Kauli za Makonda huko Kilimanjaro, Tanga na Arusha: Je, anaona waliopo wanapwaya?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Paul Makonda a.k.a Bashite wa Kolomije ameteuliwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya Uenezi wa CCM.
Bashite ikumbukwe alikuwa mkuu wa Wilaya na Baadaye Shujaa alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Bashite inasemekana amekuwa na kauli zisizo safi masikioni, be it kwa wadogo ama wakubwa zake huku akijivunia elimu ambayo wapinzani wanmtuhumu hajasoma hasa Gwajima ambaye ni mwana-ccm mwenziye.

Bashite kila alipopita amekuwa akikebehi wapinzani na kumsema Freeman Mbowe, ila alipofika kilimanjaro kwa watu wanao jielewa kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika aligeuza kauli na kusema anataka akalale kwenye kasri la Mbowe as if kwa wachagga kuna jumba kijijini ni anasa, walimshanga na hakupata mwitikio wowote .

Mbowe amejijengea nyumba ya kijijini ambapo hu ni lazma kwa kijana wa kiume kuwa na nyumba ya kijijini na wachagga wamemshanga maana makabila mengine wanaiba na kununua nyumba Dubai na South Afica lakini kwa wahaga wanafanya biashara na kuwekeza kwao walau sehemu ya kulala.

Baada ya Kilimanjaro sasa anaendelea na mikoa mingine ambayo anaweza kuendelea kutukana viongozi wa maeneo hayo.

Amekuwa na maigizo ya kuingia na punda, bodaboda, trekta na Moshi akaendesha mkokoteni-anafurahia watu walionyimwa ellimu kwa maksudi kuendesha mikokoteni.

anatamani angekuwa wenenzi kipindi cha jiwe/ Shujaa labda ili apoteze watu, ama abambikie kesi ,aama afute kabisa upinzani.
 
Back
Top Bottom