Kenya kujenga kituo cha Umeme wa Nyuklia chenye kugharimu dola Bilioni 5 na kuzalisha Megawati 4000

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Kenya kujenga kituo cha umeme wa nyuklia chenye kugharimu dola bilioni 5 kinu hicho kinatarajiwa kuwa kitazalisha umeme wa Megawati 4000

Shirika la Nishati ya Nyuklia la Kenya (NuPEA) limewasilisha ripoti kuhusu mpango wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa nyuklia ambacho ujenzi wake unatazamiwa kugarimu dola bilioni 5.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg, ujenzi wa kituo hicho unakaribia kuanza na kitazinduliwa katika kipindi cha miaka saba ijayo.

Shirika la Nishati ya Nyuklia la Kenya limewaswilisha ripoti ya ujenzi huo kwa Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa MazingiraKenya (NEMA) huku ripoti zikisema serikali ya Kenya inapanga kuzalisha megawati 4,000 za nishati ya nyuklia ifikapo mwaka 2035.

Baada ya NuPEA kuwasilisha ripoti hiyo kwa NEMA, wananchi wa Kenya wanatazamiwa kujadili masuala ya kimazingira yanayohusiana na ujenzi wa kituo hicho cha nyuklia.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza azma ya kuhakikisha kuwa uzalishaji umeme wa Kenya unaimarishwa kutoka megawati 2,712 hivi sasa hadi megawati 22,000 ifikapo mwaka 2031 ili kuimarisha sekta ya viwanda katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi mashariki mwa Afrika. Kituo hicho cha nyuklia nchini Kenya kinatazamiwa kujengwa katika Kaunti ya Tana River iliyo katika eneo la pwani
 
The nuclear agency of Kenya has submitted impact studies for a $5bn nuclear power plant. It hopes to commence operations at the plant before 2027. An agency spokesperson said the country is looking to expand have 1GW of nuclear capacity operational by 2035. The agency considers a site in Tana River County, near Kenya’s coast, as the preferred location for its first plant.

Despite the ongoing Covid-19 pandemic, China added 11.52GW of solar capacity during the first half of 2020, compared with 11.4GW in the first half of 2019. Data released by the National Energy Administration says that large-scale solar installations accounted for 7.08GW, while distributed solar accounted for 4.43GW. At the end of June this year, the cumulative solar capacity of China reached 216GW.

Canadian Solar has started construction on its 10MW Groß Siemz solar power plant in Germany. Located across an 11-hectare area near the city of Schönberg, the project will use more than 22,900 pieces of high-efficiency mono-PERC modules. GS Solar, the customer and project owner, will connect the plant to the grid in October this year.

Thai energy company Banpu has reached an agreement to acquire the 37.6MW El Wind Mui Dinh onshore wind farm in southern Vietnam, in a deal valued at $66m. The investment was made through BRE Singapore, an associate company in which Banpu owns a 50% stake through Banpu Next Co.

Source: Power Technology
 
Kwa wizi wa viongozi wa kenya,, nawasiwasi na huu mradi.. Viongozi wa kenya ni waroho na mafisadi sana.. afrika tunAkwamishwa sana na viongozi wetu aisee.
 
Mulisema hivyo kwa sgr, Lamu port, Mombasa port expansion,Nairobi expressway etc. Lakini mungu ni nani, anazidi kuaibisha kamati ya roho mbaya na wachawi. Na bado mujitayarishe kupiga ramli usiku na mchana maana Kenya haismami.
Japan walizima vinu vyote vya nuclear lakin nyie ndio mnavikimbilia,kikibuma kukipooza madhara yake ni makubwa sana
 
Japan walizima vinu vyote vya nuclear lakin nyie ndio mnavikimbilia,kikibuma kukipooza madhara yake ni makubwa sana

Japan ni Japan, Kenya ni Kenya, kila nchi ina mazingira yake, kule Japan huwa wanakumbwa na tetemeko la ardhi mpaka kila kitu kinayumba, Afrika hapa tumebarikiwa tuna hali nzuri ya mazingira, ni muda wetu wa kupaa na sio kwa ungo.
 
Japan ni Japan, Kenya ni Kenya, kila nchi ina mazingira yake, kule Japan huwa wanakumbwa na tetemeko la ardhi mpaka kila kitu kinayumba, Afrika hapa tumebarikiwa tuna hali nzuri ya mazingira, ni muda wetu wa kupaa na sio kwa ungo.
Sawa dingi yangu ni Hayo tu
 
Mh kwa kilicho wqkuta wa lebanon na nyie iwe fundisho icho kinu chwnu mkijengwe kulee karibu na Al shabaab ilikiki lipuka kuwafumukie majihadist
 
Sisemu kama Kenya haina huwezo laa , ila hii ni mbinu ya uhuru katika kujitengenezea mazingia ya kuchaguliwa tena ili apate ushawishi Kwa kutumia mbinu ya miradi mikubwa ya mda mrefu baadae hata asipo itekeleza anakua tayari kashachaguliwa .

Miaka 7 mingi mno !! Kwahiyo hii ni ahadi isiotekelezeka ila ina lengo la kuhadaa fikra za waliowengi bc wala si vingine.
 
Hii nafasi ya tenda ya $5b inafurahisha mifisadi sana. Mwishowe kama tu vile nauli SGR ipo un-affordable kisa mradi wa kinyonyaji, hivyo tu ndivyo umeme utakuwa un-affordable kenya.
Tanzania musikurupuke, tumieni mito na gesi mliopewa bure na mungu kuzalisha umeme..Technologia yake ipo simple sio lazima mzungu ama mchina akuendeshee kiwanda cha gesi/hydro. Tukumbe hadi leo, SGR ya kenya inaendeshwa na mchina
 
Back
Top Bottom