Hospitali ya KCMC imeshitakiwa na mama moja ambaye anadaiwa kutolewa kizazi pasipo ridhaa yake halisi,mwanamke huyo anadai alifanyiwa upasuaji na kuondolewa kizazi kutokana na tatizo lililokuwa linamsumbua(halijawekwa wazi).
Kwa mujibu wa vyanzo vyangu mwanamke huyu anawakilishwa na wakili PETER KIBATALA,ambapo kesi hiyo inasikilizwa chini ya KIIMA.,na upande wa mshitakiwa ambaye ni KCMC bado hawajawekwa wazi.
Mwanamke huyo nadai hospitali ya KCMC kumlipa fidia ya TSH.800M.
Wakati kesi ikisomwa ,upande wa mshitakiwa waliweka ombi kwamba kesi hiyo isijadiriwe katia lugha ya kiswahili bali kingereza,lakini jaji KIIMA alitupilia mbali ombi hilo.