KCMC ikaangoni

KCMC ikaangoni

Hii ndio tunaita Ethical dillema. Unamtoa ndio uokoe uhai wake ila hajaridhia na hakuna ushahidi kuwa ingemletea hatari kwenye uhai wake. Ni ngumu kweli kweli.
Hii ndio tofauti ya fani ya upasuaji na fani za kungojea miongozo. Unajua kabisa, bila upasuaji hapa, huyu mgonjwa haponi, lakini fani za taralila wanaanza kupinga pinga.​
 
Hii ndio tofauti ya fani ya upasuaji na fani za kungojea miongozo. Unajua kabisa, bila upasuaji hapa, huyu mgonjwa haponi, lakini fani za taralila wanaanza kupinga pinga.​

Nadhani hao mabingwa wa upasuaji wana miongozo yao kwamba ikitokea umekutana na emergency kwenye procedure ambayo ni life threatening inawapa ruhusa ya kuondoa kumuokoa mgonjwa.
 
Hospitali ya KCMC imeshitakiwa na mama moja ambaye anadaiwa kutolewa kizazi pasipo ridhaa yake halisi,mwanamke huyo anadai alifanyiwa upasuaji na kuondolewa kizazi kutokana na tatizo lililokuwa linamsumbua(halijawekwa wazi).

Kwa mujibu wa vyanzo vyangu mwanamke huyu anawakilishwa na wakili PETER KIBATALA,ambapo kesi hiyo inasikilizwa chini ya KIIMA.,na upande wa mshitakiwa ambaye ni KCMC bado hawajawekwa wazi.

Mwanamke huyo nadai hospitali ya KCMC kumlipa fidia ya TSH.800M.

Wakati kesi ikisomwa ,upande wa mshitakiwa waliweka ombi kwamba kesi hiyo isijadiriwe katia lugha ya kiswahili bali kingereza,lakini jaji KIIMA alitupilia mbali ombi hilo.
Wamrudishie kizazi chake au wamekitupa?!
 
Inawezekana katika kutolewa kizazi kumemsaidia kumaliza tatizo alilokuwa nalo. Changamoto inatokea kwa mgonjwa pale ambapo ametolewa kizazi na hana mtoto, hii inampelekea kuhisi labda hospitali haijamtendea haki, kumbe walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake.

Na hii utokea pale mgonjwa anapokuwa na uvimbe kwenye uzazi, wakati mwingine umpelekea kuvuja damu mara kwa mara, na inawezekana katika uchunguzi ikaonekana tiba sahihi ni kutoa kizazi ili uvimbe usijirudie.

Ile kukubali au kutokukubali kwa mgonjwa kutolewa, inategemea na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.​
Kuna kitu nimejifunza hususani Kwa wazungu hasa kwenye mahakama zao usimfanyie mtu wema bila ridhaa yake, ni bora umwache afe au lolote limkute sababu akipata tu kupona anakushitaki na unamlipa fidia.
 
Binadamu ni kigeugeu
Just imagine kuna mtu alimsaidia mdada kwenye ajali kabla ya gari kuwaka moto yule dada alivyopona alimshtaki kuwa alikuwa na poor handling imemsababishia kupata tatizo la mguu na anataka kulipwa dollar laki nane! Wakati kama jamaa asingemuokoa yule dada alikuwa anakufa kwenye gari.
 
Watu wengine katika dunia, wanatumika kama case study, kwa wengine kujifunza na kutokurudia hayo makosa.
 
Back
Top Bottom