Keki yenye rangi ya CCM yakataliwa!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
Halima Mdee Mbunge wa Kawe akigeukia pembeni na kuonyesha ishara ya kukataa kuigusa keki ya Shay Rose Banji huku akicheka.

Na Father Kidevu

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wa CHADEMA ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.

Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.

Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.

Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa, Wasanii muziki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.

Vipi Sugu alikuwepo?

Kwa keki hiyo haifai hata bure, au hata ukimpa mbwa wako nyumbani anaweza kupata "rabies", na akakuuma mmiliki wake!
Ningealikwa hapo ningepata konyagi zangu mbili tatu, keki sigusi!
 
Vipi Sugu alikuwepo?

Kwa keki hiyo haifai hata bure, au hata ukimpa mbwa wako nyumbani anaweza kupata "rabies", na akakuumwa mmiliki wake!
Ningealikwa hapo ningepata konyagi zangu mbili tatu, keki sigusi!

Hahahahaha! SUGU ANAKULA ILE KEKI NYINGINE ISIYOOZA, hiyo lazima aikatae teh!
 
Hii rangi ya ccm hata siku nikiwa mfu mkanifunika na rangi hiyo lazima niamke nitimue mbio.
 
Vipi Sugu alikuwepo?

Kwa keki hiyo haifai hata bure, au hata ukimpa mbwa wako nyumbani anaweza kupata "rabies", na akakuuma mmiliki wake!
Ningealikwa hapo ningepata konyagi zangu mbili tatu, keki sigusi!
hadi willi alikuwepo
s8.jpg
 
jamani hivi kweli kwa kuangalia hii picture kwa umakini kama unajua kusoma picha- kuna mtu hapo kwa mtazamo tu kuwa huyo ni majivuno na mchumia tumbo na hastahili hata kwa uongozi wa familia,maybe anastahili kuitwa baba tu ila sio baba wa familia. tazama picha kwa umakini then utagundua tu!!!!
 
Lemutuz@kugida ugiimbi.
"mewahi ona ng'ombe dume narembua" by mr. ebbo RIP
 
Jamani huyu baharia ni bar'aa-b'ara huyu? au ndio mapoowz ya New York?
 
Kukataa keki kwa kuwa ina rangi ya CCM ni ushamba na ujinga, hapo ndipo inapoonesha tuna mibunge mijinga kutoka upinzani, waikatae na bendera ya Tanzania ime sheheni rangi za CCM.

Waweke yenye rangi ya chadema waone watu waliostaarabika, wataila na kama nzuri wataisifia.
 
Nina wasiwasi na akili za Shyrose Banji kama ni mpuuzi wa viwango hivi, yaani analeta ushabiki wa vyama mpaka kwenye keki? ndio maana sikufanya makosa nyumbani kwangu minguo yote ya kijani ndio matambala ya deki na ndio ya kukung'utia michanga mlangoni na matope.
 
Back
Top Bottom