale ya kimbari au halaiki etc yakifanyika leo Rwanda au Yugoslavia ya zamani wakosaji hawawezi kupelekwa ICTR au ICTY, bali ICC.

lengo la kuwepo icc ni kufuta vimahakama vinavyoundwa eneo kwa eneo kila wakati. utaona kuwa ICTR hapo arusha inamalizia kabisa shughuli zake na mwakani wanafunga jengo kabisa, hakutakuwa na ICTR tena, bali ICC kama kuna makosa yaliyofanyika baada ya 2002. we are no longer going to have ad hoc tribunals in this world, ITAKUWA MAHAKAMA MOJA TU.

hivyo, tusichanganye ad hoc tribunals na icc, pia tusilaumu kwamba icc inawaonea waafrica, kwasababu ukiulizwa swali, kuna nchi gani ulaya, america, asia etc ambayo imefanya makosa yanayotakiwa yapelekwe icc katika kipindi kuanzia mwaka 2002,unaweza kukosa jibu. kama ipo, basi jumuiya ya kimataifa ingesha refer the matter to the Hague muda mrefu., security council, state parties au prosecutor himself proprio mottu angeshaanzisha upelelezi. i have so much to write about this matter lakini naomba nipishe wenzangu waandike...kwa upande wangu, nafikiri yatupasa tushukuru kwamba ICC inawashughulikia viongozi wa africa eg. Gbagbo etc, utamtetea mtu kama yule kwa alichofanya? je? icc ingemwacha tu kwa kuogopa kuwa wangeonekana kuwaonea waafrica?

viongozi wa africa wamekosa kitu cha kujadili hadi wanapoteza muda badala ya kujadili maendeleo na kuondokana na umasikini wa nchi zao wao wanajadili kupinga icc? kwa wale waliosaini mkataba walifikiri wanasaini nini? hawakuusoma kwanza mkataba wa Roma?

kwa kumalizia, the very possible offences among others ambazo Bush na mwenzake wangeshitakiwa ili kuwa ni kosa la AGGRESSION, ambalo katika ICC STATUTE halijaanza kufanya kazi, kulikuw ana mkutano kampala mwaka 2010 kujadili hilo lakini limeahirishwa hadi mwaka 2017 watakapokutana kujadili kama lianze kufanya kazi au la. likianza kufanya kazi, basi viongozi wa nchi watakaoamrisha nchi zao kuvamia nchi za wenzao watakamatwa viongozi hao. hii imewekwa dhahiri kuwatageti wamarekani na waisrael. kwa habari ya crimes against humanity, war crimes na genocide, inahitajika ushahidi mzito sana kuwapata bush na mwenzie, hata hivyo, inasemekana makosa hayo waliyafanya kabla ya 2002 hivyo ICC haina nguvu kwao. waliponea hapo.
 
Crucial Man

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
3,406
2,000
Ni aibu kubwa mtu kumshabikia m7 wakati yeyd ni dikteta namba moja Africa...kuna report imetolewa juzi kenya kwamba hawa mabwana wawili waliusika njia moja au nyingine kuchochea gasia kenya...hawa jamaa wanajaribu kuwadrag viongozi wa Africa kwenye personal issues zao.
 
andate

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
2,653
1,225
Sina tatizo na SHERIA kumchukua mkondo wake kabisa ila kwanza watuondolee huu mtazamo kwamba wao ni wanafiki linapokuja katika suala la nani anastahili kuitwa MHALIFU wa haki za Binadamu kwa kuwakamata akina Blair na Bush kwanza walioudanganya Ulimwengu kuwa Utawala wa Saddam Hussein ulikuwa umehodhi Silaha za Maangamizi ya Halaiki kabla ya kuja kugundulika baadaye kuwa walidanganya.Siku wakikamatwa hawa wawili basi Waafrika hatutakuwa na matatizo na ICC na tutaridhia hata kwa Kenyatta kukamatwa.Na hii pia itawarudia Watawala wa Kiafrika kwa namna walivyo wepesi kuyashughulikia makundi ya Kiraia yanapo dai haki zao na kuwaita WAVURUGA AMANI ila wamekuwa wazito sana kuwashughulikia MAFISADI na WAHUJUMU UCHUMI na kadhalika.
Ukisoma vizuri maelezo ya mdau hapa chini utapata majibu mengi ya maswali yako.

viongozi wa africa hawana ujuzi wa sheria za kimataifa, halafu wanasikia tu icc icc lakini hata hawaijui. hii ni pamoja na wakenya wote, as if kenya hakuna hatam wanasheria mmoja mwenye uelewa wa sheria za jinai ya kimataifa (international criminal law). kwa kifupi hiyo ni aibu sana kwa waafrica wote, sijui labda kwasababu viongozi wetu huko ikulu kwao hawana washauri wa kisheria au nini, kama wangekuwa nao basi wangeongea kwa akili. kenya walipewa nafasi ya kuweka mahakama palepale kenya au kutumia mahakama zao zilizopo, lakini hawakuitumia nafasi hiyo. koffi annan, mkapa na international community walijitahidi sana, hadi ocampo anakuja kenya, kila mtu alijua kenya are not willing to prosecute perpetrators. Ruto alipinga mahakama za kenya kufanya kazi hiyo na akasema bora twende icc....

kulingana na article 17 of the ICC statute, which talks about principle of complimentarity, kama kosa linaloshitakika na mahakama ya icc likitokea na nchi ikawa haiko willing kutumia local courts, hawana uwezo (labda ni failed state kama somalia), au wamefanya gelesha ya kushitaki lakini ili kumlinda perpetrator etc. nchi husika imepewa nafasi ya kwanza kutumia mahakama zake za ndani, kama haitafanya hivyo hapo ndo icc inaingilia kama mwaka mmoja umeshaisha na nchi haijachukua hatua. kenya walimaliza zaidi ya mwaka wanabembelezwa watumie mahakama yao hawakufanya hivyo, walivyoona kitu kimetinga icc, wanakuja wanalialia na viongozi wa africa wanashabikia na kutetea. hivi akili za mwafrica zitafumbuka lini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom