Kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Mar 3, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kutafakari hali ya siaza za Tanzania nimekumbuka baadhi ya kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania. Kauli hizi zinawaelezaje wahusika? Na ili kuweka mambo sawa hebu tujaze mazingira na mwaka wa kauli hizi.

  1. Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe- Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha wakati wa kikao cha bunge la bajeti mwaka 1989

  2. Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa - Mramba akiwa waziri wa fedha, mwaka.......

  3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....


  4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..


  5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...


  6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....


  Baada ya kuziweka kumbukumbu vizuri tujiulize, hivi kauli zao hao wahusika zinawaeleza vipi?. Kwa maoni yangu kauli 1 na 2 zinawaeleza mawaziri wa fedha kama watu wasiokuwa na huruma. Kauli zingine zinawaelezaje wengine?
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Give mwaw my mashine gun. How many rounds does it habe?....ok..ok, it is enough.
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi Mramba na Msuya wanatoka wapi?
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,946
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  ccm..!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sidhani kaa kuna aliyeudhika na hizo kauli. Maana nijuavyo bongo kila kitu tambarare.
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,233
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.....nafikiri hiyo statement inafanana na ile iliyotolewa na Mh Pius Msekwa..........

  7. "You can Go to Hell"........JS Malecela alipokuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.........
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Lakini ni kipi cha ajabu ?

  Tumekubali mfumo unaruhusu hawa genge la watawala watutawale ktk mfumo 'fimbo ya chuma' na tumewapa 'blank cheque' ya kuchagua lililo jema kwa niaba yetu bila kutuuliza. Sasa kama ni makosa ni yetu sote kama waTz kwa leniency, indecision & lack of daring.
   
 8. Z

  Zakayo Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Wale wote wanaosema Tanzania Railways Corporation inatoa huduma mbaya can go to hell"--John Samuel Malecela alipokuwa Waziri wa Usafirishaji na Mawasiliano mwaka 1980. Kauli ilimgharimu akakosa ubunge. Hiyo nina ushahidi iliwaudhi Watanzania wengi. Hizo hapo juu sina ushahidi
   
 9. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Alikuwa ni Pius Msekwa , Spika wa Bunge, aliposhauriwa aachane uwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom, Ili kukwepa mgongano wa maslahi kutokana na cheo chake cha Uspika!!
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 11,007
  Likes Received: 3,271
  Trophy Points: 280
  "UKITAKA biashara zako ziende vizuri basi jiunge na CCM, chagueni mafiga matatu ili muweze kupata maendeleo, mkichagua upinzani hatutaleta maendeleo."

  Nadhani mnamjua aliyesema hayo, kama haumjui soma HAPA
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Lakini ni lipi la kushangaa ikiwa wafanyabiashara hufadhili kampeni za wanasiasa na wanasiasa in return wana-scratch migongo ya wafanyabiashara ktk obvious transactions za kuuza nchi?

  Kipi kipya? Semeni!
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,937
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  ....na kauli nyingine iliyochefua ni pale dala dala za Dar zilipotishia kugoma, Mramba akiwa waziri wa fedha alisema "Wananchi watembee kwa miguu kutoka makwao kwenda vibaruani"

  Ilituchefua sana hasa sisi wakazi wa Mbagala.
   
 13. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,117
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  "mtake msitake huyu atakua rais" Julius Kambarage Nyerere alitamka maneno hayo mwaka 1995 huku akiinua bango la benjamin william mkapa, mkoani kilimanjaro..mjini moshi na uwanja mzima kila mtu akiwa ameinua mkono juu ukiwa na alma ya v ambayo ilikua alama ya chadema na nccr mageuzi...........alitupa bango chini kwa hasira na kuondoka kwenye mkutano........sitasahu siku ile nilikua mita chache kutoka alipokua mwalimu alikasirika na wananchi walifurahi
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zinawaeleza kama wamelewa fedha za hazina
   
 15. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Vizuri umeongeza nyingine na kuweka jina la mtu, cheo chake na mwaka, na kauli hiyo ilimpa zawadi gani. Tuendelee kujaza sehemu zilizobaki wazi katika kauli zingine ili kukamilisha kumbukumbu ya kauli hizo mbaya. Ni sehemu ya historia yetu watanzania
   
 16. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii nayo ni kumbukumbu katika historia ya nchi yetu lakini naona umesema watanzania walifurahi, lakini hapa tunataka kuandika historia ya kauli mbaya ambazo wananchi waliudhika sana
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Eti jamani zipo evidence za ku-back up hizi claims, kwamba wananchi waliudhika? Yaani hawa wananchi hawakuudhika kuibiwa hela zao katika IPTL, Radar, na Richimonduli, lakini waliudhishwa na kauli tu! Labda ndio maana tupo hapa tulipo! taifa la majungu majungu viongozi mpaka wananchi ni majungu majungu,

  - Ninakumbuka majungu Zitto anatembea na barua ya kujiuzulu mpaka leo bado yupo Chadema, ndio taifa letu majungu majungu tu na uongo uongo!

  - Vipi evidence?

  Respect.


  FMEs!
   
 18. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wajanja woe wapo Dar es Salaam....ya Zito Kabwe.So huku Kigoma na mikoa mingine kuna watu wa aina gani??jibu Kinyume na wajanja.Mafa**
   
 19. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Loo, huyu Mramba naona amekubuhu kwa kauli mbaya, na tena akiwa waziri wa fedha, sasa tumalizie ilikuwa mwaka gani?
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0

  - Mkuu Zakayo, hii kauli Malecela aliitolea wapi?

  Respect.


  FMEs!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...