Kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania

Kauli za mawaziri zinamaanisha kuwa wanachoamua wao hakuna wa kukipinga hata kama kinawahusu wananchi/umma.

Kauli za marais zinamaanisha kuwa njia walizotumia kuupata uongozi si za haki/ wengi wanawapinga katika uongozi na namna walivyopata uongozi na kwa kuwa hawawezi kufanywa kitu basi wanaolalamika walie tu
 
Sawa, lakini kwa Mkapa kauli zake 3 na 4 zinamwonyesha zaidi na mahususi kama ni mtu mwenye hasira na kiburi cha kupita kiasi. Je namba tano tumwelezeje kutokana na kauli yake?
 
''kila mtu anauza ngo'mbe aliyenenepa kwani utapata bei nzuri'' kauli ya mramba alipokua akitetea uuzwaji wa nmb kwani watu wengi walihoji si inajiendesha kwa faida wakati tunatakiwa tuuze mashirika yanayojiendesha kwa hasara apo ndio wengine tukajua serikali ya awamu ya tatu wamegundua ubinafsishaji mpya wa kuuza kila kitu kama kesho tunaku kiwe na faida kisiwe na faida uza tu!
 
''kila mtu anauza ngo'mbe aliyenenepa kwani utapata bei nzuri'' kauli ya mramba alipokua akitetea uuzwaji wa nmb kwani watu wengi walihoji si inajiendesha kwa faida wakati tunatakiwa tuuze mashirika yanayojiendesha kwa hasara apo ndio wengine tukajua serikali ya awamu ya tatu wamegundua ubinafsishaji mpya wa kuuza kila kitu kama kesho tunaku kiwe na faida kisiwe na faida uza tu![/QUOTE]

Ka, hivi Mramba anamatatizo gani? Mara kula nyasi, mara watu watembee kwa miguu, sasa hii ya kunenepesha ng'ombe kwani NBC ilikuwa mali yake ya ya watanzania wote, aliitoa mwaka gani? unakumbuka alitoa akiwa wapi?
 
Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe!-Mkapa ,rais wa Tanzania awamu ya tatu.
 
"wananchi wa Mbagala inabidi wazoee TU milio ya mabomu kama wananchi wa Kipawa walivyozoea milio ya ndege...eeh...eeeh watazoea tu"
Mkuu wa Mkoa Dsm, Mh. WILLIAM LUKUVI mwaka jana (2009).
 
- Eti jamani zipo evidence za ku-back up hizi claims, kwamba wananchi waliudhika? Yaani hawa wananchi hawakuudhika kuibiwa hela zao katika IPTL, Radar, na Richimonduli, lakini waliudhishwa na kauli tu! Labda ndio maana tupo hapa tulipo! taifa la majungu majungu viongozi mpaka wananchi ni majungu majungu,

- Ninakumbuka majungu Zitto anatembea na barua ya kujiuzulu mpaka leo bado yupo Chadema, ndio taifa letu majungu majungu tu na uongo uongo!

- Vipi evidence?

Respect.

FMEs!
Kaka unachosema ni kweli hasa baada yakuwa wamekumbusha statement mbaya zilizowahi kutolewa na mzee wako embe bivu..........mpaka leo wagogo wanakumbuka statement hio na ndio maana walimwangusha ubunge wakati aliposema kuwa go to hell...........pole kaka usichukie baba yangu alitunguliwa
 
Katika kutafakari hali ya siaza za Tanzania nimekumbuka baadhi ya kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania. Kauli hizi zinawaelezaje wahusika? Na ili kuweka mambo sawa hebu tujaze mazingira na mwaka wa kauli hizi.

1. Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe- Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha wakati wa kikao cha bunge la bajeti mwaka 1989

2. Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa - Mramba akiwa waziri wa fedha, mwaka.......

3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....

4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..

5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...

6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....

Kwa kweli Mkapa ndiye rais pekee katika historia ya nchi hii aliye tutukana sana!!! Hiyo kwenye red...ni mbaya kuzidi zote mkuu.
 
ukila cha mwenzio na wewe lazima uliwe

Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa

HII NI MISEMO YA KIJINGA KULIKO MISEMO YOYOTE ILE KUWAHI KUTOKEA!!!
 
[QUOTE3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....

4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..

5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...

6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....

Kwa kweli Mkapa ndiye rais pekee katika historia ya nchi hii aliye tutukana sana!!! Hiyo kwenye red...ni mbaya kuzidi zote mkuu.

Ndiyo maana inatubidi tuandike historia vizuri. Nami naona kuwa kauli namba 5. inamwonyesha Kikwete kama rais asiyejali chochote yaani ni mtu wa kupuuza mambo yanayoikabili nchi. Hii inajionyesha wazi mfano anaacha kupambana na majanga mengi katika nchi anakimbilia ng'ambo. Marais wanaopenda wananchi wao hubaki ndani ya nchi zao kutatua matatizo hasa yale ya majanga yanapojitokeza. Sasa tumalizie namba 6. tunaweza kumwelezaje mtu huyu na kauli yake?
 
Hiyo Na.4 inawezekanana kweli ni wavivu wakufikiri maana ingekuwa sio wavivu wa kufikiri tungekuwa tunachagua kilichobora sio bora kilichochaguliwa. nchi jirani tena waliotoka kwenye vita wamefikiri wakaamua kuijenga nchi yao kwa hali na mali, usafi wanaongoza na mambo mengi tena watakuja kutuacha nyuma.

Ukiangalia kwetu, maneno mengi, kulalamika kwingi, vitendo vidogo ukiangalia hali ya uchafu mijini usiseme na vipindupindu haviishi, ujenzi holela ndio kabisa, utitili wa vyama vya siasa ndio hoi, kila mtu anataka kugombea ubunge, urais, n.k yote nini madaraka la maana linaloonekana hakuna vyama vyote makao yao makuu dar. Mikoani hakuna kitu, Ukiangalia maendeleo ya elimu duni, na pengine tunaongoza kwa migomo. mashirika ya umma yamekufa lakini waliyoyaua ni sisi wenyewe kwa kuyaibia yalipofilisika yakabinafsishwa waliyoyanunua wageni ndio wameyaua kabisa kwa hiyo siku sizi hakuna sifa za Sungura tex, Mwatex wala nini; Wakulima wakipima mazao yako i.e pamba mizani zinawaibia mwishoe nao wamechoka kupoteza jasho lao wanaona waongeze uzito au kwa kutia maji au vinginevyo mazao yakienda nje yanaoneka hayana ubora tunakosa soko, Wavuvi nao wamevua kwa nyavu haramu mpaka wameharibu mazalia ya samaki matokea yake wamebaki kutulisha walivyovua na mabomu. Wakiambiwa vueni kwa kwa nyavu nzuri msiharibu mazalia ya samaki hawataki wanasubiri kiza kwenda kuvua kwa wizi ili mradi ni ufisadi kila kona. Majangili nayo hayakuachwa nyuma kuuwa wanyama n.k n.k hakuna cha kujivunia si Air Tanzania, si reli ambayo nayo ni marehemu.tumebaki kupanda ndege za wenzetu tukitataka kwenda Kenya au jirani Rwanda. Tumebaki kuimba mbuga za wanyama basi vingine vya manufaa tumeshaviangamiza migodi nayo ndiyo inachimbwa kwa bidii mwisho wa siku tunaachiwa mashimo na majangwa. Nafikiri tunagekuwa tunafikiri kweli hao Wabia tungekuwa tunawekeana nao mikataba yenye manufaa kwetu yaani kwa kipindi fulani ili ule utaalamu wao baada ya muda wanakuwa wametufundisha kisha huo muda kweli ukifika yule Mtanzania aliyewekwa pale kujifunza anachukua ile nafasi tungejikuta baada labda ya miaka kumi ile mitambo ya kuchimbia hayo madini tunaimiliki sisi wenyewe, na tena tungeshakuwa na viwanda hata vya kusafisa, kukata na kutengeneza hivyo vito bila kupeleka nje na hii strategy nafikiri Wenzetu walio makini kama Rwanda ndio wanaitumia. Wakati mwingine huwa naona aibu kama kiwanda cha matairi kimefilisika tukaanza kuagiza nje, viwanda vya nguo vimefilisika tukaanza kuvaa vya jirani zetu, shirika la ndege tumeliua tuaanza kupanda za jirani zetu ambazo kwao kama kq ipo miaka nenda rudi, reli nayo tunaiua tutapanda nini? hakuna kuinjoi. tunabaki kusema tuna madini mengi lakini yanawasaidia walio wachache. Hii Kauli ukiifikiria kwa makini ina ukweli tubaki kuliwa tu.

Na haohao tunaowalalamikia ukifika uchaguzi utakuta ndio wameshinda kwa kishindo wapinzani hoi tatizo ni nini kama sio uvivu wa kufikiri na kutambua hivi tunakwenda wapi.

Mifuko ya Plastiki wakisema inaharibu mazingira hao waosema hawawezi kuchukua action ya kuitoa kwenye soko maana ndio hao hao wenye viwanda wakale wapi. Ukiangalia Rwanda Walipiga marufuku Mifuko ya plastiki mwezi mmja tu hakuna mfuko wa plastiki uliooneka mtaani kote wamezoea kutumia mifuko ya karatasi hata kama ni kuwekea nyama. huwezi ukaona mitaro michafu yenye maji yaliyovunda kama kwetu. kwentu imebaki porojo tu. watu wanasubiria usiku ukifika wakamwage uchafu barabarani. Sasa jamani kama sio uvivu wa kufikiri ni nini. Naamini unapofikiri unaweza kupata uamuzi ulio bora na sahihi kuliko kuendelea kulalamika na ndio maana tunatukanwa kiaina. Tukiamka hatuwezi kuwa na utitiri wa vyama visivyo na tija, Tukiamka na kufikiri vyema tutawachagua wabunge, madiwani mameya, wenyeviti wa mitaa walio bora bila kuhongwa sabuni, kanga, mafuta ya kupikia n.k.

pengine kungekuwa na utawala wa majimbo labda tungesonga mbele maana tungekuwa na magavana wa majimbo so kila jimbo lingejitahidi kuendelea lisibaki nyuma. ni maoni tu.
 
CKABULA umeongea kwa hisia za uchungu mkubwa wa kuipenda nchi yetu. Ongeza hili, kuwa ni kawaida kwa wafanyabishara wa dagaa Mwanza kununua mchanga kwenye malori na kupeleka ziwani tena mchana kweupe kuchanganya na dagaa ili kuongeza uzito bila kujali athari kwa afya za watu. Wafanya biashara wa ulezi nao huweka mchanga kuongeza uzito.
 
Kaka unachosema ni kweli hasa baada yakuwa wamekumbusha statement mbaya zilizowahi kutolewa na mzee wako embe bivu..........mpaka leo wagogo wanakumbuka statement hio na ndio maana walimwangusha ubunge wakati aliposema kuwa go to hell...........pole kaka usichukie baba yangu alitunguliwa

- Eti aliyasemea wapi hayo maneno huyo baba yako? Kuanguka sio tatizo ila tatizo umeangukia wapi, kama umeangushwa ubunge wa bongo, halafu ukapewa kazi na Commonwealth as Eminent Person kwenda kuongea na Mandela jela, tena ukishirikiana na Rais wa Nigeria Obasanjo, halafu ukaja kuwa sio mbunge tu kwa miaka zaidi ya 20, bali Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, na Makamu wa CCM taifa, ume-retire na taifa linakutuza mpaka mwisho wa maisha yako, eti mkuu na mimi basi naomba kuanguka kwa namna hiyo!

- Kwenye siasa ni kama kwenye maisha inategemea umeangukia wapi na kama umeamka huko ulikoangukia,

- Again kuna yoyote huko anayejua hayo maneno huyo baba yako aliyasemea wapi ana nani waliomsikia akisema? Bwa! ha! ha! acheni kuleta majungu hapa mnaona mnavyoabika, eti alisema wapi?
Hili swali hamuwezi kujibu maana aliyepandikizwa kuanzisha yale maneno hamumjui na kwamba baada ya kutimiza ile kazi alipewa ubunge wa bure na uwaziri juu yake kama zawadi kwa ile kazi, lakini masikini ya mungu hakuenda mbali akatangulia kwenye haki ghafla, poleni sana huko na ule msiba wa ajabu sana.

Es!
 
Katika kutafakari hali ya siaza za Tanzania nimekumbuka baadhi ya kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania. Kauli hizi zinawaelezaje wahusika? Na ili kuweka mambo sawa hebu tujaze mazingira na mwaka wa kauli hizi.

1. Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe- Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha wakati wa kikao cha bunge la bajeti mwaka 1989

2. Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa - Mramba akiwa waziri wa fedha, mwaka.......

3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....

4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..

5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...

6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....

Baada ya kuziweka kumbukumbu vizuri tujiulize, hivi kauli zao hao wahusika zinawaeleza vipi?. Kwa maoni yangu kauli 1 na 2 zinawaeleza mawaziri wa fedha kama watu wasiokuwa na huruma. Kauli zingine zinawaelezaje wengine?

7.tumechoshwa kwa watanzania kubeba vimifuko vya simenti...Kigamboni iuzwe..waziri wa arizi CHILIGATI mwaka....
 
- Mkuu Ogah, hii kauli Malecela aliitolea wapi maana mpaka leo huwa hatujawahi kuambiwa alipoitolea vipi ukitusaidia alipoitolea na waliomsikia akisema?

Respect.

FMEs!
Nyie watu wengine sijuwi mukoje mukoje, mna unazi wa ajabu ajabu, iwe huyo Malecela kawa malaika si mtu kuwa hawezi kutoka kauli ya kuwaudhi watu mpaka isemwe kuwa aliwahi kusema alipokuwa na pahala fulani, ushahidi gani tena unatakiwa hapa, nijuavyo hapa si mahakamani kama tuthibitishe jinai pasi na shaka, lakini kilichosemwa ni dai ambalo inawezekana kasema, tatizo lipo wapi, acheni unazi huo.
 
Back
Top Bottom