Mkuu wangu sidhani unalotaka linawezekana..Wala hatuwezi kuiga Marekani wala Ulaya kwa sababu hata wao wamekwisha mpitisha Obama bila challenge japokuwa watu wapo wanaoweza kum-challenge. Hata wao wanazo kanuni, huwezi kuendesha chama chochote bila kanuni, utapata wapi utiifu kanuni hata Mpira una kanuni zake na ndio maana refa anapiga kipenga na wasaidizi wake wakijua kanuni za mchezo..Mizengwe ipo mahala popote lakini kanuni huwezi kuziepuka hata kidogo hakuna mizengwe, mizengewe tunayo sisi tnaotaka kukiuka kanuni.
Ndio maana nimekuuliza wewe unajua Chadema wanatumia utaratibu gani? hutaki kuelezea isipokuwa tukasome katiba..Mkuu sii kila kitu kimeelezwa vizuri ndani ya katiba, sheria hazipo ndani ya katiba isipokuwa unazisoma sheria zenyewe kwa vifungu vyake kufahamu undani zaidi lakini hutakuta ktk katiba...Utaratibu wa Chadema sio perfect na kama wewe unaona mahala panatakiwa kubadilishwa ama kufanyiwa marekebisho nadhani huu ni ukumbi mzuri sana sote tukijadili swala hilo lakini sii kulalamika tu wakati unatuacha kizani wengine..
Binafsi, ningependa kuona mfumo wa uchaguzi nchini unaboresha na kanuni za vyama vyote zinakuwa sawa sawa kwa vyama vyote wanachama wake kuliko kila chama kinajitungia, lakini tunapozungumzia Uchaguzi nadhani bora sisi tutakuwa na mfumo wetu tofauti kabisa na ule wa Marekani ambao unategemea lobbiest na hivyo mgombea anaweza tu kupendekezwa kugombea kutokana na uwezo wake wa kukusanya fedha za kugombea. Hivyo kanuni ya FEDHA kuwa msingi wa mgombea sisi hatuiwezi na haiwezi kufanya kazi kwetu maana asilimia 90 ni maskini..
Mimi nadhani, kama tunaweza kuwapa nafasi wananchi wachague mgombea urais kwa kutumia kura za maoni kwanza kisha majina yale yakapendekezwa ktk mkutano mkuu kuwa ndio wagombea ambao wananchi wamewapitisha kwa hiari yao kutumia mfuko wa fedha za chama wagombee kuliko kila mwenye kutaka kugombea maana sisi maskini ni rahisi sana mwenye fedha kununua ushindi.. Tumeshindwa kukomesha Takrima na ikiwa chaguo la wananchi ndilo litatumika nadhani hii itasaidia zaidi kuondoa hata ndoto za kugombea ikiwa umeshindwa kuwaridhisha wananchi wakati umepewa Ubunge ama kazi za chama..
Sema labda tatizo ni pale majina yameisha kusanywa na kuanza Uteuzi, hapo ndipo tunatakiwa kuangalia zaidi tunaweza vipi kuboresha mfumo wa uchaguzi ili kuondoa Makundi na kujuana maana hii asili yetu haiwezi kuondoka kirahisi hata siku moja.. Jinsi gani tunaweza kuboresha uchaguzi nchini ndio mjadala mzuri kuliko kulaumiana.