Kauli ya Diamond katika mtazamo chanya

Limpunga linaweka picha ya Traore halafu lenyewe linacheka cheka ovyo.
Kwani brother huwezi ku focus? Kwamba emoj tu zimekutoa relini. Jadili hoja zangu. Ukikosa focus ni rahisi sana mtu kuchezea akili yako. Na hii huwa inatumika sana kwenye manipulation. Focus
 
Kwani mmeanza kulalamika leo? Malalamiko yenu yalishawahi kubadilisha chochote? Hoja yangu ni kwamba " Kwa Mtanzania kulalamika ni tabia" , sehemu ya kutenda nyinyi ni kulalamika tu. Brother malalamiko hayabadilishi chochote. Mnalalamikia kila kitu.
Sasa watu wasifie kipi katika utawala huu wa CCM uliojaa ufisadi, mauaji na uhujumu wa democracy
 
Shida ya nchi yetu kuna baadhi ya watu wanahisi ukiondoa wana ccm basi raia wote wanaobaki ni chadema na vyama vingine vya upinzani wanasau kwamba kuna watu ni watanzania tu

Nyinyi wenye vyama mnafikiria juu ya miaka ya uchaguzi mtashindaje uchaguzi lakini sisi watanzania tunapoona mali za umma zinamilikiwa na watu wachache kiharamu basi tunaumia na kuwaza je watoto wetu huko 2050 watakuta nini tukiwa na ubinafsi namna hii??

Si kila anayelalamika ni kwamba hawezi kujimudu hapana wengine wana maisha yao tu bali wanawaza juu ya wengine

Ujue kuna baadhi ya watu hata mwalimu nyerere pale muhimbili angeitoa hospital angejenga apartment za wanae eneo lote lile wangemsifia .
 
Mnajiringanisha na watu wenye uthubutu!!! Hao hawaishi kulalamika tu, wanafanya, nyinyi je? Malalamikia vitu ambavyo hamuwezi kuvibadilisha
Roma haikujengwa siku moja
Watu wetu wengi hawaoni umuhimu kwa sababu ya elimu tu

Habari njema ni kwamba ccm bado hawajaamka pia
Tanzania ya mkapa siyo ya leo kwa upande wa wananchi

Alivyofariki Magufuli walijaribu kuirudisha Tanzania ya Kikwete lakini walishindwa watanzania walishakuwa wamebadilika

GenZ watoto ambao hawasikii la kuambiwa bado hawajajua siasa inaathiri vipi maisha au hawaja na experience ya chaguzi wakachagua mtu wao na akaletewa mazonge

Kifo cha ccm ni pale ambapo majukwaa ya siasa yatakuwa wametawala kizazi cha 2000 kuja huku
hicho kizazi kikijitambua tu ccm tunaisukuma kama mlevi hawana mbinu yoyote
 
Ivi mkuu nikuulize,hata wewe unaelewa ulichoandika kweli ukirudia kusoma tena??
Yani embu soma kwa utulivu ulichoandika mkuu..!
 
Huu ni mtazamo HASI. Nchi yoyote duniani ni lazima wananchi waiwajibishe serikali muda wote. Nimeishi baadhi ya nchi zilizoendelea lakini malalamiko na uwajibikaji ni mtindo wa maisha ya kila siku. Tatizo kwetu ni kwamba viongozi hawataki kukosolewa. Na huyo Diamond hana akili kwa sababu yuko hapo alipo kwa sababu ya wananchi. Leo hii wanaweza kumporomosha kwa sababu anadhani Samia ndiye kampa mafanikio.
 
Unadhani kulalamika tu inatosha? Malalamiko yetu yanabadili chochote?
 
Mfano wa Roma hauusiani na Tanzania mkuu Nchi ambayo mali zake zinateketea bure bila kuwapa faida Wananchi wake mwezi wa Kumi na moja inaanza kodi ya Ukimwi kwenye magari huku dhahabu,Tanzanite hazichangii kitu inaingia akilini hapo..
 
Kwani mmeanza kulalamika leo? Malalamiko yenu yalishawahi kubadilisha chochote? Hoja yangu ni kwamba " Kwa Mtanzania kulalamika ni tabia" , sehemu ya kutenda nyinyi ni kulalamika tu. Brother malalamiko hayabadilishi chochote. Mnalalamikia kila kitu.
Malalamiko ni kila nchi duniani unless kama haujawahi kuishi nchi nyingine tofauti na TZ kulijua hilo, stupidly unasema malalamiko hayajawahi kubadidilisha kitu unadhani serikali inavyojibaraguza kujaribu kuonyesha kwamba kuna vitu wameweza kufanya si nguvu ya wanaolalamika?
Wizi, ufisadi, utekaji, uuaji na nepotism vitalalamikiwa daima kwa kadri itakavyokuwa ikiwezekana. Hapo ni no retreat no surrender, whistleblowing always.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…