Ebu waite waje tusikie watasemaje..!
Hi...... wana jukwaa.
Kuna jambo limekuwa likiwapa wakati mgumu baadhi ya vijana kutokana na aina ya kazi wanazo fanya hii ni kwa sababu ya dhana fulani inayokuwa imejengeka katika makundi ya vijana kwamba kuna baadhi ya kazi wanaamini kwamba zina wavutia akina dada na kunanyingine haziwafutii.
Kuna vijana wengine wanashindwa hata kuwaonesha wapenzi wao maeneo yao wanayo fanyia kazi kwa kuamini kwamba hayana mvuto, kuna wengine hata hudiliki hata kujificha inapotokea bahati akapita binti mahara pa kazi yake.
Na sio tu kwa walio katika mahusiano ndo hili jambo linawakumba kuna wengine hawapendi wajulikane kazi wanazo fanya hata wanapo ulizwa na vijana wenzao, wanashindwa kuwa wawazi juu ya hilo.
Hili limesha kuwa kama tatizo ndio sababu hata utakuta baadhi ya vijana wana bagua kazi za kufanya kwa ile ile dhana ya kuamini kuna kazi nzuri na mbaya, Lakini inakuwa tofauti kidogo kwa wale wenye kazi wanazo ziita nzuri wanakuwa haraka sana kujibu yale maswali ya unafanya wapi kazi au unafanya kazi gani.
Leo naomba tuelezane kama ni kweli kuna kazi nzuri na mbaya na kama kuna kazi zinazo wavutia akina dada?
Na pia sio mbaya kama tuzijua kazi hizo ni zipi?
Na kama hazipo nini kifanyike ili kuondoa hii dhana inayo endelea kuwa umiza vijana wanaoishia kukaa vijiweni wakiamini kuna kazi zinazo leta heshima ndani ya jamii.
Na tuwasaidie mawazo wale wanao jificha wawapo makazi na wale mabingwa wa kuwazuga akina dada.
Mwanaume hela bila kujali chanzo. Dura hata mbuzi anayo. Nawashauri pigeni kazi vijana pateni jela warembo wanakuja tu wenyewe.
Hata km ww kazi yako ni kuzibua vyoo still ur handsome baada ya mshiko kuingia
kazi ni kazi ilimradi tu mkono uende kinywani na kazi ya maana ni ile ambayo haitaleta uhuni ndani yake
yaani nasemea kazi halali ndo ya kufanya yoyote ile
halafu wadada hatuko kama mnavyodhani eti sisi tunaangalia pochi au kazi za wanaume sisi siku hizi
tuaijituma kivyetu na tunafanya kila linalowezekana ili kujipatia kipato chetu hatuko kama mago:A S 13: wa zamani
Mbona maswali yenu ya kwanza huwa mnauliza kazi.
Bi dada una ukwepa tu ukweli lakini ni wazi mnaangalia sana kazi zenye taiz.
Mie napenda mabaunsa!!!!!!
mhm! kwangu siko hivyo kabis a ninachoangalia upendo tu kati yetu hta hakuna job
Kuajiriwa na kujiajiri zote ni kazi ..
Kuhusu nyie wanawake mnaotaka wapenzi wenu wawaambie kazi zao si kila mtu atakuonyesha kazi yake anayoifanya..
Mfano kazi za watu wa intelligence agencies mara nyingi ni za siri na sio za kutangaza...wengine hata wazazi wao hawajui wanafanya kazi gani ije kuwa wewe kisorokokwinyo aliyekutana na wewe mtaani..? Sidha
teh teh,acha kutuzuga hapa..! Upendo hata km mnalala na njaa..!?mhm! kwangu siko hivyo kabis a ninachoangalia upendo tu kati yetu hta hakuna job
hapo ndipo wanawake wanapopoteaga sana na ndoa zilizoingia kwa kipimo cha kazi ya mwanaume kuibukia migogoro ya kutosha..
Unakuta mdada kamzimikia mwanaume banker mshahara laki 7 net anaolewa akijua ameukata, anaingia ndani ya ndoa baadae anagundua amepotea anaanza kumtamani mume wa mwenzake anaepanga ma container bandarini hajui kuvaa tai kila siku ma ovaroli tu lakini kipato sasa mamilioni
dada zangu nawashauri kama mnapenda wanaume kwa kigezo cha pesa msiangalia mavazi na uzuri wa ofisi ya kidume, kuna watu wanatengeneza hela vibaya mno kwa kazi zisizoruhusu kupendeza..
Mnajua mume wa nancy sumari luca anafanya nini? Nenda kafanye homework yako jamaa nilimkuta kwenye container yard yake dicd amekula reflector, safety boot, jeans full kisela kama msela tu wa mjini yupo disorganised anasaidia kupanga macontainer na hapo anatengeneza hela vibaya mno..nikasema nancy ana akili sana wenzangu na mie mnaotungangania kina yahaya na tai zetu tunafurahije..
Kuna watu wa coz za ardhi pale sijui ma surveyor, artchr,contractr wanapiga hela vibaya mno lakini wapo lafu,
kuna wauza mitumba, wauza vifaa vya magari gerezani, wana hela vibaya mno but ukiwakuta kazini unafikiri waganga njaa tu nenda kaone maisha yao na familia zao utakimbia
Ukweli mtupu, teh ukiwa na doc inabidi uwe watch dogMi nipo hapo kwenye RED...Si haba ila umesahau Madaktari aisee hawa jamaa sijui wana nini na wanawake???? Uklisema mi ni dokta bhaaasssss habari imeisha
Ila hata wewe umepotea eeeh! hata kule kiringeni sikuoni bibie.