Kauli mbalimbali za wanaume wa shoka

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
49,777
2,000
WABABA TUNASEMA........

1. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo." *Napoleon_Bonaparte.*

2. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake." *George_Patton.*

3. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa." *John_Adams.*

4. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi." *Sun_Tzu.*

5. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda." *Harry_Browne.*

6. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso." *Adolf_Hitler.*

7. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea." *Friedrich_Nietzsche*

8. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka." *Confucus*

9. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo." *Albert_Einstein.*

10. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote." *Plato.*

11. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo." *Harry_Truman*

12. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili." *Benjamin_Franklin*

13. "Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria" *Lamar_Smith*

14. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa" *Doug_Larson*

15. "Siasa ni hatari kuliko vita. Kwenye vita mtu hufa mara moja tu, lakini kwenye siasa mtu hufa na kufufuka mara nyingi kadri iwezekanavyo" *WinstonChurchil*
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,285
2,000
Mbona hakuna kauli ya Mtemi Chenge?

Mzee wa kazi.

Lord Sauron

JF-Expert Member
May 4, 2017
224
250
"Mashujaa wanaonja kifo mara moja tu. Waoga hufa mara nyingi sana kabla ya kufikia kifo chao halisi. Kati ya vitu vinavyonishangaza ni wanadamu kuogopa kifo kwani kifo, kitu ambacho ni cha lazima huja muda wowote kwa jinsi kinavyotaka." William Shakespeare katika Julius Kaisari.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom