Kauli za viongozi wa Tanzania zenye utata!

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Nimetafakari, nikaona nipate pia mawazo wanafikra weledi juu ya baadhi ya kauli zenye utata za viongozi kwa wananchi

Je, huu ni uungwana kweli?

Kauli tata za vingozi wa Tanzania


  1. Mtakula nyasi lakini ndege ya Rais lazima inunuliwe (MRAMBA)
  2. Ukitaka kula inabidi ukubali na wewe kuliwa (J Kikwete)
  3. Foleni Dar ni ishara ya maisha bora (J Kikwete)
  4. Hata mimi sielewi kwa nini Tanzania ni maskini! (J Kikwete)
  5. Ningekuwa mvua ningenyeshea mabwawa (J Kikwete)
  6. Wafanyakazi hata wakigoma miaka 100 ila mshahara kima cha chini 350,000 haiwezkani (J Kikwete)
  7. Wanafunzi kupata mimba ni viherehere vyao (J Kikwete)
  8. Acheni wivu wa kike (MSEKWA)
  9. Asiyeweza nauli mpya kwenda kigamboni apige mbizi (MAGUFULI)
  10. Baada ya kutumia helikopta ya jeshi kwenda kwetu urambo mlitaka nipande punda(KAPUYA)
  11. Wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia makalio(Dr Didas Ma------)
  12. Mnaniuliza mvua kwani mimi waziri wa mvua?(WASIRA)
  13. Ngeleja kila siku ananinunulia chai wakati nina uwezo (ANNE KILANGO)
  14. Posho za wabunge lazima zipande kwa sababu maisha ya Dodoma yapo juu (Spika Makinda)
  15. Wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na janga la njaa nawashauri wakulima wahifadhi hata pumba maana zinaweza kusaidia (John Malecela)
  16. Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe - Cleopa Msuya
  17. Mheshimiwa Lema, ninakuagiza ifikapo Jumatatu asubuhi uwasilishe Bungeni ushahidi kwamba mheshimiwa waziri mkuu asema uongo bungeni (Anna Makinda)
  18. Wapinzani wanapenda mambo ya ovyoovyo wanafiki hawa wataendelea kuwa wapinzani tu (Samwel Sita)
  19. Graduates msio na kazi fugeni kuku biashara hiyo inalipa sana (Mwantumu MAHIZA)
  20. Kinachomsumbua Slaa (Dr) ni wivu, wivu kuona ndege inapaa, ndege ya uchumi wa TZ inapaa"- (Edward Lowasa)
  21. Tanzania ni muungano wa visiwa viwili, Tanganyika na Zimbabwe (Philip Mulugo)
  22. Siongei na mbwa mi naongea na mwenye mbwa (Juma Ngamia)
  23. Hakuna Rais atakayetoka Kaskazini (Ridhiwan Kikwete)
  24. Waliotoka Bara na kuja Dar es Salaam wafute kwanza tongotongo (Ukiwaona Ramadhan Mwinshehe Ditopile Mzuzuri)
  25. Mbowe amekuja hapa kajamba-jamba halafu kaondoka (Seif Khatib)
  26. (Billioni 1.2) - Hivyo ni vijisenti tu (Andrew Chenge)
 
Nimetafakari, nikaona nipate pia mawazo wanafikra weledi juu ya baadhi ya kauli za viongozi kwa wananchi, pigeni mbuzi ndo latest katika hizo, je huu ni uungwana kweli?

Fanya editing ni pigeni mbizi siyo pigeni mbuzi.
Pia ongezea na wivu wa kike.
 
Nimetafakari, nikaona nipate pia mawazo wanafikra weledi juu ya baadhi ya kauli za viongozi kwa wananchi, pigeni mbuzi ndo latest katika hizo, je huu ni uungwana kweli?

...mkuu hizo ndo kauli za watawala,kauli kama hizo hazipatikani ktk nchi zilizo na viongozi...
 
Unajua mtu akitembelea STK anawekewa full tank full kiyoyozi hawezi kujua matatizo ya watu wa kigamboni kwani hata wakisema nauli sh 10,000 wao haziwagusi kwani hawalipi na mara nyingi hata foleni huwa hawakai kwa kweli inatia uchungu sana na hizi kauli za kejeli eti pigeni mbizi.
 
Unajua mtu akitembelea STK anawekewa full tank full kiyoyozi hawezi kujua matatizo ya watu wa kigamboni kwani hata wakisema nauli sh 10,000 wao haziwagusi kwani hawalipi na mara nyingi hata foleni huwa hawakai kwa kweli inatia uchungu sana na hizi kauli za kejeli eti pigeni mbizi.
Teh teh teh!

Hiyo ya "Pigeni mbizi" nani alikuja nayo?
 
viherehere vyao.....mbayuwayu....hata wafanyakazi wasiponipa kura.....
huo mdomo huo...!

O44P4P+6fIqy9Fg64AAAAASUVORK5CYII=


:focus:

Nilishasema huko nyuma kuwa huyu jamaa ni mbwabwaji. na wananchi watamfundisha 'sheria'
 
Hizi ni kauli za kawaida kwa watawala hasa wanaotawaliwa wanapokuwa ni wajinga na wasiokuwa na uwezo wa kuchukua hatua. Tutaendelea kuzikia kauli za kudhalilishwa hadi tutakapo amka usingizini! Tunadanganywa na kudhalilishwa kwa kuwa tumeshaharibiwa na shule za kata. Ndio maana tunaambiwa eti kuna "utawala bora!" Hakuna nchi iliyoendelea duniani ikiwa inatawaliwa. Wakati tunahitaji "viongozi bora", tuliowapa dhamana wanasema wanatutawala "kwa ubora" na sisi tunafurahia na kuwapongeza. Ndio maana wanatudharau na kutuona wajinga mwisho wanaropoka wanavyotaka maana wanajua hatuna jeuri ya kuwachukulia hatua.

Vyovyote vile, tutatukanwa na kudhalilishwa hadi tutakapotoka usingizini na kuchukua hatua madhubuti ya kuchagua "viongozi" bora na sio "watawala" wanaolewa madaraka na kuishia kututawala kama wakoloni kwa majigambo eti ni "utawala bora!"
 
Nimetafakari, nikaona nipate pia mawazo wanafikra weledi juu ya baadhi ya kauli za viongozi kwa wananchi, pigeni mbuzi ndo latest katika hizo, je huu ni uungwana kweli?
Sisi wananchi tukiwa wadau wa maendeleo endelevu,tunapaswa kuongozwa na uzalendo kwa kiasi fulani.
Binafsi kwa hili sifurahishwi na kauli hizi za watawala wetu kwani ni kejeli na matusi kwetu sisi wapiga kura wao
Lakini pia tunapaswa kuwa na uzaalendo .ongezeko la shilingi 200 kwa kuvuka kigamboni ukizingatia gharama za uendeshaji ni kubwa,
Kuna vivuko kama hivyo kule mwanza katika ziwa victoria na wao wanalipa bei bei zake ni zaidi ya hizo,tena kwa muda mrefu tu.na hatujawasikia kuandamana. je? kwa nini magogoni waq imekuwa issue au sababu ya kuwa karibu na Bagamoyo.
Ebu tujiulize watanzania ni kiasi gani tunatumia kwa michango ya sherehe kama Birthday send off,wedding,get together parties,na hivi karibuni Graduations.
Na cha ajabu ukiwaalika watanzania walio wengi kuchangia miradi ya maendeleo mfano madawati ya shule nk.mahudhurio yanakuwa kiduchu na hata hao wahudhuriaji wengi wanakuwa na malengo yao binafsi ikiwa pamoja na kutaka kupigwa picha wakati wakitoa for future benefits.
 
Nimetafakari, nikaona nipate pia mawazo wanafikra weledi juu ya baadhi ya kauli za viongozi kwa wananchi, pigeni mbuzi ndo latest katika hizo, je huu ni uungwana kweli?

Kauli kama hizo husababishwa na ulevi wa madaraka wa utawala.
 
Jamani jamani tembeeeeeeni muone,msilalamike tuuuuuuuuuuuuuu,sisi wabongo vitu karibu vyote tunapata bureeeee yaaani bwelele na hii ndio imetufikisha hapa tulipoooo

wataniunga mkono wale wote waliosoma nje ya Tanzania

jamani hakuna vitu vya bure ktk hii Dunia,wenzetu huku wanalipia hadi maji ya kuoga,yaani wanafunzi wa chuo kikuu analipia maji ya kuoga,maji ya kunywa,internet na kila kitu kinachomzunguka

ktk daladala zao utamwona mzee na kadi yake anagusisha tkt kifaa kinachokata pesa auto,yaani kila kitu hapa ni pesa,

ukienda hospital ndio utacheka kwa sisi tuliozoea buree unaweza kuanza kufoka
akija Dk kukuona tu hiyo ni pesa,akikupima joto tu hiyo pesa imekwenda,wewe utakae lala na mgonjwa utalipa pesa ya chumba na malazi,

lakini sisi bongo lawama,kelele,maneno,kulialia kwa sana tu

na hii ndio inasababisha tunashindwa kukusanya mapato mengi,kwani vitu vinge vipo free

wenzetu wamebana kila kona
ukienda kata tiketi ya kwenda mji furani,watakata nauri ya gari,kodi ya kituo,na mzani mahari ambapo gari zitapita,je bongo yapo hayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa?

tuna lalama sana jamani,lipeni nauri hamtaki pigeni mbizi
 
Ndugu mchangia mada, huwezi kuilinganisha ,Tanzania na nchi zilizo endelea kiuchumi, na ukifanya ivyo utakuwa unakosea sana maana, unapoongeza bei na kodi mbalimbali lazima uangalie kama Yule mwananchi wachini kabisa kama anaweza, ku afford izo garama..kwamfano nchi kama marekani kima cha chini cha mshahara ni 2000 Ndo maana wanatoza kodi mbalimbali, je Tz yetu kima cha chini cha mshahara ni ngapi? Na wenye hajira niwangapi? Ndugu umetembea ndio ila usijilinganishe na watu walioko Tanzania, hajira hakuna na ata iyo miambili yakuvuka pale ni nyingi nakuambia..JARIBU kufanya research utaona ilo.
 
Ndugu mchangia mada, huwezi kuilinganisha ,Tanzania na nchi zilizo endelea kiuchumi, na ukifanya ivyo utakuwa unakosea sana maana, unapoongeza bei na kodi mbalimbali lazima uangalie kama Yule mwananchi wachini kabisa kama anaweza, ku afford izo garama..kwamfano nchi kama marekani kima cha chini cha mshahara ni 2000 Ndo maana wanatoza kodi mbalimbali, je Tz yetu kima cha chini cha mshahara ni ngapi? Na wenye hajira niwangapi? Ndugu umetembea ndio ila usijilinganishe na watu walioko Tanzania, hajira hakuna na ata iyo miambili yakuvuka pale ni nyingi nakuambia..JARIBU kufanya research utaona ilo.

mshahara wa prof china tena prof huyo ni mkongwe kazini ni 7000Yuan= na kama USD 1200,hivi wakati huo ni mshara wa kijana mwenye degree ya kwanza pale SUA.
Mshahara wa mwalimu mwenye degree China atakae fundisha chuo kikuu ni 2000yuan sawa na 34500 za kibongo wakati mwalimu huyo wa degree ya kwanza akija tz atalipwa 7000yuan
na hii nchi ninayo itaja tulikuwa nayo sawa ktk level ya maendeleo hadi ilifikia kipindi tuliwasaidia ktk issue ya vyakula,lakini kwa sasa angalia wapo wapi? na Serikali inamsimamo wake utalipa kodi zote na kila kitu utakacho gusa kitahitaji pesa,wananchi wake wamelizoea hili limekuwa ni moja ya maisha yao hakuna ubishi nalo

Twenda ufilipino tena wao tuliwazidi sana ktk issue ya maendeleo miaka kumi iliyopita,ila baada ya kusimamia vyema ukusanyaji wa kodi na wananchi wake kutambuwa umuhimu wa kutoa kodi nchi yao hiyoooooooooooo inapaa,nimekupa mifano ya nchi tulizokuwa nazo sawa ktk mambo ya kiuchumi na wakasimamia ukusanyaji wakodi sasa haoo wapo mbari

lakini sisi,ni kelele,lawama,ubishi hatutaki kulipa kodi,hatutaki nauri zipande na bado tunahitaji huduma ziwe nzuri,huduma nzuri bila pesa mkuu haiwezekani,
 
Back
Top Bottom