Kauli za Chalamila zinazua maswali mengi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,858
CHALAMILA KAULI ZAKE ZINAZUA MASWALI MENGI.

Na Robert Heriel.

Nani aliyemuambia wananchi wa Mwanza Wanakinyongo na Kifo cha Magufuli?

Chalamila hajamaliza hata wiki mbili tangu awe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, sasa je aliwezaje kuzipata taarifa za Wakazi wa Mwanza kwa muda mfupi tuu kuwa watu Wanakinyongo na Kifo cha Magufuli?

Je Chalamila alikuwa akiisemea nafsi yake au alikuwa akiwasilisha vinyongo vya watu wanaomzunguka kuhusu Kifo cha Magufuli?

Je Chalamila hakuwepo wakati msiba wa Magufuli na hakusikia Sababu zilizosababisha Umauti umfikie JPM?

Je nini dhamira ya Chalamila kusema kauli hiyo?

Chalamila kusema watu Waende na Mabango yenye jumbe zozote hata za MATUSI, alikuwa anajaribu Kueleza Uhuru wa namna gani?

Chalamila akiwa Mbeya aliwahi kusema hataki Mabango ya Aina yoyote yenye jumbe za hovyo, je nini kimebadilika alipofika Mwanza?

Nilishawahi kusema, Wale wote waliokuwa wakisapuza na kuhamasisha JPM aongezewe muda wa kuongoza wanapaswa waondolewe katika nafasi walizonazo. Na Kama ni wabunge mwaka 2025 wasirudi bungeni.

Bahati nzuri wanafahamika, na wanajifahamu. Hatuwezi kuwa na taifa la viongozi wasioweza kutumia akili zao vizuri.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa MOROGORO

FB_IMG_16234792578682759.jpg
 
Alizoea kutamka maneno ya kumfurahisha mwendazake, juzi alizidisha viungo akaharibu mchuzi. Ninaamini Chalamila hakuazimia kusema watu waende na mabango ya matusi.
 
CHALAMILA KAULI ZAKE ZINAZUA MASWALI MENGI.

Na Robert Heriel.

Nani aliyemuambia wananchi wa Mwanza Wanakinyongo na Kifo cha Magufuli?

Chalamila hajamaliza hata wiki mbili tangu awe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, sasa je aliwezaje kuzipata taarifa za Wakazi wa Mwanza kwa muda mfupi tuu kuwa watu Wanakinyongo na Kifo cha Magufuli?

Je Chalamila alikuwa akiisemea nafsi yake au alikuwa akiwasilisha vinyongo vya watu wanaomzunguka kuhusu Kifo cha Magufuli?

Je Chalamila hakuwepo wakati msiba wa Magufuli na hakusikia Sababu zilizosababisha Umauti umfikie JPM?

Je nini dhamira ya Chalamila kusema kauli hiyo?

Chalamila kusema watu Waende na Mabango yenye jumbe zozote hata za MATUSI, alikuwa anajaribu Kueleza Uhuru wa namna gani?

Chalamila akiwa Mbeya aliwahi kusema hataki Mabango ya Aina yoyote yenye jumbe za hovyo, je nini kimebadilika alipofika Mwanza?

Nilishawahi kusema, Wale wote waliokuwa wakisapuza na kuhamasisha JPM aongezewe muda wa kuongoza wanapaswa waondolewe katika nafasi walizonazo. Na Kama ni wabunge mwaka 2025 wasirudi bungeni.

Bahati nzuri wanafahamika, na wanajifahamu. Hatuwezi kuwa na taifa la viongozi wasioweza kutumia akili zao vizuri.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa MOROGORO

View attachment 1816057
Kuna swali moja umeshindwa kujiuliza kuwa huyu ni mkuu wa mkoa na ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Mkoa. Mchukue yeye na kila kitu kuhusu yeye kama upumbavu Ila mbakizie tu hiyo nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa na itafakari kauli yake chini ya nafasi hiyo.
 
Unajua anamuda gani tangu afike Mwanza, na tangu aanze kazi??

Kuwa mwenyekiti wa usalama Mkoa haimaanishi Kwa muda mfupi unaweza pata Data za watu wengi katika Mkoa wako.

Kusema watu Wanakinyongo ni kuzua maswali Tata Kwa wakubwa wanaokusikiliza Mkuu
 
Back
Top Bottom