Kauli ya Chagonja juu ya Nassari

Kauli ya Chagonja juu ya Nassari

Luthar

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
519
Reaction score
105
Hapa nilikuwa nasikiliza radio TRIPLE A FM asubuhi Chagonja kaulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu kujeruliwa kwa mh. Nassari Chagonja akajibu hivi. Huyo Nassari alipigwa kwasababu yeye alienda kufanya nini huko na siyo kwao. Swali langu Lowassa kule ni kwao pia naye si ni mmeru iweje leo watu tunaongelea swala na makabila? Hawa viongozi watatumaliza Mungu tuepushe na hili linalo likumba taifa ila Tanzania ya leo siyo ile ya zamani tunaelewa tulipo toka na tulipo na tunapoenda
 
....naanza kuhisi tunaviongozi misukule,inchi inahitaji maombi.Sijui mipango gani ya maendeleo itapangwa na mtu mwenye kauli kama hizi...
 
Viongozi wengi wa Tanzania hawanaa weredi na utashi public relation!
 
huyu mzee ni mbumbu,anaropoka tu,haelewi chochote,ila watanzania tuliyataka wenyewe.
 
Kuna haja hawa viongozi waende kozi kujifunza public speaking na weledi.
 
Ni kweli amesema hivyo? Kama kweli basi nimeamini sasa kuwa kuna watu na viatu.Na hiki ni kiatu tena ni malapa ya public toilet.
 
Hakujua kama anasikika ndiyo maana akaamua kutapika ili kujipa ujiko
 
Duh!! ... huyo ndiyo mpelelezi mkuu au? Mbona kama mchemshaji?

Yani changoja unatumia nguvu kubwa sana kujibu hoja nyepesi... na kwa alivyo na cheo chake haviendani kabisa, ila tumuache kwani

(Tumeumbwa kwa mavumbi na tutarudi wote mavumbini)
 
mh.. hii kauli inamashaka ikiwa ameitoa...

Jana taarifa ya habari ya channel 10 nilimsikia akisema kwamba kuna nchi zimekataa kutoa ushirikiano kwa ajili ya kuwapata walipuaji wa mabomu Arusha....

Kwa kweli nilishindwa kujua sababu ya nchi hizo kufanya hivyo na ni nchi gani zilizotoa statement hiyo....But yeye akasema wanauwezo wa kuwatafuta watuhumiwa popote pale walipo...nilishindwa kumwelewa pia.
 
Hapa nilikuwa nasikiliza radio TRIPLE A FM asubuhi chagonja kaulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu kujeruliwa kwa nassari Chagonja akajibu hivi. Huyo nasari alipigwa kwasababu yeye alienda kufanya nini huko na siyo kwao. Swali langu lowasa kule ni kao pia naye si ni mmeru iweje leo watu tunaongelea swala na makabila? Hawa viongozi watatumaliza mungu tuepushe na hili linalo likumba taifa ila tanzania ya leo siyo ile ya zamani tunaelewa tulipo toka na tulipo na tunapoenda

Chagonja ferler
 
Nachelea kuamini kuwa Maneno ya kipuuz kama haya yanaweza kutolewa na kiongozi wa ngazi yake. Kama ni kweli, basi Watanzania tuna tatizo kubwa kuliko tunalolifahamu.
 
Back
Top Bottom