Yaaani jamani hivi watanzania hasa viongozi wa umma wanasikilizia wapi?
Hapa kinachotakiwa kwenye katiba mpya ijayo tuweke kipengele cha kuwa :Rais akifanya jinai basi ashitakiwe na kuchukuliwa hatua kisheria.maana tukifanya hivyo moja kwa moja tutakuwa tumeweka wazi kuwa kiongozi anawajibishwa,kuliko katiba ya sasa ambayo ibara ya 45 na 46 zina mpa kinga mtawala kitu ambacho huwafanya kufanya makosa kwa makusudi.
Mfumo wetu wa kiutawala sio mzuri unawapendelea sana viongozi na wana siasa.kwa maana hiyo Rais amelundikiwa madaraka mno kiasi ambacho yanamshinda na badala yake mam:hungry:bo yanakwenda hovyo hovyo na kuonekana kama vile serikali imekwenda likizo kumbe ipo.