Kazi jamani..!!

Mkuu Fidel achana na mawazo ya kizamani.Siku hizi hakuna mtu ambae anaweza akapata kazi kwa sababu ya kutoa rushwa ya ngono.

Mkuu chunguza utabaini.
Waulize wadada watakwambia nafasi ya rushwa ya ngono makazini.
 
kazi ipo ila cv yake aiweke hadharani,hususani picha na kama ameolewa au la
 
Ardhi haijaisha ndugu yangu HUKU TANZANIA..Unashauri akalime?..Tusaidiane kimawazo vizuri juu ya hili, anaweza kuwa mkulima pia!
Asante

BelindaJacob
umeona majibu ya wenzetu walioko ng'ambo?
wala husishtuke kumbuka tu ile methali "MASIKINI AKIPATA ****** HULIA MBWATA". Kwa kifupi ni jibu la hovyo hovyo, linakera kwani haliendani na topic
 
kwani huko TANZANIA ardhi ya kilimo imekwisha?

Mkuu wewe si unabeba box huko rudi na wewe uache ukuli uje tusaidiane kulima tunapenda watu kama nyie muwe mnakumbuka kwanza nyumbani na kulijenga taifa sio mnajisahau huko kwenye kubeba box.
 
kazi ipo ila cv yake aiweke hadharani,hususani picha na kama ameolewa au la

Niwie radhi mkuu, sitaweza kuiweka CV yake hadharani. Kama una nia nzuri ya kumsaidia angalau kuwa shortlisted kwenye kazi, mimi nakutumia CV yake. Bado hajaingia chama cha ndoa!..
Asante!
 
Mtatutibulia hali ya hewa kwa masihala ktk mambo ya maana. Msaidieni mhusika kupata kazi,kama huna hint si ukae kimya?
 
BelindaJacob
umeona majibu ya wenzetu walioko ng'ambo?
wala husishtuke kumbuka tu ile methali "MASIKINI AKIPATA ****** HULIA MBWATA". Kwa kifupi ni jibu la hovyo hovyo, linakera kwani haliendani na topic

Ndugu Sipo
Nimeona mwenzangu, kuna wengine wameshakuwa watasha siku hizi kitabia mana rangi haibadiliki. Na aliye juu siku zote mngojee chini pia maisha ni kupanda na kushuka!Mwenye nia ya kusaidia hawezi kujibu vile bora hata angeniambia sehemu inatangazwa kazi ili nimwambie rafiki yangu aombe!
Asante!
 
Mkuu wewe si unabeba box huko rudi na wewe uache ukuli uje tusaidiane kulima tunapenda watu kama nyie muwe mnakumbuka kwanza nyumbani na kulijenga taifa sio mnajisahau huko kwenye kubeba box.

Ni vijimambo tu mkuu wangu!..shifti za mzigoni zinaumiza kweli na stress juu yake!..bongo unaishi simple life na unamshukuru Mola!..Na hata mkulima siyo mtu wa kumbeza,anaweza akakosa mambo kadhaa ya ziada kwenye maisha ila hatakosa chakula kuingia kinywani..
 
Hapa ndipo utakapo watamanisha mapedeshee wa humu ndani.
Yaani anaweza akala shavu muda si mrefu kwenye showroom za magari.

Sijasema jinsia yake lakini!..Shauri yenu,muingie kichwa kichwa tu!..
Enewei, ukisikia chochote kuhusu kazi ya uhasibu iwe shirika binafsi au serikalini nishtue. Yupo tayari kujaribu bahati zaidi na zaidi! Mungu hamtupi mja wake!
Kaitaba na Next Level sijui watatoa lini tena kazi za wahasibu ili wamshortlist?..Tunasoma matangazo mpaka kuchoka! kutafuta kazi nako ni kazi!
 
Belinda,
Huyo ndg yako yuko mkoa gani. Amepasi angalau zaidi ya average? Anachagua mshahara?Kama una mojawapo ya barua yake nitumie. Nijaribu kui fwd kwa watoa kazi. Hawa watoto wa IFM(labda excluding him/her)wanajiwekea status ambazo hawajatengeneza. Lakini la ziada kama alivyosema mchangiaji 1,kama huna experience mzazi aliyekusomesha miaka yote hiyo lazima awe tayari kukulipia angalau nauli ufanye practicals/fields hata kama ni bila senti 1 ujaze CV yako na humo x 2 unaweza kuwa unapata na access ya facilities na contacts.Kazi za magazeti nyingi wanakuwa wameishakalia meza ndio wanatangaza,uliza aliyepasi -utaambiwa hata kwenye inteview hakuwepo alikuwa kazini.
Kt.
 
Kaitaba!

Ndugu yangu huyu yupo mkoa wa Dar na pass yake ilikuwa zaidi ya average. Mshahara hachagui,ni kunegotiate (itategemea na utakavyopendekeza mkuu).
Experience anayo ndogo sana ambao alipata wakati wa kufanya field katika organization fulani.Hiyo field ni part ya kozi aliyosomea, ni ya vitendo. Ili kupata experience zaidi inabidi apate kazi kuendeleza career yake.
Kweli magazeti tumesoma sana na kujaribu bahati kuomba kazi ila hajafanikiwa..
 
BelindaJacob
umeona majibu ya wenzetu walioko ng'ambo?
wala husishtuke kumbuka tu ile methali "MASIKINI AKIPATA ****** HULIA MBWATA". Kwa kifupi ni jibu la hovyo hovyo, linakera kwani haliendani na topic

Mkuu Sipo,

wengi wanaelewa visivyo huo usemi....hata mimi nilikuwa nasema hivyo hivyo kama ulivyoandika....ukiangalia usemi ulioandika hauleti maana kabisa.......usemi sahihi ni kama ifuatavyo

MASIKINI AKIPATA ****, (i.e. from neno takwa/hitaji...) HULIAMBATA (hili ni neno moja....i.e. haliachii....yaani yeye hilo ****/takwa/hitaji lake haliachii)....

kwa hiyo umetumia huo usemi visivyo...............

tuendelee kumtafutia kazi ndg yetu kama alivyotuomba Belinda

Invisible
naomba rekebisha hiyo ***** zako maana maneno mengine ni lugha tu.........
 
Aisee mbona hajakaa sana kwani mimi huu ni mwaka wa nne napeta uswahilini mpaka elimu yangu yote imeyeyuka.......
 
Mtatutibulia hali ya hewa kwa masihala ktk mambo ya maana. Msaidieni mhusika kupata kazi,kama huna hint si ukae kimya?

Mtabiri
Wahenga wanasema kitanda usichokilalia hujui kunguni wake!..kwahiyo mtu kama huyo 'SOA' ni kumuacha tu, mdhungu huyo ati wa landani..
Asante na tuhabarishane ukisikia kazi ya uhasibu..
 
Back
Top Bottom