Mnaambiwa mwache kulalamika mfanye kazi malalamika tena😀, mbona nyie watu hamweleweki, Kila awamu nyie ni kulalamika tu.
Tukiachana na awamu ya Nyerere na Mwinyi ambayo sina kumbukumbu sahihi, awamu ya mkapa mmelalamika, awamu ya Kikwete mmelalamika, awamu ya Magufuli ndiyo kabisa🤣🤣, mlimwita kila aina ya majina baba yule. Aliwapigania kwa kila namna, wanaopiganiwa sasa😀😀. Mwisho wa siku akajifia zake(Nasikia kuna watu walifanya sherehe🤣). Ila kabla hajaondoka akawaachia neno "mtanikumbuka".
Then mama akaingia kazini, cha kushangaza hata mwaka haukupita mkaanza tena kulalamika🤣🤣, mara mama anakopa sana, mara Abdul kafanyaje. Hata hamjui mnataka nini.
Fanyeni kazi.
Hata kama mpate rais mzalendo kiasi gani, tabia ya kulalamika hamtaacha.
Na inawezekana kuwa ni jambo la hatari kuwa kiongozi mzalendo kwenye nchi ambayo wananchi hawaelewi wanataka nini? Akitokea mtu au kikundi cha watu kikawamanipulate, dakika hiyohiyo wanakugeuka.
Wenzenu wakipata rais mzalendo wako tayari kufa kwa ajili yake. Wakati nyinyi mnamkebehi na kumlalamikia. Kwa kifupi kujifanya mtetezi wa Mtanzania wa kizazi hiki ni kujitia matatizoni (Mifano mnayo).
KWA NINI MPO HIVI?
1. Watanzania wengi hawana fikra tunduizi (Critical thinking), huwa wanalipuka tu.
2. Uwoga na Kujipendekeza hii tabia mnayo sana tu. Mnasifia hata pasipotakiwa kusifiwa, mnawa manipulate hata vingozi wenu wanashindwa kujua wapi wako sahihi wapi hawako sahihi.
3. Tabia ya kuongea bila kufanya utafiti.
4. Elimu isiyoendana na mahitaji ( ni ngumu kutofautisha msomi na asiye msomi).
5. Malezi - uaminifu, ukweli, uwazi, usawa na uzalendo nitabia, na tabia inatengenezewa misingi tangu ukiwa mdogo. Tujiulize kama watoto wetu tunawafundisha haya tangu wakiwa wadogo.
MATOKEO YAKE SASA😀
1. Tunazalisha kizazi cha watu wanaojipendekeza muda wote😀 aka machawa( taaluma mpya hii)
2. Kizazi cha watu wanaolalamika muda wote.
3. Viongozi ambao hawajui wanataka nini. Nao wanalalamika😀
BADILIKENI