Kenya inakosea kuhusu Corona ya Tanzania

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,795
2,000
Watanzania pia Ni binadamu wanaoogopa kufa. Isingewezekana mtu aache kujifungia (lockdown), kunawa mikono, kujisanitize, kuvaa barakoa na kukaa mbali Kama jirani zake, wafanyakazi wenzake, wanachezaji wenzake, wafanyabiashara wenzake, wanafunzi wenzake na ndugu na jamaa zake wangekuwa wanakufa kwa COVID-19.

Ukiona watu hawavai barakoa Ni ishara kuwa mambo Ni shwari kweli huko mitaani, kwenye familia, makazini, viwanjani na mashuleni wanakoishi, wanakofanyakazi, wanakosoma na wanakocheza

Kenya Ina raia wake wengi ambao wako Tanzania kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia, kisiasa , kikazi, kibiashara, kijamii na kimichezo. Je, Kuna raia wake yuko Tanzania amekufa kwa CORONA? Tuna wachezaji wa Kenya wanacheza ligi ya Tanzania, je wamekufa kwa COVID-19?

Shule na vyuo vyote vimefunguliwa watoto wanasoma, Kama kungekuwa na Corona iliyokithiri lazima ingefahamika tu.

Hatukatai kwamba COVID-19 haipo Tanzania lakini sio kwa kiwango wanachofikiria wakenya. Malaria, TB, minyoo, na ajali za bodaboda Ni nyingi kuliko COVID-19.

Kwanini ujihangaishe kuwapima watu wasiokuwa na dalili kujua Kama Wana corona au hawana. Mbona hatufanyi hivyo kwa magonjwa mengine?

Hata Malaria na typhoid, Kama ukiwapima damu zao watu woote dar es Salaam lazima utakuta wengi Wana vimelea vya malaria na typhoid kwenye damu yao. Unawapima kwa madhumini gani? Je, mnafahamu wakenya wote Wenye maambukizi ya TB, Leprosy, malaria, saratani, na minyoo kwenye miili yao? Mbona hamuwapimi (screen) kufahamu idadi yao? Why corona?

CORONA ipo lakini sio Kama wanavyoikuza Kenya, muulizeni mchezaji wenu mmoja Kama shihata, shikalo wawaeleze ukweli wa hali ya corona Tanzania maana wapo huku, waulizeni wafanyakazi wa KCB na KCB maana wako huku wanawahudumia WATU ILI WAWAAMBIE UKWELI WA HALI HALISI YA COVID-19 Tanzania.

Mtajifungia hadi lini ndugu zetu?
 

Barca

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,083
2,000
Uko sahihi sana mkuu. Ndo maana magonjwa mengi tunapima wagonjwa wakija hospitali. Right tungekuwa tunapima kila mtu watu karibu wote wangekuwa na maambukizi
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,795
2,000
Kenya wanajipendekeza sana
Ukoloni bado haujawaisha vichwani, wao bila ya misaada ya wazungu wanaona dunia itasimama. Lazima waongee kiingereza hata na ng'ombe wakati wa kuwachunga na kuwakamua. Bila kiingereza dunia yao itasimama
 

mzalendoalltz

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
767
1,000
Wamuulize Kahata anaechezea Simba maana yeye anaenda bar, sokoni bila hata barakoa. Nafikiri atawapa story nzuri zaidi.
Kwa sasa Corona imepotea kwa kiasi kikubwa sana ila nina waswasi wakifungua mipaka itaanza tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom