Kauli mbiu ya Lowassa kugombea ubunge 2010

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
105
Wanajamvi nimeitafakari kauli mbiu ya MH Lowassa kama inavyoonekanaa katika mabango yake ya kampeni huko Monduli na Kusomeka: Tulihuzunika pamoja....na tutashinda pamoja.

Je kwa hisia za kawaida mtu huyu ana machungu fulani moyoni mwake na kupitia wapiga kura wake pia anawashirikisha katika kujikomboa kwenye upweke huo..

Natumai EL ni mwanasiasa mjanja na huenda ana mikakati ya kutumia ajali yake kisiasa kurejeaa kwa kishindo katika uongozii wa juu hapa nchini..

Tujadili kauli mbiu yake..
 
Kauli mbiu yake ingefaa kuwa " NILIFISADI PEKE YANGU LAKINI NILIWAFEDHEHESHA NA NYIE"
 
Kwani alifanya kosa lipi lisilosameheka jamaniukweli ni kwamba mbali na TETESI za ufisadi juu yake mimi sijaona mtu mchapakazi wa EL,Kama yupo mtaje
 
Kwani alifanya kosa lipi lisilosameheka jamaniukweli ni kwamba mbali na TETESI za ufisadi juu yake mimi sijaona mtu mchapakazi wa EL,Kama yupo mtaje

Mchapa kazi kwelikweli, alihakikisha kila siku tanesco wanailipa richmond 135,000,000.00 bila ya kuzalisha umeme.
 
Kwani alifanya kosa lipi lisilosameheka jamaniukweli ni kwamba mbali na TETESI za ufisadi juu yake mimi sijaona mtu mchapakazi wa EL,Kama yupo mtaje

Kosa alilofanya na katu hatosamehewa ni kutumujimu sisi wananchi kwa manufaa yake na mafisadi wenzie pesa waliokuwa wanalipa tanesco kwa siku kwenda richimonduli ingeweza kununua madawa mahospitalini kukawa hakuna sida ya madawa, vitanda vingeongezwa mahospitalini kusinge kuwa na uhaba wa vitanda hali kadhalika mashuleni kungekuwa na vitabu vyote na madawati, barabara zingeboreshwa na huduma nyingi za jamii, leo hii unaona shida wanazowapa watanzania ambao ni maskini kwa kula mlo mmoja kwa siku tena ka chini ya dola moja hata ajitakase vipi wanaichi bado wanamachungu nae!!! :mad2::mad2::mad2:
 
Wanajamvi nimeitafakari kauli mbiu ya MH Lowassa kama inavyoonekanaa katika mabango yake ya kampeni huko Monduli na Kusomeka: Tulihuzunika pamoja....na tutashinda pamoja.

Je kwa hisia za kawaida mtu huyu ana machungu fulani moyoni mwake na kupitia wapiga kura wake pia anawashirikisha katika kujikomboa kwenye upweke huo..

Natumai EL ni mwanasiasa mjanja na huenda ana mikakati ya kutumia ajali yake kisiasa kurejeaa kwa kishindo katika uongozii wa juu hapa nchini..

Tujadili kauli mbiu yake..

...There is a wish I have to grant, na ni huu Uwaziri Mkuu... Mpaka leo haamini angeweza kujitega, kujipiga mwereka na kuanguka mwenyewe! Akikumbuka ving'ora na kufukuza wafanyakazi wa umma akiwa amesimama kwenye jukwaa la siasa, hana hamu
 
Mkuu capacity charge ilikuwa 152,000,000 daily wazlishe wasizalishe.
Huyo ndo Richard Monduli mzee wa kuuma na kupuliza
 
mie watanzania wengine siwaeleqi kabisa

kuwatumikia kama huna moyo wa chuma basi inakua kazi

pamoja na mapungufu yake huyu mkuu, amejitahidi sana katika kuleta UFANISI SERIKALINI, pia kusimamia kwa dhati maendeleo ya taifa lake

suala la ardhi linajulikana vipi alilisimamia, suala la uwajibikaji serikalini vipi alilishughulikia, suali la elimu vp alilishughulikia, suali la maji hadi sasa ndugu zetu kule wanafaidi vp alilishughulikia

kwa kweli kuna mengi ambayo ameyafanya na kuwatumikia wananchi wenzake

ila binaadamu wengine wanaendeshwa na hisia za kichama zaidi kuliko utaifa

mimi nnamkubali sana, ni miongoni mw ma PM waliothubutu, ingawa maamuzi yake mengine sasa yanamgharimu
 
Lowasa ni kichwa nyie.
Hiyo kauli mbiu ni mwafaka sana, kilaza asingeweza kuitunga hiyo.
 
Kwani alifanya kosa lipi lisilosameheka jamaniukweli ni kwamba mbali na TETESI za ufisadi juu yake mimi sijaona mtu mchapakazi wa EL,Kama yupo mtaje

Rutunga na mdomo wako bana!!
Kama ni mchapa kazi na msafi kwa nini aliachia ngazi!!!?
 
Kwa nchi inayofuata utawala bora, huyu muungwana alitakiwa awe amefungwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali. Hayo machache mnayoona ameyafanya kwa ufanisi ilikuwa ni janja yake ya kutaka kula na kupuliza. Hata hivyo kuwa hadi leo ni mtu huru ukilinganisha na utajiri alionao, sielewi kwanini asitulie nyumbani akalea wajukuu. Na kama hana, asaidie hata wa majirani:eyeroll2:
 
kwani alifanya kosa lipi lisilosameheka jamaniukweli ni kwamba mbali na tetesi za ufisadi juu yake mimi sijaona mtu mchapakazi wa el,kama yupo mtaje

fisadi ni fisadi. Kuna faida gani ya kuiba mabilioni kupitia richmondi na bado tz mgao wa umeme ukaendelea kama kawaida. Hivi unaweza kumsifu jambazi anayeibia wengine na kuwaacha taabani na kwenda kula na familia yake kwamba ni baba mzuri,huku wewe uliyeibiwa ukifa na njaa na familia yako. Poor tanzanians, lazy thinkers and cowards will stand for lowasa. The patriots will stand and say no to him forever
 
Kwa nchi inayofuata utawala bora, huyu muungwana alitakiwa awe amefungwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali. Hayo machache mnayoona ameyafanya kwa ufanisi ilikuwa ni janja yake ya kutaka kula na kupuliza. Hata hivyo kuwa hadi leo ni mtu huru ukilinganisha na utajiri alionao, sielewi kwanini asitulie nyumbani akalea wajukuu. Na kama hana, asaidie hata wa majirani:eyeroll2:

hizi ni chuki binafsi, na choyo cha watanzania

mtu akiwa na pesa basi fisadi

ukweli utabaki wazi kuwa ni mtu alijitoa kulitumikia taifa lake na watu wake

ndio maana watu wake wanampenda na atashinda kwa kishindo
 
Hakika wewe ni miongoni mwa wale Watanzania waliolala fofofo.
 
EL alisema alijiuzuru uwaziri mkuu,Kiranja Mkuu akamkubalia,sasa kama ni kichwa inatusaidia nini sasa? Mawaziri wakuu tumeona wengi toka Mwalimu Nyerere, Kawawa,Sokoine Msuya,Salim, Warioba,Samuel,Mtoto wa mkulima.Sasa anagangania nini? one mistake one goal.
 
Lowasa jeuri yake itaisha pale mtu ambaye anadai 'hawakukutana naye barabarani' atakapolazimika kutoka 'white house' mwaka huu na kuingia sura nyingine atakayekiita 'kijiko,' 'kijiko,' 'kisu,' 'kisu,' nk!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom