Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema Chadema ilikurupuka na kudandia hoja ya Katiba mpya ya nchi bila kuzingatia maslahi ya Watanzania na kuonya kuwa mchakato wa kuunda Katiba unaweza kushindwa kama utafanywa kwa lengo la kukidhi matakwa ya watu wachache wanaoshinikizwa na wageni.
Akizungumza kwa simu jana, Mtikila alisema si viongozi wa Chadema wenye dhamira ya dhati ya uundaji wa Katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania, kwa kuwa wanataka Katiba iundwe, kwa maslahi binafsi kwa lengo la kuendeleza zama za ukoloni.
Mimi nilipojaribu kuzungumzia Katiba mpya na haja ya kuwa na Serikali tatu, watu waliniona kichaa, jambo ambalo lilisababisha kampeni ya kutaka Katiba kuwa ngumu na isiyo na mafanikio sasa watu hao hao wanataka Katiba mpya kwa maslahi yao, alisema.
Hata hivyo Mtikila alimwomba Rais Kikwete, asisahau kumjumuisha kwenye Tume atakayoiunda kwa kuzingatia kuwa ametumia muda mwingi kudai Katiba mpya ya nchi akiwa na dhamira ya dhati.
niliposoma muanzishaji wa huu uzi na kugundua kuwa ni wewe nilijua tu contents zitakuwa ni crap!!!
Anyway heri Chadema wanaodai Katiba kwa maslahi ya Tanzania kuliko yeye (Mtikila) aliyekuwa anadai katiba kwa kutaka umaarufu.