Kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania

Nyie watu wengine sijuwi mukoje mukoje, mna unazi wa ajabu ajabu, iwe huyo Malecela kawa malaika si mtu kuwa hawezi kutoka kauli ya kuwaudhi watu mpaka isemwe kuwa aliwahi kusema alipokuwa na pahala fulani, ushahidi gani tena unatakiwa hapa, nijuavyo hapa si mahakamani kama tuthibitishe jinai pasi na shaka, lakini kilichosemwa ni dai ambalo inawezekana kasema, tatizo lipo wapi, acheni unazi huo.

- Fact: Rais Kikwete alisema bungeni Dodoma, kwamba ukitaka kula lazima uliwe,

- Unazi: Malecela aliwaambia wananchi go to hell!,

sasa kama huu sio unazi sema alisemea wapi, du inasikitisha unakaataa unazi unaousema anyways, mkuu hupendi unazi sema Malecela alisemea wapi hayo maneno, kama huna facts basi achana na unazi,

- Ni kawaida yetu JF kudai facts inapobidi au kwa sababu mni Malecela hatuhitaji facts? ila unazi tu unatosha!, Bwa! ha! ha!

Es
 
Mzee FMES, usibishe kuwa Malecela hakuwahi kutamka kuwa".... I will tell them, you can go to hell." Ukweli ni kuwa John ambaye bado alikuwa angali kijana wakati huo (almost 30 years ago) alimwaga lazi hiyo kwenye hafla fulani ya TRC pale Gerezani . Mimi nilikuwa Mgulani JKT wakati huo na ninakumbuka sana mjadala uliofuatia kuhusu kauli yake ile. Nina imani kuwa hakuwa anataka kutukana watu bali labda alikuwa anatia utani tu kwenye hotuba yake kwani alikuwa keshatuliza safari kadhaa. Lakini kubisha kuwa it never happened utakuwa huwatendei haki waliozaliwa baada ya hapo.
 
- Mkuu Kichuguu, wewe ni msomi na ni mtumzima sana, sasa kwanza ni dhambi kwa Mungu wako kushuhudia uongo au kitu chochote usichokuwa na uhakika nacho, na this one huna ukweli wala facts ila simply unashudia UONGO.

- Hii habari inadaiwa na walioitengenza kwamba aliisema kwenye hafla iliyofanyika kwenye Club ya Railways, iliyokuwepo pale karibu na kituo cha Treni za TRC pale karibu na Central Police, kwa hiyo kama kweli ulisoma mijadala iliyofuata basi ungejua kwamba huu unaousema wa Gerezani ni uongo wa mchana! Kwamba alikua na miaka 30 ni pure nonsense!

- Pili waliotunga hii habari walidai alikuwa amelewa, ukweli ni kwamba hakuwa amelewa, siku tatu kabla ya hiyo siku kiongozi mmoja wa CCM enzi hizo kwa jina Mhaville, alimuonya ofisa mmoja wa Wizara ya Mwasiliano kwamba "'...huyo super waziri wenu kuna siku ataona cha moto.." katika mjadala wa kongamano moja lilohusu Mawasiliano. Malecela siku ya siku alihudhuria hafla pale TRC Club, sherehe ilipomalizika aliondoka kuelekea nyumbani kwake, kesho yake Jumapili asubuhi magazeti ya Mzalendo na Sunday News, yaliibuka na habari nzito sana kurasa za mbele kwamba Malecela amewatukana wanachi, it was a big shock kwenye Malecela's world kwa sababu alipokuwa pale kwenye party hakuongea wala kusema anything.

- Ikafuatia a very serious investigations ambayo iliibua mengi sana as majibu ya hii habari na walioitunga, na kwamba walimtumia Marehemu Mapunda aliyekuwa Personal Assistant wa Malecela, within two weeks Mapunda akapewa Ubunge wa taifa, na akawa waziri wa kazi. Lakini maskini wa mungu alikuwa ameshamalizwa maini na ulevi wa pombe kali, unajua enzi zile waliosomea Soviet kama huyu mzee, but the damage was done as usual of politcs.

- Nyang'anyi alipokuwa waziri wa hiyo hiyo wizara na yeye alisingiziwa kwamba ameiba hela za panton ya kigamboni, mpaka ulipokuja kugundulika ukweli kwamba alieiba ni aliyekwua katibu wake Ongara, but the damage was done ndio akahamishiwa ubalozi DC.

Respect.

FMEs!
 
Kuna hii ya Mzee Ali H. Mwinyi enzi zile akiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.....
Alimuachia huru rubani mmoja hivi (Kapt Aziz) aliekutwa akisafirisha dhahabu kwa njia ya magendo..Mzee ruksa alisema;...
"Mama yake amekuja kwangu na amenililia saana ametia huruma sana mama yuule, kasema ni mwanae pekee anemsadia kwani yeye ni mzee sasa. Jamani ametia huruma sana mama yule, nika msamehe Rubani Aziz"
Sasa kimbembe kikaja, watanzania wa Tz wangapi wamefungwa na wazazi wao hawana uwezo wa kumuona Raisi ili wasamehewe?? tena wengine wlifungwa kwa kusingiziwa tu na wengine kwa makosa madogomadogo kama kuiba sahani kwa mama lishe, kuiba saa ya mkononi n.nk!!!

Nimecheka sana na umenikumbusha enzi za fagio la chuma teh teh Mzee Ruksa
 
- Mkuu Kichuguu, wewe ni msomi na ni mtumzima sana, sasa kwanza ni dhambi kwa Mungu wako kushuhudia uongo au kitu chochote usichokuwa na uhakika nacho, na this one huna ukweli wala facts ila simply unashudia UONGO.

- Hii habari inadaiwa na walioitengenza kwamba aliisema kwenye hafla iliyofanyika kwenye Club ya Railways, iliyokuwepo pale karibu na kituo cha Treni za TRC pale karibu na Central Police, kwa hiyo kama kweli ulisoma mijadala iliyofuata basi ungejua kwamba huu unaousema wa Gerezani ni uongo wa mchana! Kwamba alikua na miaka 30 ni pure nonsense!

- Pili waliotunga hii habari walidai alikuwa amelewa, ukweli ni kwamba hakuwa amelewa, siku tatu kabla ya hiyo siku kiongozi mmoja wa CCM enzi hizo kwa jina Mhaville, alimuonya ofisa mmoja wa Wizara ya Mwasiliano kwamba "'...huyo super waziri wenu kuna siku ataona cha moto.." katika mjadala wa kongamano moja lilohusu Mawasiliano. Malecela siku ya siku alihudhuria hafla pale TRC Club, sherehe ilipomalizika aliondoka kuelekea nyumbani kwake, kesho yake Jumapili asubuhi magazeti ya Mzalendo na Sunday News, yaliibuka na habari nzito sana kurasa za mbele kwamba Malecela amewatukana wanachi, it was a big shock kwenye Malecela's world kwa sababu alipokuwa pale kwenye party hakuongea wala kusema anything.

- Ikafuatia a very serious investigations ambayo iliibua mengi sana as majibu ya hii habari na walioitunga, na kwamba walimtumia Marehemu Mapunda aliyekuwa Personal Assistant wa Malecela, within two weeks Mapunda akapewa Ubunge wa taifa, na akawa waziri wa kazi. Lakini maskini wa mungu alikuwa ameshamalizwa maini na ulevi wa pombe kali, unajua enzi zile waliosomea Soviet kama huyu mzee, but the damage was done as usual of politcs.

- Nyang'anyi alipokuwa waziri wa hiyo hiyo wizara na yeye alisingiziwa kwamba ameiba hela za panton ya kigamboni, mpaka ulipokuja kugundulika ukweli kwamba alieiba ni aliyekwua katibu wake Ongara, but the damage was done ndio akahamishiwa ubalozi DC.

Respect.

FMEs!

Haya ni mambo yaliyotokea zamani sana wakati wa utawala wa Mwalimu; ni kipindi ambacho vyombo vya habari vilikuwa vinamilikiwa na serikali pamoja na CHAMA. Udaku kwenye vyombo vya habari haukuwepo kabisa wakati huo unless waliozusha taarifa hiyo ni hiyo wawe wametoka serikalini kwa ajili ya propaganda. Hata hivyo ni vigumu sana kwangu mimi kukubalikuwa huo ulikuwa uzushi kwani sioni motive yoyote hasa kwa vile Malecela huyo alibaki kuwa ni mmoja na pekee kati ya mawaziri walitumikia serikali ya Nyerere kwa muda mrefu sana hadi Nyerere anaondoka madarakani mwaka 1985.

Inawezekana kuwa details nyingine za lini na wapi zikakosewa hapa na pale lakini jambo hilo lilitokea. Na kama hukubali kabisa basi tufanye project ya kutafurta records za RTD, Daily/Sunday News na Uhuru/Mzalendo. Haiwezekani tasisi zote hizo zikawa zimepoteza record hizo. Hata kama wamepoteza records zao, tunaweza kupata nakala za magazeti yote yaliyochapishwa Tanzania kutoka kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yamehifadhiwa kwenye microfiche.
 
"Kama CCM haitashinda tutawaambia TRA waje wakague kama huwa mna lipa kodi ya mapato lakini hatutafanya hivyo ikiwa tu mtatupa kura" Waziri wa Nishati na madini Mh Ngeleja wakati wa kampeni za ubunge mji mdogo wa Katoro trh 21/5/2009
 
"Msisikilize kile kinachosemwa bungeni, bunge lina mambo yake mimi kama waziri mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni" PM Mizengo Pinda Feb 2010
 
Haya ni mambo yaliyotokea zamani sana wakati wa utawala wa Mwalimu; ni kipindi ambacho vyombo vya habari vilikuwa vinamilikiwa na serikali pamoja na CHAMA. Udaku kwenye vyombo vya habari haukuwepo kabisa wakati huo unless waliozusha taarifa hiyo ni hiyo wawe wametoka serikalini kwa ajili ya propaganda. Hata hivyo ni vigumu sana kwangu mimi kukubalikuwa huo ulikuwa uzushi kwani sioni motive yoyote hasa kwa vile Malecela huyo alibaki kuwa ni mmoja na pekee kati ya mawaziri walitumikia serikali ya Nyerere kwa muda mrefu sana hadi Nyerere anaondoka madarakani mwaka 1985.

Inawezekana kuwa details nyingine za lini na wapi zikakosewa hapa na pale lakini jambo hilo lilitokea. Na kama hukubali kabisa basi tufanye project ya kutafurta records za RTD, Daily/Sunday News na Uhuru/Mzalendo. Haiwezekani tasisi zote hizo zikawa zimepoteza record hizo. Hata kama wamepoteza records zao, tunaweza kupata nakala za magazeti yote yaliyochapishwa Tanzania kutoka kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; yamehifadhiwa kwenye microfiche.

- Mwalimu Kichuguu wewe ni mtumzima na unaheshimika sana hapa, acha kuendelea kujivua nguo ndugu yangu, huna ukweli on this ishu kubali tu, habari yako ya kwanza umesisistiza kwamba Malecela alisema na unajua as a fact kwamba alisemea Gerezani, na kwamba alikuwa in his 30s, huu ni uongo either wa makusudi au wa kutokuelewa,

1. TRC Club haiko Gerezani, ambako ndiko inakosemekana alisema hayo maneno,

2. Pili hebu piga hesabu ilipodaiwa amesema na umri wa Malecela wa sasa, halafu with your right mind usimame kama ulivyofanya pale nyuma na kusema Malecela alikuwa na miaka 30, ndio ninakwambia wazi kwamba huelewi unachosema kwa sababu huna ukweli, sasa kaa pembeni au tafuta ukweli, si unajua no research no right to speak,

- Sasa kwanza umeleta uongo, haalfu baada ya kubanwa unasema ndio tuka-research, Kichuguu hili taifa linadidimia kwa sababu ya watu kama wewe, mnatumainisha kwamba ni wasomi, halafu mnaaanza kutuuzia mbuzi kwenye magunia, wewe mtumzima na akili timamu kweli unaweza kusimama mbele ya hii public na kusema eti enzi zile magazeti yalikuwa hayasemi uongo!

- Tuliambiwa maneno mangapi ya uongo kuhusu Kambona?, uongo kuhusu Kawawa?, uongo kuhusu Jumbe? uongo kuhusu vijiji vya ujamaa ni gazeti gani kati ya hayo unayoyasema liliwahi kukubali kwamba wananchi wanaliwa na simba katika kuhamishwa kutoka sehemu zao za asili kwenda kwenye mapori ya vijiji vipya vya ujamaa?

- Kichuguu soon vitabu vinakuja, vya kujbu propaganda nyingi sana za uongo wa enzi zile ili kuwapa wananchi alternative na waamue nani alisema ukweli na nani alisema uongo, Mkuu nilikuwa ninakuheshimu sana mpaka nilipoona huu uongo wako wa jana pale juu. Maana tizama maelezo yako na yangu mkuu si unaona uongo na ukweli vinavyjitenga!

Respect.

FMEs!
 
Ukisimamisha jiwe kwa tiketi ya ccm kwenye uchaguzi, litashinda.........
 
Si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge-Basil Pesambili Mramba

Kaitoa hiyo kauli jana huko himo kwenye mkutano wa KKT
 
Si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge-Basil Pesambili Mramba

Kaitoa hiyo kauli jana huko himo kwenye mkutano wa KKT
hahahah hata mimi nimeisoma leo asubuhi hii kauli in IPP Media
 
Hakuna kauli iliyowaudhi "sana" Watanzania.Ingewaudhi "sana" wangewatoa hawa CCM kwenye utawala, hawajafanya hivyo.
 
- Eti aliyasemea wapi hayo maneno huyo baba yako? Kuanguka sio tatizo ila tatizo umeangukia wapi, kama umeangushwa ubunge wa bongo, halafu ukapewa kazi na Commonwealth as Eminent Person kwenda kuongea na Mandela jela, tena ukishirikiana na Rais wa Nigeria Obasanjo, halafu ukaja kuwa sio mbunge tu kwa miaka zaidi ya 20, bali Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, na Makamu wa CCM taifa, ume-retire na taifa linakutuza mpaka mwisho wa maisha yako, eti mkuu na mimi basi naomba kuanguka kwa namna hiyo!

- Kwenye siasa ni kama kwenye maisha inategemea umeangukia wapi na kama umeamka huko ulikoangukia,

- Again kuna yoyote huko anayejua hayo maneno huyo baba yako aliyasemea wapi ana nani waliomsikia akisema? Bwa! ha! ha! acheni kuleta majungu hapa mnaona mnavyoabika, eti alisema wapi? Hili swali hamuwezi kujibu maana aliyepandikizwa kuanzisha yale maneno hamumjui na kwamba baada ya kutimiza ile kazi alipewa ubunge wa bure na uwaziri juu yake kama zawadi kwa ile kazi, lakini masikini ya mungu hakuenda mbali akatangulia kwenye haki ghafla, poleni sana huko na ule msiba wa ajabu sana.

Es!

Mkuu Field Marshal ES,

Nimecheka sana mkuu wangu.Napenda sana unavyojibu hoja kwa vigongo...duh,sina mbavu hapa
 
Kuna hii nayo,

Zanzibar siyo nchi-Mizengo Pinda

Aliisemea bungeni,kauli hii iliwaudhi sana watanzania wa visiwani
 
- Hivi katika siasa za vyama vingi, technically nini tatizo la hii kauli?

Respect.

FMEs!

Mkuu Respect. Tatizo la hii kauli ni kukua kwa utamaduni wa KIFISADI CCM. Yaani ili upate tenda za kuliibia Taifa ni lazima uwe karibu na wale walijitwalia dhamana ya kutawala. Hii ni moja ya kauli za KIFISADI ambao leo hii hata wewe unaupinga. Chanzo cha UFISADI ni wafanyabiashara ambao msingi wao ni faida na wanapoingia CCM kushika nafasi za uongozi basi wao FOCUS yao ni kufaidika binafsi
 
''....nimeonewa sana,nimesemwa sana kwenye jambo hili,nimetukanwa sana,........nimenyanyaswa sana mimi,...!na kwakweli sijatendewa haki!...najua tatizo ni huu uwaziri mkuu..''

kweli hii hata mimi ilinikera hasa pale alipoongezea "kama mimi wanaweza kunifanyia hivyo je hao wadogo" maana yake kuna tabaka la walionacho na wasionacho
 
''ukitaka kula lazima uliwe'' - kikwete kwenye live television when he adresses the nation.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom