Kauli hizi za JK inatufundisha nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hizi za JK inatufundisha nini hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisoda2, Mar 24, 2011.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Hivi karibuni nimebahatika kuzisikia kauli za muungwana JK katika runinga akiwa kwenye sindimba zake za kutembelea wizara.
  kauli kama hizi:-
  1. kwani kuna wafanya kazi/watumishi hewa(UTUMISHI)
  2.Mnauza nyumba/kupangisha kwa bei kubwa (Nyumba na makazi- NHC)
  3.tuangalie katika kuwahamisha wavamizi wa hifadhi za bara bara,tusijikute bara bara imejengwa halafu ikakosa wa kumhudumia.

  hivi anapoongea kauli kama hii (red) ana halalisha ama anatueleza nini?
  Kwa kiongozi kama yeye kutwambia eti bara bara itakosa wa kumhudumia, basi sheri hizi zifutwe ama bara bara ya mlandizi chalinze isingejengwa kwani pembezoni hakuna watu wakuhudumiwa na hiyo bara bara.

  Kibaya zaidi ni style anayotumia kuinterrupt maelezo ya mhusika kana kwamba wapo kwenye kusutana(Mipasho ya mashangingi wa KKoo)
  Inaonyesha kichwa yake haiwezi kutunza kumbukumbu ili aje amuulize maswali hayo mwisho wa story.
   
 2. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Anataka kuwatuaminisha kuwa yeye ni mzuri ila anaangushwa na watendaji wake. Ndio maana kaamua kuwadhalilisha mawaziri wake kwa kuwapinga na kuwabwatukia mbele ya UMMA. Naamini anaridhika anapo sifiwa eti yeye ni mzuri ila watendaji wanamwangusha.

  Asicho jua JK ni kuwa kama yeye ni kocha timu ikifungwa yeye ndiye wakwanza kunyoshewa kidole.
  Tatizo lake anapenda kuwa One man show.
   
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Imefikia kipindi wengine tunaangalia tu!
  Sometimes anazungumza kama ameishi Marekani miaka sita mfululizo na hakuwa anatumia vyombo vyovyote vya habari. Ni kama kila kitu yeye hajui wakati baadhi ya utumbo ulipitishwa na Cabinet yeye akiwa Mwenyekiti. Utendaji mbovu bandarini unasababishwa na nini zaidi ya kampuni ya rafiki yake Karamagi iliyopewa mkataba mrefu hata kabla ule wa mwanzo haujamalizika?
  Watu wengine wanadhani JK anachukiwa kwa sababu za wivu lakini ukijaribu kuangalia utendaji kazi wa huyu jamaa utagundua hakuzaliwa wala kulelewa kuwa kiongozi. Kuna watu wanapata ufuasi kwa kuchekacheka mbele za watu na kulipa fadhila lakini uwezo wa kuongoza ni Negative. JK angeuza filamu nyingi sana kama angefanya shughuli kama za akina Kanumba na Ray. Anapendeza kuigiza.
  Siku moja nimebishana sana na watu waliodai alisoma BA. Economics pale Mlimani maana kwa anayofanya sijui kama anajua hata maana ya cost and benetit analysis. Jana nimemwona ktk TV akizungumzia kununuliwa meli mpya katika maziwa makuu.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimeshindwa kumwelewa siku za mwanzo nilitaka kuelewa kwamba amekuwa mkali kwa watendaji wake lakini ukifatilia kwa umakini ni usanii zaidi...
   
 5. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  ......ni sawa na mama anayekumbuka kumpa mtoto lishe nzuri siku ya Clinic, akiamini ya kuwa ataongezeka uzito..!
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  we kiatu kwenye red hapo, ni kipindi kipi kampuni ya karamagi iliongezewa mkataba? JK alikuwa rais. Tatizo lako unaongea huku ukitumia makalio kufikiria badala ya brain.
  Nyie mnaowalaumu Kikwete na Pinda, bila shaka hamna nyumba karibu na barabara. haiingii akilini sheria ibadilishwe 2007 halafu mimi nitu hapo tangia uhuru unibomolee tu bile fidia. come on.
   
 7. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Zinatufundisha Sanaa ya Utawala
   
 8. N

  Ntandalilo Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenifanya nicheke mkuu...................... !!!
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  kauli ya jana pia iliniacha hoi.
  Sumatra: "...Tunapata vikwazo sana kwani wamiliki wengi wa daladala ni askari polisi...."
  JK:"....Ahahahaha! ya leo kali...."
   
 10. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuwa na Rais ama CEO/GM ambaye ana deal na details kiasi hiki. This is a high leve management failure or weakness. Rais anatakiwa ku-deal with only high level strategic issues. Sasa issue kama hizo ni so small for his position hata waziri napo zaweza kuwa ndogo. Mimi sielewi Job description yake iko vipi, anatakiwa awe na mifumo inayofanya kazi ili kuweza kushughlikia issue hizo. Mfano hao Ghost workers, si jukumu lake kupata habari kwa katibu au mtu wa level ya chini, anatakiwa apate audit reports na kuziangalia from that angle na kama kuna issue ambayo itakuwa kubwa then ndo a- chip in otherwise waziri ndo anatakiwa adeal na hizo issue. Kama basi kaweka mfumo wa yeye ku-deal na kila kitu ndo maana hata hao mawaziri and people down him hawaoni haja ya ku-act.
   
 11. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sasa hapa ni kauli ya kucheka hiyo kwa mtu makini?
  badala ya kujiuliza wamepata wapi hizo hela za kumiliki hayo madaladala wakati mishahara yao haiwezi kuishawi taasisi yeyote ya kifedha kumpa mkopo wa kuweza kulimiliki hilo dala dala !
  anaishia kucheka.

  kweli kazi tunayo.
   
 12. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  wewe uliyejenga barabarani utueleze ikowapi tuje kuitumia sheria ya mwaka 34!!
   
 13. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Anataka awaaminishe wa Tz kuwa yeye ni mkali na yupo serious wakati uozo huo umeanza muda mrefu. hosp.ya mkoa moro kunajamaa zangu wanadai kupandishwa vyeo tangu 2006 hadi leo hawapandishwi wala nin. Jk huwezi jipendekeza leo tumekuchoka. Mawaziri kila cku mnakutana baraza la mawaziri kwanin uckemee toka huko. Mbona mwezio Mkapa hakuwahi kutembelea wizara lakin akiongea tu mambo yanatekelezwa, huna makucha na huwez kusimamia kile unachoamin. I hate to have a weak president like Jk. I dont know in history is there any country had weak president like Jk.
   
 14. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  ndg yangu ina maana ulikuwa humjui huyu au hujawah kuckia pumba zake? Me Nshazoea kuckia pumba zake hvyo huwa simsikiliz kwan najua huwa haongei mambo ya maana hata kidogo.
   
 15. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  mie naamini wewe ndio ambae hutumii akili yako vizuri badala yake u let ur emotion 2 think 4 u. All u think about is the potential personal loss/gain the same way mafisadi do. Magufuli anatekeleza sheria kwa uaminifu. Uji-nga wako na wengine walioivamia barabara ndio unatutatiza. Kabla hujaamua kujenga ni lazima kuwaendea watu wa ardhi ili kyjiridhisha.
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu ok uko sawa. Pia wajuzi wa mambo hatujawahi kuona kampuni ya karamagi bandarini. Karamagi akiongelewa kwenye TICTS wala hana power na ana 1/100 shares. Ila kwa kuwa kuna kitu kinaitwa siasa chafu,basi nami ntajitaidi kuaminishwa kuwa Karamagi ana kampuni inaitwa TICTS,japo yeye pale ni mpiga debe tu/kuwadi. Nikielekea kwa point yako ya mwisho,unataka kueleza umma kuwa Magufuli anakosea au? Ivi ulishawahi kumkuta magufuli amekaa chini ya mti anatunga sheria kinyemela au anatekeleza tu?! Usiongelee waliojenga kabla ya sheria,hao wanalipwa ila sisi tuliopuuza sheria kuna kitu kinaitwa "ignorance of law is not an execuse". Alichofanya Jk ni kuhairisha 'mazishi' ila msiba upo hata ikiwa miaka 10. Kuvunja ni lazma wala tusichenge ili kumfurahisha Ngwendu. Alichofanya jk ni staki unizidi umaarufu magufuli! Akisema wawape muda walau mpaka miaka 2/3 itakuwa ni lini iyo? Si mwaka 2014 mpaka 15 wakati ambao Jk atakuwa ameshapata kinua mgongo? Kwa ufupi hapa amemwambie magufuli akae posta,afike asign asubiri jion asign daftari la maudhurio kazini,asubiri mshahara ili japo isogee mpaka 2014 wastaafu wote nao waanze kumlaumu rais ajaye kwa kumweka waziri ambaye sasa atavunja rasmi. Kumbuka Anna Tibaijuka alitaka kuvunja pale Hananasif akiwa UN akapigwa mkwara! Kwa kweli Tz ni vioja ndugu. Usiku mwema Ngwendu.
   
Loading...