Elections 2010 Kauli mbiu mpya ya JK 2010

37291_1474883801206_1507034707_31191570_1756386_n.jpg

mwananchi akiuguza nduguze wagonjwa katika Zahanati kijijini Kisaki, Bwakila, Morogoro



37291_1474883921209_1507034707_31191571_7753096_n.jpg


wagonjwa wakiwa wamelazwa katika Zahanati kijijini Kisaki, Bwakila, Morogoro

Hapa mahali very resourceful........ardhi nzuri........madini kibao...selous next door...TAZARI inapita.....lakini umasikini kibao....JK hajawahi kufika hapa vinginevyo hizo 'samadari' zingegeuzwa kuni(LoL)
 
37291_1474883801206_1507034707_31191570_1756386_n.jpg

mwananchi akiuguza nduguze wagonjwa katika Zahanati kijijini Kisaki, Bwakila, Morogoro



37291_1474883921209_1507034707_31191571_7753096_n.jpg


wagonjwa wakiwa wamelazwa katika Zahanati kijijini Kisaki, Bwakila, Morogoro

Babu, amini nachokwambia mimi, leo hii tukienda wote Kisaki kwa huyu huyu mama utamwona kavaa kagha za mwaka 2005 za " CCM Ushindi" tena mpiga kampeni no 1 uchaguzi huu, ameshasahau yote haya. ushindi wa CCM unachangiwa zaidi na wananchi kutoelewa elimu ya uraia.

Safari ni ndefu mno lakini nina imani kuna siku itafika wananchi (kama huyu mama) watashituka na kusema "yatosha"
 
haoni hata aibu na makauli mbinu yaliyojaa maneno ya uongo
Wana JF,

Katika pitapita yangu leo nimeweza kugudua kauli mbiu ya Mh Jakaya atakayo tumia katika uchaguzi mkuu mwaka huu kama ifuatayo:

KASI ZAIDI
NGUVU ZAIDI
ARI ZAIDI
TULIAHIDI TUMETEKELEZA!


Hii ndio kauli mbiu itakayotumika mwaka huu ktk uchaguzi
 
haoni hata aibu na makauli mbinu yaliyojaa maneno ya uongo

Bujibuji - ni watanzania wangapi wanajua kwamba haya maneno ni kauli mbiu za kitapeli? hiyo 75% ya watanzania ambao wanaitwa Bendera fuata upepo cha kusikitisha na wanazuoni wamo humo humo - kazi kweli kweli.

Sasa hivi utasikia maandamano nchi nzima kusupport uamuzi wake wa kuchukua form.
 
JK aja na Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi
4659014.jpg

Tuesday, June 22, 2010 10:33 AM
RAIS Jakaya Kikwete jana wakati alipokwenda kuchukua fomu ya kuwania urais alikuja na kauli mbiu mpya ya kutetea nafasi hiyo iliyosema Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi hii ni katika kuboresha kauli mbiu ilioyopita ktka kutimiza ahadi zake kwa w Rais Kikwete alisema pindi atakapochukua kiti hicho ataboresha zaidi na ameshaweka vipaumbele kumi muhimu ikiwemo kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Alisema vipaumbele vingine ni kuongeza jitihada na mipango zaidi ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini zaidi ili waweze kushiriki na kunufaika na uchumi unaokua.

Vipaumbele vingine atahakikisha serikali ijayo itaongeza jitihada za kupanua wigo na kuboresha huduma muhimu za kijamii hasa afya na maji mbazo zimeonekana ni kero kubwa kwa wananchi walio wengi.

Pia alisema atahakikisha huduma za umeme, miundombinu na mawasiliano zitaboreshwa zaidi.

Rais Kikwete aliyasema hayo mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisini ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Bw. Yusuf Makamba aliongozana na familia yake na wadhamini wake mjini Dodoma.

Pia Kikwete alitimiza na kulipia shilingi millioni moja kama ada ya kuchukulia fomu na kuonyesha wananchi risiti waliohudhuria hafla hiyo.
 
Ni kauli mbiu ya kipuuzi - ametudanganya vya kutosha. Najua atapata uraisi tena kutoka kwa watanzania waliolala, ila najua kura yangu ataikosa, najua pia kuikosa kura yangu hakutamzuia yeye kuwa raisi, bali wakati huo ukifika roho yangu itafarijika kwamba sikuridhika na sikushiriki yeye kuwa pale.
 
Wana JF,

Katika pitapita yangu leo nimeweza kugudua kauli mbiu ya Mh Jakaya atakayo tumia katika uchaguzi mkuu mwaka huu kama ifuatayo:

KASI ZAIDI
NGUVU ZAIDI
ARI ZAIDI
TULIAHIDI TUMETEKELEZA!


Hii ndio kauli mbiu itakayotumika mwaka huu ktk uchaguzi

Kweli duniani kuna watu. Mwe!
 
wagonjwa wakiwa wamelazwa katika Zahanati kijijini Kisaki said:
Bwakila, Morogoro[/B]/QUOTE]


...Kilichopo KATIKATI ya Miji miwili inayotumalizia hela ikishindana kuwa Mji Mkuu wa Tanzania!!! :mmph:
 
Sikumpata vizuri Mh.Prezidaa hivi amesema tuliahidi tumeteketeza au tumetelekeza au tumetekeleza.

Ni ukweli usiopingingika Maisha bora kwa Kila Mtanzania yamekwisha telekezwa na kuteketezwa.

Bora angesema fix zaidi,usanii zaidi tungemuelewa.
 
ameshaweka vipaumbele kumi muhimu ikiwemo kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

JK na mkakati ulishindwa kabal ya kuanza! eti ataongeza kasi ya kupambana na rushwa! ataongeza kasi ipi wakati hayo mapambano na rushwa hajayaanza? kasi huongezwa kwa kitu ulichokwisha anza fanya aache UONGO bana aaaaaaaa!
 
Wana JF,

Katika pitapita yangu leo nimeweza kugudua kauli mbiu ya Mh Jakaya atakayo tumia katika uchaguzi mkuu mwaka huu kama ifuatayo:

KASI ZAIDI
NGUVU ZAIDI
ARI ZAIDI
TULIAHIDI TUMETEKELEZA!

Hii ndio kauli mbiu itakayotumika mwaka huu ktk uchaguzi

Bila Aibu nashindwa kuamini ...
 
Ingawa hii ndiyo ina-make sense zaidi kuliko ile ya 2005:

Hebu angalia

2005
Ari
NGUvu
KAsi ..........Mpya...........................ANGUKA Mpya

2010
Ari
NGUvu
KAsi .........Zaidi...........................ANGUKA Zaidi


Nani anasema muungwana siyo msaniii? Bagamoyo ndiyo kuna chuo cha sanaa!!!!!
 
HEKAHEKA URAIS CCM 2010- Msibadili farasi katikati ya mto-JK


spacer.gif
Tuesday, 22 June 2010 05:18

*Achukua fomu, ataja vipaumbele 10
*Asema miaka mitano ilikuwa tanuru


Na John Daniel, Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete amefungua pazia la kinyang'anyiro cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) baada ya kuchukua fomu jana huku akilinganisha miaka mitano ya uongozi wake na kisa cha mpanda farasi anayevuka mto.

"Upo msemo kwamba kama unavuka mto ukiwa umepanda farasi sio busara kushuka na kubadili farasi katikati ya mto, hasa kama farasi huyo amehimili mawimbi.
Katika miaka mitano iliyopita, tumehimili mawimbi makubwa yaliyotishia umoja wa nchi yetu.


Tanzania yetu leo hii bado ni ile ile, nchi yenye amani na utulivu tunayoijua sote na ambayo dunia inaijua hivyo. Tumejifunza mengi na tumepikwa katika tanuru la moto na tumeiva kama chuma cha pua. Na tumefaulu mtihani na changamoto za uongozi wa Taifa letu. Na tumedhihirisha kwamba tunao uwezo wa kuivusha nchi yetu kuelekea kwenye neema," alisema Rais Kikwete.

Alitamba kuwa Serikali ya CCM bado ina uwezo mkubwa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita hivyo Watanzania wana kila sababu kuipa miaka mingine mitano ili kukamilisha mafanikio hayo.

Akizungumza na wana CCM pamoja na mamia ya wananchi waliojitokeza kumpokea Makao Makuu ya CCM mjini hapa jana, Rais Kikwete, alisema licha ya nchi kupitia kipindi kigumu katika utawala wake, amefanikiwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho na kuboresha maisha ya watanzania kwa kiasi na kuendesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Alisema pamoja na mambo mengine, kubwa lililomsukuma kuchukua fomu kuomba ateuliwe na CCM kwa awamu ya pili ni mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wake na kwamba haitapendeza CCM kuacha kumpa nafasi hiyo kuwa mgombea wake.
Alitaja mambo mengine yaliyomsukuma kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo kuwa ni pamoja na imani kubwa waliyo wananchi na chama chake juu yake pamoja na kujiamini kwake kwamba anao uwezo wa kuifikisha Tanzania kwenye neema.
Alitaja vipaumbele 10 vya Serikali yake iwapo atapewa ridhaa na CCM na Watanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba na kuweka wazi kwamba anaguswa na matatizo ya Watanzania hivyo amepania kumalizia mazuri aliyoanza yenye lengo la kuinua maisha yao.
“Safari ile (mwaka 2005) nilisema mkinichagua nitafanya kazi kwa Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi Mpya, matokeo yake tumeyaona safari hii nasema mkinichagua nitawatumikia Watanzania kwa Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi Zaidi katika dhamira yetu ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, kwa pamoja tuzidi kusonga mbele,”alisema Rais Kikwete na kuongeza;

“Mkinipa nafasi ya kuwa mgombea wa chama chetu na mara tutakapofanikiwa vipaumbele vya serikali ijayo vitasukumwa na misingi kumi ifuatayo:-
Kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na umoja, amani na usalama. Kujenga msingi wa uchumi wa kisiasa wa Taifa linalojitegemea kwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha zaidi mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda.
Kuongeza jitihada na mipango zaidi kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini ili waweze kushiriki na kunufaika na uchumi wetu unaokua.
Vilevile tutaweka mkazo katika kulitambua na kuliwezesha kwa namna yake kundi la wajasiria mali wa tabaka la kati ili waweze kushiriki katika uwekezaji mkubwa katika nchi yetu.
Kutumia fursa ya kijiografia ya nchi kuifanya lango kuu la biashara na usafirishaji kwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini na Kati hasa kwa kuimarisha ufanisi wa reli na bandari zetu.
Kuongeza jitihada za kuhakikisha Taifa linanufaika zaidi na rasilimali za asili za nchi yetu kuanzia madini, misitu, wanyamapori mhadi vituo mbalimbali vya utalii.
Kuweka mkazo sasaa kwenye kuboresha elimu ya msingi na sekondari,kupanua elimu ya ufundi na elimu ya huu hasa katika masomo ya sayansi.
Kuongeza jitihada za kupanua na kuboresha huduma muhimu za kijamii hasa huduma za afya na maji, huduma za kiuchumi hasa umeme, miundombinu ya usafirishaji na mawasiliano na huduma ya fedha.
Kuimarisha utawala bora, sheria, demokrasia, hasa kwa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa,matumizi mabaya ya madaraka, ubadhilifu, wa mali ya umma, na kuendelea kuviwezesha kirasilimali kitaasisi/kimuundo na kisheria vyombo vya kutoa na kusimamia haki
nchini.

Kuipa dola na vyombo vyake husika uwezo mkubwa zaidi wa kupanga mipango ya uchumi na kusimamia uchumi wa nchi wa nchi kwa ufanisi bila kuingilia sekta binafsi ili kulinda maslahi ya nchi yetu na watu wake.
Kulinda mafanikio tuliyapata katika nyanja zote tangu uhuru wan chi yetu ikiwemo katika kipindi ha miaka mitano iliyopita na kukamilisha yale tuliyoahidi mwaka 2005 ambayo kwa sababu moja au nyingine hatukuweza kuyakamilisha katika miaka mitano hii,”alisema Rais Kikwete.
Alitaja baadhi ya mafanikio makubwa ya utawala wake kuwa ni pamoja ongezeko la wanafunzi kuanzia elimu ya msingi, sekondari, vyuo, vyuo vikuu, miundombinu, maji safi na salama, uboreshaji wa sekta ya afya hususan mapambano dhidi ya malaria,Kifua Kiku (TB), UKIMWI pamoja na ajira.
“Tumetekeleza Ilani kwa umakini mkubwa na matokeo yake yanaonekana pande zote, takriban mambo yote tuliyoahidi tumeyatekeleza na pale ambapo yapo ambayo hatujatekeleza kwa kweli si mengi na ni kwa sababu za msingi, hata hivyo yale ambayo hatukujaliwa kutekeleza safari hii tutakamilisha tukipewa heshima ya kuliongoza Taifa letu katika awamu ijayo,”alisisitiza.
Tukio hilo la uchukuaji fomu kwa Rais Kikwete lilionekana kuteka shughuli mbalimbali mjini hapa ikiwemo Bunge ambapo takriban nusu ya wabunge wa CCM na idadi kubwa ya mawaziri.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete ameendelea kupokea michango kutoka kwa vikundi mbalimbali vya CCM na vile vya wananchi waliochangia gharama ya mafuta ya kuzungusha fomu mikoani ambapo zilipatikana zaidi ya sh. milioni 13.5.
Awali akimkaribisha Rais Kikwete kuzungumza na wananchi na wanaCCM waliofurika White House kushuhudia tukio Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yusuf Makamba, alieleza kuwa kuna kila dalili kiongozi huyo kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo mwaka huu.
“Mhe. aliyetangaza nia alikuwa Shibuda na ameshajitoa, sasa kuna dalili kwamba unaweza kuwa peke yako, Shibuda wewe mtu bwana! lakini usirudi nyuma maana muungwana ni vitendo, hata mke wako amesikia,” alisema Bw. Makamba.
Katibu huyo Mkuu alimwita Bw. Shibuda mbele ili kumpa mkono pamoja na Rais Kikwete hali hatua iliyoibua vifijo na nderemo .
Akizungumza na Majira Bw. Shibuda alisema kujitoa kwake mwaka huu katika kinyang'anyiro hicho ni kuonesha ukomavu wa uongozi.
“Subira hujenga ubora wa uongozi, mcheza mpira akikaa nje anasoma jinsi timu yake inavyocheza na akiingia anafunga goli, sijajitoa kugombea urais ila nimeondoa dhamira yangu kwa mwaka huu,”alisisitiza Bw. Shibuda.
Wagombea wote watakaochukua fomu hizo, watakiwa kuzirejesha Julai mosi mwaka huu.


 
Me naona kuwa kweli walahidi na ni kweli wametekeleza ila tatizo ni moja tu, kuwa walichoahidi sicho walichotekeleza na walichotekeleza sicho walichoahidi!

Lakini na'doubt moja kama alikuja na ari, kasi na nguvu mpya ikashindwa nani kamuongezea na kuwa zaidi?
 
tunaangushwa na walala hoi na watu wa vijijini, wanashau mapemaa kama kuku,akipewa tshirt hewala kesho anampigia kura
 
Back
Top Bottom