Kenya na Uganda kufanya uuzaji wa pamoja ili kuvutia watalii wa nje

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Kenya na Uganda zinatarajiwa kuanza kufanya shughuli za uuzaji wa pamoja ili kuvutia watalii kutoka nje.

Akiongea kwenye uzinduzi wa maonesho ya barabarani yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Uganda (UTB), Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Waendesha Utalii wa Kenya Fred Kaigua amesema jijini Nairobi kuwa ushirikiano wa wadau wa utalii wa Kenya na Uganda utasaidia sekta hiyo kuondokana na athari za janga la UVIKO-19. Amesema sekta hii ina uhusiano wa karibu kwasababu wana vivutio vya aina mbalimbali ambavyo vitahimiza wageni kufika kwenye kanda hiyo.

Naye meneja mauzo wa UTB, Clare Mugabi amesema ukuaji wa sekta ya utalii nchini Kenya pia utaleta athari chanya kwenye sekta ya usafiri ya Uganda, kwani watalii wa kigeni watakaokwenda Kenya na baadaye kwenda Uganda watapata uzoefu mzuri wa usafiri kupitia urithi ulioshiba wa utamaduni wa Afrika.
 
Hakuna nchi duniani isiyokuwa na vivutio vya utalii.

Mtu anaweza akashangaa kwa nini nchi kama ya Ufaransa inaongoza kwa kupata watalii wengi kushinda nchi yoyote duniani wakati hawana hata zoo tu achilia mbali mbuga za wanyama.

Ndipo tunakuja kugundua kwamba kumbe sio mbuga za wanyama tu eti ndio vivutio vya utalii. Kuna watu wanaopenda kwenda sehemu yoyote kwa ajili ya kubadili mawazo tu.

Ingekuwa kwamba swala la utalii ni kuona tu wanyama basi Tanzania ingekuwa inaongoza kwa kupata watalii wengi kushinda nchi yoyote duniani na kwa hayo mapato nchi isingekuwa imeparara hivi.

Hivyo tunakuja kugundua kwamba utalii ni zaidi ya kuona wanyama.
 
Well Noted Mkuu
 
Kuna nchi inaenda kupigwa hapo. Watu watashukia Nairobi, Naivasha kufika Uganda hela zimeisha.
Kenya janja janja sana.
 
Back
Top Bottom