Kazi jamani..!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi jamani..!!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by BelindaJacob, Jul 15, 2009.

 1. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Wakuu!

  Nina rafiki yangu amemaliza IFM mwaka jana na alisoma Advanced Diploma in Accountancy. Kwakweli amejaribu kuomba kazi mbalimbali zilizotangazwa bila mafanikio.
  Siyo kuwa anajiamini bila ya kuwa na Godfather ila ni kwamba hana kabisa kwa hiyo amekuwa anajaribu kuona kama atafanikiwa.
  Mwaka umefika sasa hii July tangia amalize chuo bila dalili ya kazi.
  Ninaomba msaada wenu na kama kuna maswali mengine muhimu ya kujibu nitajibu.Tusaidiane

  Asanteni!!!
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Habari za kuadimika mama.
  Naona mzee anasema mlikuwa vekesheni wote sijui kweli?
  Haya mwambie huyo rafiki yako ajiunge hapa JF atapata tu kazi kazi zipo nyingi tu mwambie tu ajiunge hapa.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Akina Fidel180 wasianze kuuliza kama huyo mtafuta kazi ni mwanaume au mwanamke, maana ndo zao hawa!
  Jamani, anybody with news of vacancy, plz help that guy!
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180

  Nzuri tu mkuu, vekesheni imeisha tunaendeleza shifti kama kawaida.
  Huyu rafiki yangu hayupo JF ila karibia kazi nyingi nionazo kupitia hapa za uhasibu namtumia na ni mvumilivu maana anaomba kweli bila mafanikio. Kweli anahitaji kazi!..
   
 5. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Wakuu kama sikosei ilikuwa jana nilipoomba kuwa kwa wale Ma HR watwambie nini wanachotaka kwenye hizo barua za kuomba kazi kweli hii imekuwa kero unajipinda unatuma barua halafu hata jibu hupati au ndo zile tabia za masecretary kuchana barua za watu ili za ndugu zao ndo ziende kuwa shortlisted.

  Kweli inakera sana tena sanaaaaaaa
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  We acha tu,nitawaambia mtafuta kazi ni mtu kama sisi!..Jinsia yake haina umuhimu kwenye maombi ya kazi maana ni ya uhasibu.
  Asante mkuu, tushtuane kama unaweza kuwa Godfather maana kazi za siku hizi zinahitaji kujuana japokuwa kuna wengine wanapata bila hivi..
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Siku hizi naona mambo yamebadilika sana, Godfather amekuwa ndo nguzo ya kukusaidia kupata kazi haraka. Japokuwa kuna wengine wanapata bila ya kutumia Godfather, huyu rafiki yangu ameshindwa na anasononeka sana kuwa hana hata huyo ndugu ya kumsaidia kumuunganishia..
  Ma HR nashindwa kuelewa lakini ndo Tz yetu hiyo, lazima wana watu wao wengineo hivyo CV zinapokeleka kama kawaida ila husikii kitu wala nini..
  Hujui tu huzuni aliyonayo maana ni mchakarikaji akisikia kazi tu inahusiana na kisomo chake na vigezo lakini haambulii kitu..
  Inawezekana hana kismati!..who knows??!!
   
 8. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nafasi za ya kazi

  anahitajika haraka msichana mwenye stashahada ya business administration na uzoefu wa masuala ya accounts usiopungua mwaka mmoja. Anapendekezwa awe msichana umri kati ya miaka 20 - 30. Awe anajua kutumia computer na hususan programu ya excel..

  Kwa maelezo zaidi piga simu 0713 839363, 0784 888982
  global publishers ltd
  dar es salaam
  tanzania
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi ni wa kike au wa kiume maana kazi siku hizi zinatolewa kijinsia namaanisha ladies first kama ni dume ataendelea kusubili.
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mkuu JosM

  Asante sana, nimemtumia via email aombe na hii kazi!
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mkuu Fidel80

  Kazi siku hizi zinatolewa kwa kujuana siyo jinsia. yaani umenichekesha kweli!.
  Ni rafiki yangu wa kitanzania!...Please tusaidiane!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwambie awe makini Shigongo mwanaume wa shoka.
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Akili yake yote inawaza kupata kazi ili asapoti familia yao. I wish ungejua hali aliyonayo kimaisha..ana nia na kazi tu mengine siwezi kumsemea ila kazi kwasasa ndiyo muhimu kwake!..
   
 14. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Wanabadilikaka hao.jana nilicheka kuwa Adam Mchomvu siku hizi kaisusa hata familia yake baada ya maisha kumnyokea.Kwa hiyo na huyo usitupe 100% kuwa kwa sasa yupo commited na kazi.kwanza yatakuwa maamuzi yake sisi hayatuhusu kikubwa apate kazi kama itakuwa ya kwenda maisha club au kusaidia familia yake that is.
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kikubwa apate kazi hayo mengine ni maisha ya mtu binafsi na nisiyasemee sana!..
  Asante!
   
 16. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Fidel achana na mawazo ya kizamani.Siku hizi hakuna mtu ambae anaweza akapata kazi kwa sababu ya kutoa rushwa ya ngono.ikitokea hivyo nimtu kapenda mwenyewe.Sasa huo ushoka wa Shingongo ndio utamsaidia kitu gani? mtu anahitaji kazi nyie mnaanza kumpa vitisho vya ajabu ajabu.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa msoto huo alio kuwa nao na wasi wasi hata rushwa ya ngono anaweza toa wallah maana kasota sana benchi. Duh kuhusu familia wengi mambo yakinyooka iwa wanakata hata mguu.
   
 18. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inategemea na msimamo wa mtu mkuu,sio kila mtu akipata msoto kidogo tu anajiachia.kuna wanawake ngangari mkuu usipime kabisa.
   
 19. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Ni kweli msoto anao sana!..Siwezi kumsemea mengi,kubadilika kwa mtu au la ni mambo yake japokuwa wengi wanakuwa kama ulivyosema..
  Hebu mtafutie kazi na uwe Godfather wake kwenye suala hili la ajira!.
  Asante
   
 20. b

  bnhai JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,206
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Inawezekana na credit crunch pia imehit soko letu lakini hatuna takwimu ndio maana watu kukosa kazi siku hizi imekuwa kitu cha kawaida. Lakini pia bongo undugunisation saana yaani ni kero ishu si utendaji!!!
   
Loading...