MTAZAMO: Makonda kuchukua jukumu la Majaliwa, Dotto Biteko, ndani kwafuka!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Paul Albert Bashite Makonda al maarufu kama Bashite ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya Dar es salaam na badae kuwa mkuu wa Mkoa awamu ile ya Mkono wa Chuma na kutumbuliwa na Awamu hiyo hiyo kabla ya kupigwa kikumbo kabisa na awamu iliyofuata sasa awau hiyo hiyo imemrudishwa kwenye siasa :

Baada ya kurudishwa, amenza kazi vizuri hasa kwa kufanya ziara lakini ametishia kazi za Waziri Mkuu Majaliwa , ametishia kazi ya Dotto Biteko na pia anayishia kazi ya Katibu Mkuu/CEO wa CCM bwana Chongolo.

Team CCM mabadiliko vs Sukuma Gang ambayo inarudi kwa namna nyingine nayo inaonekana kutaka uwaziri mkuu 2025 lakini pia inaonekana mwaka 2025 kuna wanaotaka umakamu wa Rais na Uwaziri Mkuu, kila mtu anapambana kivyake.

Makonda amekuwa akitumia gharama kubwa kwenye chama kuliko hata anazotumia mwenyekiti wake, anatumia walinzi binasi zaidi ya nane, anatumia walinzi wa chama 5 na walinzi wa serikali ambao ni kinyume na sheria japo haijafhamika vizuri.

Makonda amepigwa marufuku kukanyaga MarekaniTaarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ijumaa, Januari 31, 2020 marufuku hiyo pia inamhusisha mke wa Makonda Mary Felix Massenge. Bashite na mkewe ambapo kipindi cha SHUJAA alikuwa kila muda wanakwenda kula bata New York na Manhatan sasa wamepigwa BAN na sababu ya kuwa black listed ni tuhumu za KUKATISHA MAISHA YA WATU.

Ukandamizaji wa haki ambao Makonda anashutumiwa kuutenda ni pamoja na kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu.
"Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Michael Pompeo ametumia mtandao wake wa Twitter kutangaza marufuku hiyo.
Makonda amekuwa akiingilia majukumu yasiyo yake:

Wakubwa zake wanajiuliza:

1. Nani kampa Makonda mamlaka ya kusikiliza kero za wananchi na kumwagiza Waziri atekeleze?

2. Nani kampa mamlaka ya kusikiliza kesi zilizopo Mahakamani na kuonyesha ku-side na upande mmoja bila kusikiliza upande wa pili lakini pia hata kusikiliza upande wa pili mamlaka hayo ni yake au ya
mahakama?

3. Nani kampa mamlaka ya kufanya mikutano mida ya kazi wakati Magufuli alitumia mbinu hiyo kipindi
akiwadhibiti akina Mbowe na Lissu, aliwaambia muda wa kazi kusiwe na mikutano na wao walirelax
kufanya mikutano lakini kwa sasa Makonda muda wa kazi ndio.

4. Mpaka leo, kuvamia clouds TV, kashfa za viwanja na magari ya GSM ama hazijajibiwa ama wamefanya
watanzania ni wasahaulifu.

5. Inasemekana aliwahi kutukana mama mjamzito akimwambia apotee na tumbo tumbo lake, , kumkashifu Chongolo na wengine wengi, hajawahi kuomba radhi hadharani.

6. Kwa mwendo huu, wakati wa Mchakato wa mgombea urais 2024/5 huko NEC ataharibu vikao akiwa na SUKUMA GANG wanaorudi taratibu madarakani?
Pichani hapo Chini ni Makonda leo akiingia Mara, picha inajieleza,comments ziwe fupi fupi.

 
Ukiwa huna taarifa, usiudanganye umma. Makonda aliteuliwa na JPM kuwa Mkuu wa mkoa na huyo huyo ndiye aliyemtengua. Hakuna awamu ilifuata tofauti na hii ya sasa iliyomteua tena.
Ngoja kijana aimarishe chama na kukirejeshea uhai.
Kampeni za makonda hufanikiwa sana

1. Walimu wa Dar kutolipa nauli
2. Vita vya Shisha
3. Wanaume waliotelekeza watoto.

Kwa tathmini ya haki, mafanikio yalikuwa makubwa zaidi ya 75%.
Jembe lipo kazini, piga kazi.
Taifa linahitaji Makonda 10 tu ili kusonga mbele
 
Makonda kasababisha mwenyekiti wetu aahirishe kuendelea na mikutano yake aliokuwa amepanga kuifanya nchi nzima.

Mwenyekiti kaingia wasi wasi, aibu na fedheha, kuona mikutano yake ilidorora huku ya Makonda ikikusanya umati wa watanzania 🤣🤣🤣

Hivyo kaamua kukusanya chawa wake mitandaoni, ukiwemo mleta mada ili mje kuandika ujinga wa kumtoa Makonda kwenye reli ili kumpunguzia mwenyekiti aibu ya kuendelea na operation zake uchwara.

1699857405632.jpg
1699886527898.jpg
images (4).jpeg
Screenshot_20231112-071835.png
 
Ukiwa huna taarifa, usiudanganye umma. Makonda aliteuliwa na JPM kuwa Mkuu wa mkoa na huyo huyo ndiye aliyemtengua. Hakuna awamu ilifuata tofauti na hii ya sasa iliyomteua tena.
Ngoja kijana aimarishe chama na kukirejeshea uhai.
Kampeni za makonda hufanikiwa sana
1. Walimu wa Dar kutolipa nauli
2. Vita vya Shisha
3. Wanaume waliotelekeza watoto.
Kwa tathmini ya haki, mafanikio yalikuwa makubwa zaidi ya 75%.
Jembe lipo kazini, piga kazi.
Taifa linahitaji Makonda 10 tu ili kusonga mbele
1. Walimu kutolipa nauli ni jukumu la WAziri wa Uchukuzi , huyu waziri anasimamia LATRA na waziri wa Elimu anayesimamia walimu [Bashite aliingilia majukumu yasiyo yake-uongozi mbovu].

2. Shisha inapigwa vita na nani, wapi imepigwa vita wakati Shoisha ni halali na inalipiwa kodi TRA, so long as mvutaji amefika miaka 18, tatizo lako dogo upo huko Namanyere ukiskia shisha unahis ni kitu marufuku.

3. Wanaume wanaotelekeza watoto alikuwa anmlenga mwanasiasa fulani na si kampeni, bahati mbaya alimkosa maana alipandikiza jimama liseme limezaa na huyo mwanasiasa, chuki chuki chuki na uzandiki: Jukumu la mtu kutelekezwa ni Ustawi wa Jamii na Mahakama za WAtoto na si Mkuu wa Mkoa, yeye anaweza kusikiliza pande mbili na kupokea ushahidi na kutoa hukumu? Mamlaka hayo amepewa na sheria ipi?
Wacha upuuzi wewe!
 
Anayoyafanya makonda unaweza kudhani ni JPM mpya!anajipendekeza kupitiliza
INgelikuwa sahihi angefanya kwa ndani ya sheria.

Ukiskiliza mikutano yake, yaani inafaa kwa mikoa maskini:
Hivi mtu ana kesi mahakamani kama yule mzee wa Mwanza jana, ameshindwa kesi mpaka mahakama ya Rufaa anaenda na Makaratasi kwa makonda anataka Makonda aagize apewe ardhi, hizo akili akienda Mikoa inayojielewa hawezi fanya huo upuuzi.

Yani hukumu ya mahakama ya rufaa itenguliwe na katibu mwenezi wa Chama? Sijui wanatuonaje?
 
Ukiwa huna taarifa, usiudanganye umma. Makonda aliteuliwa na JPM kuwa Mkuu wa mkoa na huyo huyo ndiye aliyemtengua. Hakuna awamu ilifuata tofauti na hii ya sasa iliyomteua tena.
Ngoja kijana aimarishe chama na kukirejeshea uhai.
Kampeni za makonda hufanikiwa sana
1. Walimu wa Dar kutolipa nauli
2. Vita vya Shisha
3. Wanaume waliotelekeza watoto.
Kwa tathmini ya haki, mafanikio yalikuwa makubwa zaidi ya 75%.
Jembe lipo kazini, piga kazi.
Taifa linahitaji Makonda 10 tu ili kusonga mbele
Kumbe chama kilikufa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom