Kenya: Familia yalazimika kutumia trekta kusafirisha maiti sababu ya barabara mbovu

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,282
Familia ya Kirui ililazimika kutumia trekta kuusafirisha mwili wa mpendwa wao kutoka hifadhi ya maiti kutokana na hali mbovu ya barabara iliyosababishwa na mvua kubwa.

Mwili huo ulikuwa unasafirishwa hadi kijiji cha Kapsita kwa ajili ya mazishi jinsi Citizen TV ilivyoripoti Ijumaa, Septemba 11. Marehemu aliaga dunia Septemba 4 ila hospitali ya Elburgon ilidiinda kuipa familia yake mwili.

Kutokana na hali mbovu ya barabara ya Mau-Kapsita, jamaa zake hawakuwa na budi ila kutafuta trekta ya kumsafirisha marehemu mwenye umri wa miaka 58 hadi nyumbani.

Wakazi waliilaumu serikali ya kaunti kwa miundo mbinu msingi duni katika eneo hilo. Kisa sawa na hicho kilitokea kaunti ya Nyandarua mwaka wa 2019 baada ya gari lililokuwa limembeba Alice Njoroge kukwama kwenye matope kutokana na hali mbovu ya barabara.

Juhudi za kujaribu kuliondoa gari hilo katika matope hayo ziligonga mwamba huku familia yake ikilazimika kukomboa huduma za punda kuusafirisha mwili wa mwenda zake hadi kwao eneo la Shamata.

Read more: Familia yalazimika kutumia trekta kusafirisha maiti sababu ya barabara mbovu
 
Back
Top Bottom