Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

kama sikosea huyo ni jaji wa tatu kwenye hii kesi.... na kila Jaji akija malalamiko ni yaleyale... sasa muafaka ni nini?.....wafuasi wetu uelekeo upi wafuate..., tunaendeleaje kufuatilia kesi na kusubiri matokeo yake ilihali tunaamini jaji yupo kimkakati.... Je tutasemaje mwishoni jaji huyu akimuachia mtu wetu?...
 
Nadhani ameshangazwa na umakini wa shahidi mshitakiwa. Kama shahidi mashitakiwa kaamua kusema ukweli anaoujua yeye, ni lazima wenye hila wajiulize kwanini yuko na mtiririko huo!

Kinachoshangaza kwa sisi maamuma wa sheria ni kama kuna ushahidi usiokuwa na mashaka kuwa mashitaka yatathibishwa - kina haja gani ya mshitaki kuweka pingamizi la kutaka mshitakiwa asijieleze?

Ajabu zaidi sababu wanazotumia kupinga upatikanaji wa document ya shahidi wa mashitaka (mpaka ikapelekea kuhoji kama mahakama imewasiliana na mshitaki kinyume cha taratibu) ndio wanazotumumia kuhoji barua anayotaka kuwasilishwa imemfikiaje mahabusu asiyekuwa huru!! Wanasisitiza hata kuhusu chain of custody ni shida, jambo ambalo hawakuonesha ni shida upande wao.

Leo wanasema Kibatala ni wakili wa mshitakiwa wa nne (Mbowe) hivo hakupaswa kuandika barua. Anasahau mawakili hawa hawajiwakilishi bali kampuni zao kama wao wasiviwakilisha isipokuwa serikali! Wanasahau hawajapinga Kibatala kuhoji mashahidi wao ambao walikuwa wanatoa ushahidi kuhusu walivowakata washitakiwa 1-2 na wala sio hata 3.

Mawakili wa serikali wameshindwa hata kutambua kuwa hata wao hawana mawakili dhidi ya mshitakiwa mmoja mmoja. Wamesahau washitakiwa wote wako katika kesi moja 16/2020 na wote wanashitakiwa kwa makosa yanayofanana isipokuwa mmoja kuhusu silaha na risasa!!
 
Huyu anatakiwa kupimwa akili, sidhni kama ana akili timamu. Hivi pale kizimbani shahidi anapelekewa hayo mijibu ya maswali na nani ambaye watu wasimwone. Au ni mizimu yake huyo jaji, ambayo yeye pekee yake ana uwezo wa kuiona imekaa na shahidi kizimbani?

Mawakili, washaurini washtakiwa wamkatae jaji kwa vile wana mashaka kama ana akili timamu.
 
Mna visingizio sana tulieni dawa iwaingie maana mlitamba sana mama anaupiga mwingi.

Mkome kabisa tabia ya kuingilia mahakama.
Hivi wewe mkuu huna hata aibu wakati mwingine kukurupuka kujibu mada ambazo aidha hujaelewa content ama unajitoa tu ufahamu. Wakati mwingine ushabiki weka pembeni ama kaa kimya kama huna chakuchangia.

Mbona wengine huwa tunajizuia kukaa kimya kama hatujaelewa mada ama vinginevyo.
 
Nadhani ameshangazwa na umakini wa shahidi mshitakiwa. Kama shahidi mashitakiwa kaamua kusema ukweli anaoujua yeye, ni lazima wenye hila wajiulize kwanini yuko na mtiririko huo...
Nilijua tu, kwenye cross examination mawakili wa serikali lazima waonekane kituko, hawana namna yoyote ya kumuondoa shahidi kwenye reli vinginevyo wakizidi kumuuliza maswali yasiyoeleweka ndio shahidi atazidi kufunguka wazidi kuvuliwa nguo na waliowatuma.

Wanachofanya sasa ni kutafuta vitu vya nje ya ushahidi unaotolewa na mtuhumiwa ndio wanaviwekea doubt ambazo nazo kimsingi hazipo, shahidi aliyeteswa na askari akanyimwa chakula, huo ushirikiano angepewa na nani kituoni alipokuwa ameshikiliwa?
 
Simply jaji haamini shahidi anachoongea, yani kwa maana nyingine jaji kaamua kuweka "objection" kuwasaidia mawakili wa serikali, hii kesi iishe tu, mahakama ya rufaa ndio kimbilio lililobaki
Mimi sidhani kwamba haamini, ninadhani kuwa shahidi katoa maelezo mazuri na kwa ufasaha hadi jaji akahisi kuwa anafundishwa majibu, inshort jaji alitamani Ling'wenya avurunde, ndio maana baada ya kuona majibu ni mazuri akaweka pingamizi.
 
Ajabu zaidi sababu wanazotumia kupinga upatikanaji wa document ya shahidi wa mashitaka (mpaka ikapelekea kuhoji kama mahakama imewasiliana na mshitaki kinyume cha taratibu) ndio wanazotumumia kuhoji barua anayotaka kuwasilishwa imemfikiaje mahabusu asiyekuwa huru!! Wanasisitiza hata kuhusu chain of custody ni shida, jambo ambalo hawakuonesha ni shida upande wao.
hili la bwn Shahidi kuomba hizo documents ni pigo la kustukiza ambalo hakujipanga nalo ndio maana Wakili wa serikali amaamua kutoa hoja kwa maelezo marefu kupoteza muda halafu mwisho anaomba HAIRISHO😄 ili waende kujipanga na kuskilizia maagizo toka muhimili uliojichimbia kwenye mihimili mingine utoe maelekezo kwa jaji akubali pingamizi.

Hii imenionyesha namna gani mawakili wa utetezi walivyo smart na kuwa mbele ya muda 😄😄 ngoja tuongeze popcorns zaidi tuendelee kuangalia mwisho unakuaje
 
Wadau wengi sana wamejitokeza kuhoji uadilifu wa Jaji anayeendesha kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu , kauli aliyoitoa Mahakamani iliyojaa uongo ya Kwamba Shahidi aliyekuwa anahojiwa na Mawakili wa Utetezi Mbele yake na mbele ya umati wa watu , komando Ling'wenya huenda alipewa majibu ya maswali aliyokuwa anaulizwa , imeleta Taharuki kubwa na imethibitisha mashaka ya siku nyingi kwamba huenda Jaji Tiganga yuko upande wa Jamhuri .
Erythrocyte kwa ushahidi huu kwanini huyu shetani Mbowe asikatae? Hii ni wazi kuwa kwa vyovyote vile atampendelea. Mkataeni tujue moja.
 
kama sikosea huyo ni jaji wa tatu kwenye hii kesi.... na kila Jaji akija malalamiko ni yaleyale... sasa muafaka ni nini?.....wafuasi wetu uelekeo upi wafuate..., tunaendeleaje kufuatilia kesi na kusubiri matokeo yake ilihali tunaamini jaji yupo kimkakati.... Je tutasemaje mwishoni jaji huyu akimuachia mtu wetu?...
Mkuu shida iliyojitokeza ni vema ikazungumzwa hadharani.Hivi ni sahihi alichokisema Jaji wakati jop la mawakili wa Jamhuri wamejaa tele vipi wasione hadi aone Jaji?

Kuna mambo kiukweli yanafikirisha sana ukiacha ushabiki wa kisiasa pembeni.
 
hili la bwn Shahidi kuomba hizo documents ni pigo la kustukiza ambalo hakujipanga nalo ndio maana Wakili wa serikali amaamua kutoa hoja kwa maelezo marefu kupoteza muda halafu mwisho anaomba HAIRISHO😄 ili waende kujipanga na kuskilizia maagizo toka muhimili uliojichimbia kwenye mihimili mingine utoe maelekezo kwa jaji akubali pingamizi
Hii imenionyesha namna gani mawakili wa utetezi walivyo smart na kuwa mbele ya muda 😄😄 ngoja tuongeze popcorns zaidi tuendelee kuangalia mwisho unakuaje
Hivi ni barua gan please, I have lost the truck
 
Mimi sidhani kwamba haamini, ninadhani kuwa shahidi katoa maelezo mazuri na kwa ufasaha hadi jaji akahisi kuwa anafundishwa majibu, inshort jaji alitamani Ling'wenya avurunde, ndio maana baada ya kuona majibu ni mazuri akaweka pingamizi.
Sasa hilo pingamizi aliloweka ndio atakwenda kulitolea maamuzi kwenye hukumu, Lin'gwenya ataadhibiwa kwa kusema kwake ukweli.
 
Sasa hilo pingamizi aliloweka ndio atakwenda kulitolea maamuzi kwenye hukumu, Lin'gwenya ataadhibiwa kwa kusema kwake ukweli.
Sijui kesho nini kitajitokeza inaonesha tunapoelekea ni patamu sana!
 
Ivi walalamikaji siwalikuwepo live wakati shahidi anatoa ushahidi wake, imekuwaje wasione kitendo cha shahidi kuelekezwa jinsi ya kutoa ushahidiwake.

Mbona akina kibatala waliibua wenyewe ishu ya shahidi mlalamikaji kuwa na note book kizimbani.
Nimeshangaa kidogo ila wakili wa washtakiwa alihendo ishu professionally sana,kwa kumuambia shahidi, ukiwa unajibu muangalie jaji usoni ilikumtoa wasiwasi.
😀😀😀
 
Back
Top Bottom