William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Nyie watu wengine sijuwi mukoje mukoje, mna unazi wa ajabu ajabu, iwe huyo Malecela kawa malaika si mtu kuwa hawezi kutoka kauli ya kuwaudhi watu mpaka isemwe kuwa aliwahi kusema alipokuwa na pahala fulani, ushahidi gani tena unatakiwa hapa, nijuavyo hapa si mahakamani kama tuthibitishe jinai pasi na shaka, lakini kilichosemwa ni dai ambalo inawezekana kasema, tatizo lipo wapi, acheni unazi huo.
- Fact: Rais Kikwete alisema bungeni Dodoma, kwamba ukitaka kula lazima uliwe,
- Unazi: Malecela aliwaambia wananchi go to hell!,
sasa kama huu sio unazi sema alisemea wapi, du inasikitisha unakaataa unazi unaousema anyways, mkuu hupendi unazi sema Malecela alisemea wapi hayo maneno, kama huna facts basi achana na unazi,
- Ni kawaida yetu JF kudai facts inapobidi au kwa sababu mni Malecela hatuhitaji facts? ila unazi tu unatosha!, Bwa! ha! ha!
Es
Mzee FMES, usibishe kuwa Malecela hakuwahi kutamka kuwa".... I will tell them, you can go to hell." Ukweli ni kuwa John ambaye bado alikuwa angali kijana wakati huo (almost 30 years ago) alimwaga lazi hiyo kwenye hafla fulani ya TRC pale Gerezani . Mimi nilikuwa Mgulani JKT wakati huo na ninakumbuka sana mjadala uliofuatia kuhusu kauli yake ile. Nina imani kuwa hakuwa anataka kutukana watu bali labda alikuwa anatia utani tu kwenye hotuba yake kwani alikuwa keshatuliza safari kadhaa. Lakini kubisha kuwa it never happened utakuwa huwatendei haki waliozaliwa baada ya hapo.
Kuna hii ya Mzee Ali H. Mwinyi enzi zile akiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.....
Alimuachia huru rubani mmoja hivi (Kapt Aziz) aliekutwa akisafirisha dhahabu kwa njia ya magendo..Mzee ruksa alisema;...
"Mama yake amekuja kwangu na amenililia saana ametia huruma sana mama yuule, kasema ni mwanae pekee anemsadia kwani yeye ni mzee sasa. Jamani ametia huruma sana mama yule, nika msamehe Rubani Aziz"
Sasa kimbembe kikaja, watanzania wa Tz wangapi wamefungwa na wazazi wao hawana uwezo wa kumuona Raisi ili wasamehewe?? tena wengine wlifungwa kwa kusingiziwa tu na wengine kwa makosa madogomadogo kama kuiba sahani kwa mama lishe, kuiba saa ya mkononi n.nk!!!
- Mkuu Kichuguu, wewe ni msomi na ni mtumzima sana, sasa kwanza ni dhambi kwa Mungu wako kushuhudia uongo au kitu chochote usichokuwa na uhakika nacho, na this one huna ukweli wala facts ila simply unashudia UONGO.
- Hii habari inadaiwa na walioitengenza kwamba aliisema kwenye hafla iliyofanyika kwenye Club ya Railways, iliyokuwepo pale karibu na kituo cha Treni za TRC pale karibu na Central Police, kwa hiyo kama kweli ulisoma mijadala iliyofuata basi ungejua kwamba huu unaousema wa Gerezani ni uongo wa mchana! Kwamba alikua na miaka 30 ni pure nonsense!
- Pili waliotunga hii habari walidai alikuwa amelewa, ukweli ni kwamba hakuwa amelewa, siku tatu kabla ya hiyo siku kiongozi mmoja wa CCM enzi hizo kwa jina Mhaville, alimuonya ofisa mmoja wa Wizara ya Mwasiliano kwamba "'...huyo super waziri wenu kuna siku ataona cha moto.." katika mjadala wa kongamano moja lilohusu Mawasiliano. Malecela siku ya siku alihudhuria hafla pale TRC Club, sherehe ilipomalizika aliondoka kuelekea nyumbani kwake, kesho yake Jumapili asubuhi magazeti ya Mzalendo na Sunday News, yaliibuka na habari nzito sana kurasa za mbele kwamba Malecela amewatukana wanachi, it was a big shock kwenye Malecela's world kwa sababu alipokuwa pale kwenye party hakuongea wala kusema anything.
- Ikafuatia a very serious investigations ambayo iliibua mengi sana as majibu ya hii habari na walioitunga, na kwamba walimtumia Marehemu Mapunda aliyekuwa Personal Assistant wa Malecela, within two weeks Mapunda akapewa Ubunge wa taifa, na akawa waziri wa kazi. Lakini maskini wa mungu alikuwa ameshamalizwa maini na ulevi wa pombe kali, unajua enzi zile waliosomea Soviet kama huyu mzee, but the damage was done as usual of politcs.
- Nyang'anyi alipokuwa waziri wa hiyo hiyo wizara na yeye alisingiziwa kwamba ameiba hela za panton ya kigamboni, mpaka ulipokuja kugundulika ukweli kwamba alieiba ni aliyekwua katibu wake Ongara, but the damage was done ndio akahamishiwa ubalozi DC.
Respect.
FMEs!
"Kwani kuna ubaya gani kukumbatia Matajiri kwenye Chama...Tukiita masikini tutaletewa Kuku"!
-Yusufu Makamba, Katibu Mkuu wa CCM, 2009
Haya ni mambo yaliyotokea zamani sana wakati wa utawala wa Mwalimu; ni kipindi ambacho vyombo vya habari vilikuwa vinamilikiwa na serikali pamoja na CHAMA. Udaku kwenye vyombo vya habari haukuwepo kabisa wakati huo unless waliozusha taarifa hiyo ni hiyo wawe wametoka serikalini kwa ajili ya propaganda. Hata hivyo ni vigumu sana kwangu mimi kukubalikuwa huo ulikuwa uzushi kwani sioni motive yoyote hasa kwa vile Malecela huyo alibaki kuwa ni mmoja na pekee kati ya mawaziri walitumikia serikali ya Nyerere kwa muda mrefu sana hadi Nyerere anaondoka madarakani mwaka 1985.
Inawezekana kuwa details nyingine za lini na wapi zikakosewa hapa na pale lakini jambo hilo lilitokea. Na kama hukubali kabisa basi tufanye project ya kutafurta records za RTD, Daily/Sunday News na Uhuru/Mzalendo. Haiwezekani tasisi zote hizo zikawa zimepoteza record hizo. Hata kama wamepoteza records zao, tunaweza kupata nakala za magazeti yote yaliyochapishwa Tanzania kutoka kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yamehifadhiwa kwenye microfiche.
hahahah hata mimi nimeisoma leo asubuhi hii kauli in IPP MediaSi kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge-Basil Pesambili Mramba
Kaitoa hiyo kauli jana huko himo kwenye mkutano wa KKT
- Eti aliyasemea wapi hayo maneno huyo baba yako? Kuanguka sio tatizo ila tatizo umeangukia wapi, kama umeangushwa ubunge wa bongo, halafu ukapewa kazi na Commonwealth as Eminent Person kwenda kuongea na Mandela jela, tena ukishirikiana na Rais wa Nigeria Obasanjo, halafu ukaja kuwa sio mbunge tu kwa miaka zaidi ya 20, bali Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, na Makamu wa CCM taifa, ume-retire na taifa linakutuza mpaka mwisho wa maisha yako, eti mkuu na mimi basi naomba kuanguka kwa namna hiyo!
- Kwenye siasa ni kama kwenye maisha inategemea umeangukia wapi na kama umeamka huko ulikoangukia,
- Again kuna yoyote huko anayejua hayo maneno huyo baba yako aliyasemea wapi ana nani waliomsikia akisema? Bwa! ha! ha! acheni kuleta majungu hapa mnaona mnavyoabika, eti alisema wapi? Hili swali hamuwezi kujibu maana aliyepandikizwa kuanzisha yale maneno hamumjui na kwamba baada ya kutimiza ile kazi alipewa ubunge wa bure na uwaziri juu yake kama zawadi kwa ile kazi, lakini masikini ya mungu hakuenda mbali akatangulia kwenye haki ghafla, poleni sana huko na ule msiba wa ajabu sana.
Es!
- Hivi katika siasa za vyama vingi, technically nini tatizo la hii kauli?
Respect.
FMEs!
''....nimeonewa sana,nimesemwa sana kwenye jambo hili,nimetukanwa sana,........nimenyanyaswa sana mimi,...!na kwakweli sijatendewa haki!...najua tatizo ni huu uwaziri mkuu..''