KCMC ikaangoni

KCMC ikaangoni

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,816
Reaction score
4,455
Hospitali ya KCMC imeshitakiwa na mama moja ambaye anadaiwa kutolewa kizazi pasipo ridhaa yake halisi,mwanamke huyo anadai alifanyiwa upasuaji na kuondolewa kizazi kutokana na tatizo lililokuwa linamsumbua(halijawekwa wazi).

Kwa mujibu wa vyanzo vyangu mwanamke huyu anawakilishwa na wakili PETER KIBATALA,ambapo kesi hiyo inasikilizwa chini ya KIIMA.,na upande wa mshitakiwa ambaye ni KCMC bado hawajawekwa wazi.

Mwanamke huyo nadai hospitali ya KCMC kumlipa fidia ya TSH.800M.

Wakati kesi ikisomwa ,upande wa mshitakiwa waliweka ombi kwamba kesi hiyo isijadiriwe katia lugha ya kiswahili bali kingereza,lakini jaji KIIMA alitupilia mbali ombi hilo.
 
Attachments

  • kcmc.jpg
    kcmc.jpg
    31.2 KB · Views: 1
Inawezekana katika kutolewa kizazi kumemsaidia kumaliza tatizo alilokuwa nalo. Changamoto inatokea kwa mgonjwa pale ambapo ametolewa kizazi na hana mtoto, hii inampelekea kuhisi labda hospitali haijamtendea haki, kumbe walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake.

Na hii utokea pale mgonjwa anapokuwa na uvimbe kwenye uzazi, wakati mwingine umpelekea kuvuja damu mara kwa mara, na inawezekana katika uchunguzi ikaonekana tiba sahihi ni kutoa kizazi ili uvimbe usijirudie.

Ile kukubali au kutokukubali kwa mgonjwa kutolewa, inategemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.​
 
Hapo consent form ni moja ya nyaraka itakayowasilishwa mahakamani.

Hapo naona kuna mazingira mawili.

1. Doctor waliingia kwenye operation wakiwa hawana wazo la kutoa kizazi.
Katikati ya operation wakagundua kizazi kimeshaharibika. Wakafanya ile Tumsaidie tuu huyu mama , tuondoke na kizazi .asisumbuke kurudi kwenye operation nyingine tena. Tutamuelezea baadae.

Au
2. Katika kufanya operation mambo yameharibika , ili mama atoke salama theatre inabidi watoe kizazi.
 
hakuna tumsaide tu,kabla hawajaingia theatre,huwa wanakuwa na majibu ya vipimo vyote na linakaa jopo la madaktari kujadiri majibu hayo na kuteua nani na nani watasimamia zoezi hilo,unless otherwise ni dharura ndio huwa inafanywa bila kikao.
 
Inawezekana lengo lilikuwa ni kusafisha kizazi, baada ya upasuaji ikaonekana labda njia sahihi ni kuking'oa, mbaya zaidi mgonjwa alishadungwa drip la usingizi.

Kwa ujumla hospitali itashinda; Ila, kama watetezi watang'ang'ania mambo ya checklist, kabla ya kufanya nini nini kilitakiwa kufanyika?, hapo hospitali inaweza kuingia hatiani.

Ndio maana wanashauri, katika taaluma yoyote ile fuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwenye taaluma hiyo; hakuna aja ya kuoneana huruma.

Inawezekana, mgonjwa alionewa huruma; matokeo yake, shukrani ya punda ni mateke.​
 
Inawezekana katika kutolewa kizazi kumemsaidia kumaliza tatizo alilokuwa nalo. Changamoto inatokea kwa mgonjwa pale ambapo ametolewa kizazi na hana mtoto, hii inampelekea kuhisi labda hospitali haijamtendea haki, kumbe walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake.

Na hii utokea pale mgonjwa anapokuwa na uvimbe kwenye uzazi, wakati mwingine umpelekea kuvuja damu mara kwa mara, na inawezekana katika uchunguzi ikaonekana tiba sahihi ni kutoa kizazi ili uvimbe usijirudie.

Ile kukubali au kutokukubali kwa mgonjwa kutolewa, inategemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.​

Kawaida kama mgonjwa hana fahamu mume, mzazi au ndugu yake wakaribu anatakiwa asaini kwa niaba yake.
 
Hospitali ya KCMC imeshitakiwa na mama moja ambaye anadaiwa kutolewa kizazi pasipo ridhaa yake halisi,mwanamke huyo anadai alifanyiwa upasuaji na kuondolewa kizazi kutokana na tatizo lililokuwa linamsumbua(halijawekwa wazi).

Kwa mujibu wa vyanzo vyangu mwanamke huyu anawakilishwa na wakili PETER KIBATALA,ambapo kesi hiyo inasikilizwa chini ya KIIMA.,na upande wa mshitakiwa ambaye ni KCMC bado hawajawekwa wazi.

Mwanamke huyo nadai hospitali ya KCMC kumlipa fidia ya TSH.800M.

Wakati kesi ikisomwa ,upande wa mshitakiwa waliweka ombi kwamba kesi hiyo isijadiriwe katia lugha ya kiswahili bali kingereza,lakini jaji KIIMA alitupilia mbali ombi hilo.
Kama kibatala yupo hiyo pesa watamlipa.
Alitakiwa aombe fidia ya bilioni tano.
 
Inawezekana katika kutolewa kizazi kumemsaidia kumaliza tatizo alilokuwa nalo. Changamoto inatokea kwa mgonjwa pale ambapo ametolewa kizazi na hana mtoto, hii inampelekea kuhisi labda hospitali haijamtendea haki, kumbe walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake.

Na hii utokea pale mgonjwa anapokuwa na uvimbe kwenye uzazi, wakati mwingine umpelekea kuvuja damu mara kwa mara, na inawezekana katika uchunguzi ikaonekana tiba sahihi ni kutoa kizazi ili uvimbe usijirudie.

Ile kukubali au kutokukubali kwa mgonjwa kutolewa, inategemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.​
Ridhaa ni lazima, kama mgonjwa hajitambui, basi mume/wazazi/mlezi lazima waridhie.
 
hakuna tumsaide tu,kabla hawajaingia theatre,huwa wanakuwa na majibu ya vipimo vyote na linakaa jopo la madaktari kujadiri majibu hayo na kuteua nani na nani watasimamia zoezi hilo,unless otherwise ni dharura ndio huwa inafanywa bila kikao.
Huwa kuna Intraoperative diagnosis.! Inawezekana kilichokutwa baada ya upasuaji ndo imepelekea atolewe kizazi.
 
Back
Top Bottom